[wanabidii] Ningekuwa mim ni EL nisingesema yale kwa wahariri wa vyombo vya habari

Wednesday, May 27, 2015
• Ningekuwa mim ni EL nisingesema yale aliyosema Jana na wahariri kwa sababu
hayabebi ile dhana ya 'presidential material':

1. Ningeshukuru CHAMA kwa hatua ya kutuweka huru na kuruhusu kuingia ktk mchakato.

2. Ningewashukuru wanachama, viongozi na watanzania kwa ujumla wanaoniunga mkono kwa kuwa na subra ktk kipindi cha mpito na ambao walikuwa wanataraji kupokea maamuzi mazuri na ya busara vikao vya chama.

3. Ningeweka wazi nia,na dhamira ya kuomba ridhaa kwa wanaccm.

4. Ningesema kwanin nagombea.
kueleza mazuri yaliyofanyika ktk kipindi cha awamu ya 4 na kuyaendeleza.
malengo ya baadae na mikakati ya kushughulikia matatizo ya nchi yetu. kuanzisha mbadala wa kitaifa ili kukubaliana na muelekeo kuweka vipaumbele vya Taifa ktk uekelezaji wa bajeti ya 2016/17 mpka 2020. Mapendekezo yangu ni kuwekeza vya kutosha ktk na Elimu, kilimo, miundombinu na Afya.

5. Kuunda serikali makini yenye mchanganyiko wa namna zote wazee, Vijana na wanawake. Bila kujali msimamo wake kisiasa ndani ya CHAMA, dini, ukabila, na kuimarisha Muungano wetu.
6. Nina imani wanaccm wenzangu wataniunga mkono na nawahakikishia kuwa nchi yetu itapiga hatua ya maendeleo makubwa kwa kipindi kifupi kijacho kea kutumia Rasilimali Gesi, madini, viwanja, na kilimo.

7. Utawala wa sheria na kukuza demokrasia ndani ya CHAMA na katika nchi yetu.

Kuanzisha mjadala ,Lazima ujue kuwa ndani ya ccm unapoomba urais ndio unaomba au unatazamwa kwa sura ya kuja kuwa mwenyekiti wa CHAMA.

Sasa ukija na wasiotaka wahame?
Serikali legelege?
Tukapimwe afya?
Sihusiki na RICHMOND?
Noooooooooooooo
Hapana hapaswi kuwa defensive.
Nadhani jamaa zake kama akina watamfikishia ili aache mipasho aende kwenye mantiki flow'
Na aboreshe aafu yake ya washauri wa mambo ya matamko na hutuba.
Then kupunguza 'uchildish' wapambe wa hovyohovyo!

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments