[wanabidii] NGOMA AFRICA BAND KUTUMBUIZA MJINI BREMEN,UJERUMANI JUMAMOSI 30 MAY 2015

Tuesday, May 26, 2015

NGOMA AFRICA BAND KUTUMBUIZA MJINI BREMEN,UJERUMANI JUMAMOSI 30 MAY 2015
 
FFU Kulitingisha hekalu la UEBERSEE MUSEUM-Bremen,Ujerumani siku 30 May 2015

Bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya Ngoma Africa band almaarufu kama FFU-Ughaibuni yenye maskani yeke nchini Ujerumani,siku ya jumamosi 30 Mei 2015 bendi hiyo italitingisha hekalu la Uebersee Museum mjini Bremen,kuanzia Saa moja Usiku hadi kumekucha. Onyesho hilo la usiku usiokwisha limeandaliwa na utawala wa hekalu hilo la makumbusho la Uebersee Museum,ambapo utawala huo umeiomba bendi ya Ngoma Africa band kwenda kutumbuiza,kwa kuwa bendi hiyo ilitumbuiza mwaka 2013 na  kuvunja rekodi ya kuwavuta washabiki wengi kuliko bendi yeyote katika historia ya matamasha yafanyikao katika hekalu hilo.
Ngoma Africa band inayoongozwa na kamanda  Ras Makunja ni bendi pekee ya kiafrika yenye mvuto mkubwa barani ulaya,na washabiki wake wameipachika majina mengi ya kiusanii kama vile FFU-Ughaibuni,Viumbe wa ajabu  ANUNNAKI Alien's (himaya ya mazimwi wa Anunnaki), pia maarufu kwa majina kama Mzimu wa Muziki,na "Watoto wa Mbwa" . Ngoma Africa band pia inatajiri wa wanamuziki wenye vipaji vya hali ya juu wakiwemo yule mpiga solo mahiri Afande  Chris Bakottesa aka Afande Chris-B, Sanjint major Jo jo Sousa, wanamuziki chipukizi wengi walizalishwa na bendi hiyo ambayo inawanamuziki kumi.
Ngoma Africa band ilianzishwa mwaka 1993 na kiongozi wa bendi hiyo ambaye pia ni mtunzi wa nyimbo nyingi za bendi hiyo Ebrahim Makunja aka Kamanda Ras Makunja.
unaweza kuwasikiiza FFU


unaweza kujumuika nao pia at ngoma4u@gmail.com

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments