[wanabidii] Je kwa Dar es saalam kuwasha taa za mitaani na barabarani ni "Mission Impossible"?

Tuesday, April 14, 2015
Enzi za mwalimu Dar es salaam ilikuwa na Meya mmoja tu lakini taa za mitaani na barabarani zilikuwa zinawaka mpaka mtaa wa Manda ambao uko mafichoni kule Magomeni Mikumi.

Leo Dar es salaam ina Mameya wanne lakini mji uko gizani. Je tatizo ni nani wa kugharimia luku au uwezo wa Mameya wetu kiutendaji umefikia kikomo? Mbali na giza, mji wa Dar es salaam umejaa takataka kila kona na mitaro inayomwaga maji machafu barabarani.

Hebu niambieni wanabidii wezangu mlio karibu na hao waheshimiwa, tatizo ni nini? 

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments