Sent from my iPad
Begin forwarded
Subject: Sayyid Majid Bin Sultn.
Sayyid Majid Bin Sultn.
(Na. Dkt.Muhammed Seif Khatib)
Miaka 153iliyopita,ardhi ya Tanzania Bara wakati huo ikiitwa Tanganyika katika kijiji cha wavuvi cha Dar es Salaam kilichokuwa kikijulikana kwa jina la Mzizima kilipata mgeni aitwaye Seyyid Majid Bin Said Bin Sultan.Ni mtoto Sultan Seyyid Said Bin Sultan kati ya
watoto wake 36 aliozaa.Seyyid Said ni Sultan wa Oman, Muscat,Zanzibar na Mwambao
wa Afrika ya Mashariki na visiwa vyake wakati huo.Sultan huyu baba, ndiye aliyewafurusha Warenu huko Mombasa walipokuwa wamejichimbia katika ngome zao 1837.Kabla yake aliiteka kisiwa cha Pemba huko Zanzibar Warenu walipokuwa na ngome
pamoja na Unguja .Mwaka 1832 Sultan Seyyid Said Bin Sultan El -Busaidy aliyafanya
Makao Makuu yake ya utawal yawe Unguja Mjini kutoka Muscat.Baba huyu alifariki
katika meli wakati anarudi Muscat na kuzikwa kwa siri usiku hapo Zanzibar katika Kasir
yake.Kifo hicho kikafungua ukurasa mpya wa utawala kuendeleza Usultani kwa kugombania mamlaka kwa watoto wake.Hatimaye watoto wake Seyyid Said wawili kati
ya 36 wakagawana mamlaka ya Zanzibar na Oman. Mtoto mmoja aitwaye Thuwein Bin
Said akatawala Oman na mwingine Majid (1856-1870) akatawala Zanzibar.Watoto wake wengine waliowahi kuitawala Zanzibar ni pamoja na Barghash bin Said (1870-1888),Khalifa bin Said (1888-1890),Ali bin Said (1890-1813).Mgeni huyu asiyealikwa
Seyyid Majid Bin Sultan baada ya kutawazwa Zanzibar kuwa Sultan hapo tarehe 19 mwezi
wa Oktoba mwaka 1856 akaanza kupanua mamlaka yake.Miaka sita tu baada ya kukaa
katika kiti chake cha Usultani mwaka 1862 akatia nanga katika kijiji cha wavuvi cha Mzizima. Baada ya kuvutiwa na mandhari nzuri ya mchanga mweupe wa ufukwe,miti ya
kila aina na upepo mwanana,akaamua aweke maskani yake pia.Bila ya shaka mengi
yamemvutia ikiwemo mimea ya vyakula vya kila aina, ukarimu wa wavuvi ukihitimishwa
na amani na upendo.Bila kuchelewa Mzizima baada ya kumzizima mgeni asiyetarajiwa wala
kualikwa akaibatiza Mzizima ya wakati huo kwa jina zuri lenye mvuto na raha na starehe
na kuita kwa lugha yake ya Kiarabu ya Dar Es Salaam.Nini maana yake?
' Pepo Ya Amani' au 'Paradiso ya Amani'.Seyyid Majid hakubatiza tu lakini pia Mzizima na
na eneo kubwa la Tanganyika na kuwaweka 'Maliwali' wake sawa na Magavana.Maliwali
wake waliwekwa katika visiwa vyote vya Mwambao vikiwemo Kilwa, Pate,Mafia, Lamu
pamoja na miji kadha ya mwambao na ndani ya Tanganyika hadi Kindu huko Kongo.Huyu
Majid alikuwa Sultani wa kwanza kuitawala Zanzibar,Sehemu ya Tanganyika,Kenya na
Kongo.Huu ulikuwa 'Muungano' wa nchi nyingi ulioletewa kwa ncha ya upanga wake.Hauna ridhaa ya watu, viongozi,au wawakilishi wa vyma au mataifa ya nchi zao.Ni 'Muungano'
wa mtu mmoja mwenye uroho wa madaraka na uhodhi wa mali na rasimali za watu.Siyo
'Muungano' uletao tija kwa umma katika kuwaletea maendeleo na kuwatatulia matatizo yao.Yeye kiongozi alikuwa 'Seyyid' kwa maana ya 'Mtukufu' au ' Bwana' na wale wanaoishi
katika mamlaka yote ya nchi hizo ni ' Raia wa Sultan'- ni mali yake yeye.Kodi yote ile
inayokusanywa na Maliwali hupelekewa yeye Seyyid Majid. Mwezi wa Oktoba tarehe
Saba mwaka 1870, Seyyid Majid akafariki na kurithiwa na nduguye Seyyid Barghash. Mwaka 1964, ulipoasisiwa Muungano wetu, imepita miaka 102 tangu 'Muungano' wa
wa kulazimishwa usiokuwa na ridhaa wala mkataba wa kimaandishi ulipoasisiwa na mtu
mmoja tu kwa matashi na tamaa yake. Siye mwingine ila Seyyid Majid Bin Said Bin Sultan.
Lakini miaka 51 iliyopita Muungano wa kweli uliasisiwa.Ni Muungano uliotokana na ridhaa
ya watu wa Mtaifa mawili Huru.Muungano uliopitishwa na kuridhiwa na mbaraza mawili
halali ya kikatiba ya Baraza la Mapinduzi,Baraza la Mawaziri na Bunge. Muungano
ulioridhiwa na viongozi wa vyama vya kizalendo,kimapinduzi na ukombozi vya TANU na
ASP.Muungano ulioasisiwa na viongozi wa dola mbili halali zilizotambuliwa na kukubaliwa
na vyombo vya kimataifa.Muungano uliohalalishwa kwa taratibu za kisheria za kuwekwa saini na Marais wa nchi mbili nao Rais Abeid Amani Karume na Rais Julius Kambarage
Nyerere.Muungano unaothamini na kuheshimu kila upande wa Muungano.Hakuna mdogo hakuna mkubwa. Hakuna 'Seyyid' hakuna 'Maulana' hakuna 'Mtwana' hakuna ' mjakazi'.
Muungano uliojengwa juu ya usawa na haki ya kila upandehakuna mtawala wala mtawaliwa
Muungano uliojengwa katika kuwaendeleza wananchi wa dola shirika na sio wa kuwaweka
'Maliwali' kama wanyapara na wakusanyaji wa kodi kwaajili ya manufaa na masilahi ya
'Seyyid'.Bila ya shaka kutokana na misingi mizuri na dhamira njema ya kisiasa iliyopo leo
tunasherekea nusu karne ya uwepo wa Muungano. Wakati tunasherehekea Muungano
wetu na kwa sababu za kihistoria ,wengine tunamkumbuka Seyyid Majid Bin Said
El -Busaidy kwa kujaribu 'kuunganisha 'Zanzibar na Tanganyika pamoja na Kenya na Kongo mwaka 1862.Leo ni zaidi ya miaka 153 imepita sawa na karne moja nusu.Muungano wetu Tanzania siyo wa masilahi ya 'Seyyid' bali ni wa wananchi,kwa sababu hiyo na udumu.
L
Sent from my iPad
0 Comments