[wanabidii] KWELI TUTAFIKA KWELI KWA ADA KUBWA NAMNA HII?

Sunday, February 08, 2015
Hivi kweli ni sahihi shule ya awali kulipia ada ya Tshs.1,200,000/= na zaidi kwa mwaka? Kweli hii hali ya kupandisha watoto wadogo kwenda kusomea shule za mbali itaisha? Kama shule ya karibu ada hiyo hiyo. Hivi hizi shule binafsi nani anadhibiti ada ada zake? Kila shule na ada yake kweli tutafikia BRN? Ni wakati umefika sasa pawepo na chombo cha kupanga ada za shule za binafsi kulingana na huduma inayotolewa. Hebu wanaohusika walivalie njuga swala hili! Au hili nalo linasubiri Rais Ajaye? Aaah hebu wanaohusika wawajibike!

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments