[wanabidii] Fwd: Chafya!

Sunday, February 08, 2015


Sent from my iPad

Begin forwarded message:

From: Muhammedkhatib <muhammedkhatib@yahoo.co.uk
Subject: Chafya!

                 Chafya!
(Dkt.Muhammed Seif Khatib)
 Nini chafya? Ni hewa inyosukumwa kwa nguvu kutoa puani kutokana na
kukeketwa au mwasho unaosabababishwa na vumbi au mafua.Jee ikitokea
hali hiyo wnyewe Waswahili huitaje? Kupiga chafya! Wengine nahau hiyo
huita enda chafya.Chafya haichaguwi humwendea mtu ye yote. Si mkubwa si mdogo si mume si mke.Chafya haina muda maalum wa kumvamia yoyote yule
imtakaye.Yaweza  kuwa alfajiri sana ama usiku wa manane.Wala haina miongo ya Vuli au Kaskazi.Chafya haina adabu wala heshima huweza kumtokea mtu
mbele ya mame mume au baba mkwe. Lakini chafya si maradhi bali ishara ya
uzima na afya.Hukuwahi kusikia wewe endaye chafya huambiwa 'afya'? Kwa
baadhi ya Wazungu au wale Waswahili wapendao uzungu ikitokea ukenda
chafya mbele yake hukwambia ' Mungu akubariki'. Nini maana yake ?Aanakupenda  na anakuombea Mungu uishi muda mrefu na uwe na afya kamili.
Vyama vya siasa kama viumbe vyenye uhai.Vinazaliwa,vinalelewa,vinakuzwa
na kuimarisha.Hujui kama vipo vyama vichanga vinavyoenda tata?Vipo vyama vikongwe vinavyoendea mkongojo?Vyengine vigonwa vipo
vitandani vimahututi na vinapumulia mashine?Lakini vipo vyama vikomavu
vyenye uzoefu vina viongozi weledi.Chamatawala kilichoongoza nchi hii
tokea kudai uhuru hadi leo.Sasa ni nusu karne kipo madarakani.Kilichotokea
Jumapili iliyopita kule Songea ni chama hiki kilipopata baraka ya kwenda
chafya mbele ya halaiki ya watu.Hii ilitokana na kupatwa mkeketo wa
uchaguzi.Chafya ilikuwa ishara ya uhai na uzima wa chama hiki.Chafya
iliashiria kutoa gesi chafu iliyokwisha tumika mwilini na kuingiza gesi safi ya
osigini.Nini matokeo yake? Tulikumbushwa kuwa nchi yetu itakuwa na
uchaguzi Oktoba mwaka huu. Huu utakuwa Uchaguzi Mkuu wa Tano wa
vyama vingi. Miaka kumi ilihudumiwa na Rais Mkapa na miaka kumi
mingine imehudumiwa na Rais Kikwete.Chafya ilitukumbusha kuwa uhai
wa taifa la Tanzania unategemea nahodha mweledi wa Taifa hili.Amani,
utulivu,utangamano na usitawi wa Tanznia unategemea rubani mahiri.Nani
nahodha na rubani? Ni yule atakayepewa jukumu la Urais wa Tanazania
na kuongoza nchi Oktoba mwaka huu.Waisilamu wakitaka kufanya
marejeleo ya mwenendo mzuri hurejelea kitabu chao Kitukufu Kurani
na maonyo ya Nabii Muhammad.Nao Wakristo wakitaka kufnya rejea
hurudi kwenye kitabu kuitakatifu cha Biblia na mahubiri ya Nabii Issa.Huko
kwa imani zao ndiko kwenye uongofu na ruwaza njema.Hata waumini hawa
wanapokabiliwa na mambo mazito hutakiwa kurejea katika vitabu vyao na
Manabii wao kupata mwongozo.Katika utamaduni wa Waswahili huelekezwa
kuwa wafate methali inayowataka watafute busara za wazee.Wanambiwaje?
' Isokongwe Haivushi'! Mkitaka kuvuka salama katika ziwa,mto au bahari
watafuteni wazee wakupeni busara na hekima.Watanzania wanataka kuvuka
'Mto au bahari ama ziwa?'Ndiyo! Uchaguzi Mkuu upo Oktoba.Si maji mafu
ya kuvuka kwa kihori na mashua.Wanataka busara zaa waee.Ndipo hapo
Watanzania wanpohitaji wasia watu wenye busara na hekima.Kama Wakristo
na Waisilamu wanao watu wa kupata hekima nao Watanaznia bila kujalii
imani ya dini, rangi,kabila, eneo na itikadi ya vyama wanao watu wa kupewa
rejea.Ni baba wa Taifa Mwalimu Nyerere anatwambia nini kuhusu uchaguzi
wa Oktoba mwaka huu? Rais anaweza kutoka katika chama chochote cha
siasa.Lakini Rais Bora atatoka ndani ya Chama cha Mapinduzi.Anachomaa
nisha ni kuwa wanaotaka Urais wapo wengi.Na wala si kosa kwa vyama vya
siasa kutamani kuingia Ikulu.Hoja ni kuwa kupenda na kutamani ni jambo
jengine na kukubaliwa na kuweza ni jambo jengine.Wapendao Urais wengi
wamearibu nafasi hizo mara kadha wa kadha.Yupo mgombea Urais aliyeanza
na Mkapa miaka ishirini iliyopita na alishindana na Kikwete kwa vipindi
viwili.Yeye bado hauoni na uchavu.Atagombea tena mwaka huu.Wengin
wamegombea vipindi vitatu wengine viwili na wengine kimoja.Ama kwa
huko Zanzibar yule Maalim amegombea na baba yake Mzee Wakili,
akagombea na kaka yake Dr.Salmin,akashindana na mdogo wake
Amani na mwisho na jamaa yake Dr.Shein. Amekuwa katika mbio hizo za
kutaka kuingia Ikulu ya Zanzibar kwa muda wa miaka 35. Lakini huko
Ikulu ya Dar es Salaam inawaniwa na wengi kutoka vyama vya upinzani.Sina hakika
na uadilifu wa wagombea wao hao wanaotajwatajwa sasa.Wapo waliotimuliwa
katika uongozi wa kanisa kwa kukiuka kiapo na nadhiri ya ya Kanisa.Ni  
wenye kesi mahakamani za kugombania akina mama.Wapo wagombea vijana wa
mijini wanaolala na kushinda katika vilabu vya usiku.Ni vijogoo  visivyojali
kufukuzana na kuku makoo na matembe.Hawa wanaviota bungeni na nje Bunge.Wapo
wanaotumwia bila kujua kuwa wao ni maboya tu.Hawawashi hawazimi.Hawana kauli
hawana sauti.Wakiingia Ikulu watakuwa ni mamluki tu.Nadhani chafya iliyotokea
kwa Chama Cha Mapinduzi kule Songea kumtupa uhai na kutukumbusha kurejea
wasia wa Mwalimu kuwa Rais Bora atatoka ndani ya Chama Cha Mapinduzi na
si vyenginevyo.Wahenga walisema,'Iso kongwe haivushi'. Tukitaka tuvuke Oktoba
mwaka huu tufate wasia wa Mwalimu.



P




Sent from my iPad

Share this :

Related Posts

0 Comments