[wanabidii] PINDA NI MUHANGA WA VITA YA URAIS

Thursday, January 08, 2015

PINDA NI MUHANGA WA VITA YA URAIS.

*Kashfa ya sukari - MAJIBU.

Hivi karibuni kumekuwepo na taarifa ya uzushi ambayo imesambazwa kwenye mitandao ya kijamii na kwenye baadhi ya magazeti yenye kichwa cha habari "KASHFA YA SUKARI *Pinda ndani, * Masaburi amvaa Kinana"

Katika habari hiyo, inatajwa kuwa kuna ufisadi mkubwa katika mchakato mzima wa utoaji wa vibali vya sukari na kwamba, Waziri Mkuu Mizengo Pinda anatuhumiwa kuwa ni mnufaikaji mkubwa na mhusika namba moja wa ufanikishaji wa ufisadi huo.

Pamoja na kuhusika kwa Mhe Pinda pia, habari hiyo inataja kuwa Janeth Masaburi, mfanyabiashara Turki, Zacharia, Mohamed Enterprise pamoja na Didas masaburi ni wahusika wa moja kwa moja katika ufisadi huo;

Kwa kuwa habari yenyewe ni ya kutungwa, uongo usiomithilika na ya kipuuzi hatukuipa umuhimu wowote kwa mara ya kwanza, lakini kutokana na kusambaa kwake na athari zinazoendelea kujitokeza hasa kwa kuendelea kuchafuka kwa jina na hadhi kwa Mhe Waziri Mkuu lakini pia kwa maslahi na heshima ya viongozi wengine wa Chama na Serikali pamoja na wafanyabiashara waliotajwa katika habari hiyo tumeona umuhimu wa kuitolea ufafanuzi na kuwaeleza watanzania ukweli halisi na kupinga upotoshaji, uzushi na uongo uliyomo kwenye habari hiyo;

@ Ktk habari hiyo inatajwa kuwa tarehe 13th July 2014, Bwana Turki (mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM kutoka zanzibar) alikabidhi fedha taslimu kiasi cha Bilioni 4.13Tshs, kwa Bwana Didas Masaburi (mpiga kampeni wa Pinda), katika hotel ya PEACOCK.

--> Majibu ya hoja hii ni kama ifuatavyo:-
1. Ndugu Hassan Turki, si mjumbe na hakuwai kuwa mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM kutoka Zanzibar.

2. Tarehe tajwa hapo juu yaani 13th July 2014, Waziri Mkuu Mhe Mizengo K. Pinda alikuwa bado hajatamka nia yake ya kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hivyo hakuna ukweli wowote kuwa Mhe Pinda alikuwa akimtumia ndugu Didas Masaburi kama mpiga debe wake.

3. Kiasi cha fedha bilioni 4.13 ni kikubwa sana, makabidhiano ya kiasi hicho cha fedha kufanyika katika hotel tena katika mfumo wa fedha taslimu ni uongo mwingine wa dhahiri, ambao kila mmoja anaweza kuushuhudia.

@Katika habari hiyo imetajwa kuwa, mnamo tarehe 8/9/2014 ndugu Janeth Masaburi akiongozana na Kijana anayeitwa Mole (kijana wa Maswi wa ESCROW) walifika katika ofisi za Kwanza Limited, Kampuni Tanzu ya Mohamed Enterprise, eneo la Kamata na kukabidhiwa milioni 900.7 tshs.

--> Hii ni hoja nyingine dhaifu, kwani taarifa hiyo inataka kuliambatanisha suala hili na Escrow, jambo ambalo halihusiani kabisa lakini pia taarifa hiyo haisemi fedha hiyo ilitolewa kwa ajili ya kazi gani au makubaliano yapi.

@Habari hiyo ya uzushi pia inataja kuwa mnamo tarehe 22 Nov 2014, Ndugu Turki alitoa kiasi cha Bilioni 3 kwa ajili ya salamu za X-mass na mwaka mpya, ambapo kila mjumbe wa Halmashauri Kuu alipewa kiasi cha shilingi laki 8 (800,000tshs) na wajumbe wa mkutano mkuu kiasi cha shilingi laki 4 (400,000) na kwamba fedha hiyo alikabidhiwa Ndugu Didas Masaburi kupitia akaunti yake namba 01j2692311300 iliyopo Tawi la Azikiwe, CRDB.

--> Tuhuma hizi zinaonyesha udhaifu mkubwa unaotokana na kukosa hoja zenye msingi wa kihisabati, wajumbe wa NEC jumla yake ni 327 na wajumbe wa mkutano mkuu hawazidi 2300. Kwa kiasi cha uwiano wa laki 8 na 4 kwa kila mjumbe, haiwezi kutumika hata nusu ya Bilion 3.

Lakini udhaifu mwingine wa hoja hii ni ushahidi kuwa hakuna mjumbe hata mmoja wa Halmashauri kuu ama mkutano mkuu aliyepokea hata elfu 20,000 tu kutoka kwa Mhe. Pinda kwa ajili ya X-mass na Mwaka mpya.

Pamoja na hayo, ndugu Didas Masaburi hana na hakupata kuwa na akaunti katika tawi la azikiwe, CRDB yenye namba hizo tajwa.

Ama juu ya kauli za Ndugu Masabiri kuwa amemtuhumu Ndugu Kinana (Katibu Mkuu wa CCM) na Mwenyekiti wa chama hicho Mhe Jakaya Kikwete kuwa wamemuandaa MAGUFULI kuwa mgombea wa CCM na Rais wa Awamu ya tano ni ngonjera isiyohitaji kiitikio, hakuna namna ya kulijibia hili isipokuwa ni kulipuuzia, ni upuuzi unaopaswa kupuuzwa.

Huu ni muendelezo wa siasa chafu, zinazofanywa ili kuharibu hadhi na sifa za wengine. Ni upuuzi na ufedhuli kutunga uongo ili kumchafua mwengine, na kama PINDA anatafutwa katika kesi ya RUSHWA kwa namna hii, basi HATOPATIKANA.

Pamoja na maelezo haya ambayo yanatoa ufafanuzi katika tuhuma hizo za kutunga, bado wahanga wa uongo huo wanayo haki ya kisheria ya kufungua kesi na kuwashitaki wale waliohusika ktk kutunga na kusambaza uzushi na uongo huo wenye kulenga kuwafedhesha na kuwavunjia heshima waliyonayo mbele ya jamii.


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments