[wanabidii] Dawa zilizofutiwa usajili na TFDA kwa matumizi ya binadamu

Saturday, January 24, 2015
Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini Tanzania (TFDA) imefuta usajili wa aina tano za dawa za binadamu na kuamuru ziondolewe sokoni na vituo vyote vya kutolea huduma za afya mchini kote mara moja kutokana na kubainika kuwa zina viambata vinavyosababisha maradhi sugu ikiwemo kiharusi, na wakati mwingine kusababisha vifo.

Dawa zinazotajwa kufutiwa usajili na kuzuia uingizwaji kuwa ni pamoja na dawa za kutibu malaria ya maji na vidonge, dawa za kutibu mafua na kikohozi za maji, vidonge na kapsuli (capsules) zenye kiambata cha Phenylpropanolamine. Nyingine ni dawa ya sindano aina ya Chloramphenicol inayotengenezwa na kiwanda cha Lincoln cha nchini India na dawa za kutibu ukungu (fungus) ya vidonge na kapsuli.

Akitangaza dawa hizo mkurugenzi mkuu mamlaka ya chakula na dawa TFDA Bw. Hiit Sillo amesema hatua hiyo imefikiwa baada ya uchunguzi wa kitaalam wa muda mrefu kwa kutumia mifumo ya ufuatiliaji wa usalama na ubora wa dawa ambao pia unafanya kazi kwa kutumia mtandao wa kimataifa kwa ushirikiano na Shirika la Afya Duniani (WHO).

Aidha, TFDA imefanya mabadiliko ya matumizi ya dawa ya malaria ya SP kutumika kama kinga ya malaria kwa wanawake wajawazito tu na kuagiza watengenezaji kubadili machapisho na vifungashio vyake mara moja ambapo Mkurugenzi wa dawa TFDA, Bw. Mitangu Fimbo pamoja na kufafanua athari, anawataka watoa huduma nchini kote kuondoa dawa hizo na kuziteketeza mara moja kabla ya kuanza kwa msako.

Dawa aina Tano zilizofungiwa ni:-
  1. Dawa ya kutibu fungus ya vidonge na kapsuli aina ya Ketoconazole
  2. Dawa ya kutibu Malaria ya maji na vidonge aina ya Amodiaquine (Monotherapy)
  3. Dawa za kutibu mafua na kikohozi za maji, vidonge na kapsuli zenye kiambato hai aina ya Phenylpropanolamine
  4. Dawa ya kuua bakteria ya sindano aina ya Chloramphenicol Sodium Succinate inayotengenezwa na kiwanda cha Lincoln Pharmaceuticals Ltd, India
  5. Dawa ya kuua bakteria ya maji na kapsuli aina ya Cloxacillin

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments