[Mabadiliko] Uchambuzi Wa Habari: Ukawa Wamerusha Karata Ya Hatari...

Saturday, January 24, 2015


Ndugu zangu,

Nimesoma tamko la UKAWA juu ya kususia kura ya maoni Aprili 30.

Siasa kama mchezo wa karata wakati mwingine anayecheza hubaki na karata ambayo anapoirusha huleta matokeo mawili; ama kubaki mchezoni au kuondoka.

Na kwenye siasa karata nyingine ni za hatari. Nionavyo, katika hili la Kura ya Maoni, Ukawa wamerusha karata ya hatari. Wanaweza kupoteza kwa hoja moja kuu;
Kuwa Sababu zinazotolewa na UKAWA leo za kususia kura ya maoni zinaonyesha kutokuwepo na uwajibikaji wa kiupinzani.

Mara nyingi tunafikiri ni chama tawala na Serikali ndizo zinazopaswa kuwajibika. Upinzani pia unapaswa uonyeshe uwajibikaji hata kwenye dhana ya upinzani.

Na hiyo isitafsiriwe kuwa wajibu wa upinzani ni kupinga tu kila linalofanywa na Serikali na Chama tawala.

Ona mfano huu wa Profesa Lipumba akinukuliwa na gazeti la Mwananchi akisema; Kuwa pamoja na kutangazwa kwa siku ya kupiga kura bado uandikishwaji wa daftari la wapiga kura haujaanza kwa sababu wanasubiri vifaa.

Sasa hapa inaonyesha tatizo ni maandalizi na sio uhalali wa jambo lenyewe.

Jambo lingine ni ukweli kuwa mchakato mzima uko kisheria na sheria hazikupitishwa Ikulu bali Bungeni.

Kama kuna udhaifu katika mchakato mzima na sheria yenyewe, basi, Ukawa walipaswa kuwajibika kiupinzani kwa kuyafanya mawili; 
kutumia bunge kujenga hoja za kupinga, na pia njia za mazungumzo nje ya bunge. Na si kukimbilia kususia kura za maoni leo hii wakati wananchi wanajua pia kuwa Ukawa ilishiriki kupitisha sheria na kanuni ambazo leo ndizo zimetufikisha hapa.

Kimsingi hii ni moja ya changamoto ya siasa za vyama vingi kwenye nchi yetu.

Watanzania wanahitaji uwepo wa siasa za vyama vingi hivyo kuleta ushindani wa kisiasa. Na hatimaye kuharakisha maendeleo.

Wasiwasi wangu, isifike mahali Watanzania wakadhani siasa za vyama vingi maana yake ni siasa za kulalamika tu, kususia tu, kugoma tu, kuandamana tu na mengineyo yenye kufanana na hayo.

Isifike mahala Watanzania wakachoshwa na siasa za upinzani.
Maggid,
Dar es Salaam.

http://mjengwablog.com

--
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
 
 
For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Mabadiliko Forum" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
To post to this group, send email to mabadilikotanzania@googlegroups.com.
Visit this group at http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania.
To view this discussion on the web visit https://groups.google.com/d/msgid/mabadilikotanzania/CAMD-ye7mBHrfMR6rchN61oTeA%3DVYVYiUbdsUJA1JCbVwU9Q5yQ%40mail.gmail.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments