Ndugu zangu,
Ni usiku wa kwanza katika siku ya kwanza ya mwaka mpya. Duniani hapa, kama kiumbe hakikui, basi huanza kudumaa. Na mimea vivyo hivyo.
Lakini, mara nyingi wanadamu huwa hatujiangaishi kujiuliza swali muhimu; kwanini mwanadamu anaacha kukua, au kwanini mmea unaacha kumea?
Mwanadamu unaweza kumaliza ndoo za maji kuumwagilia mmea na wala usimee. Kumbe, mche uliopanda una gugu kando yake. Gugu ndio lenye kunyonya vyote, maji na rutuba.
Na maisha yetu haya tunayoishi, yumkini tunaishi na magugu kando yetu. Ni wanadamu wenzetu wenye kutufanya tusimee, tusichanue. Ni kwa hila, wivu na choyo zao. Ni hao wenye kuhangaika na kutia fitina kwa kila unachofanya. Kimsingi, hawapendi uchanue. Yawezekana akawa ni rafiki yako, au anayejifanya kuwa rafiki yako. Yawezekana akawa ni mwenza wako anayejifanya anakupenda, kumbe hapendi hata kumwona anayempenda akimea na kuchanua!
Na katika maisha, mwanadamu huna namna yoyote isipokuwa kujenga ujasiri wa kuondoana na magugu yanayokuzunguka. Vinginevyo, utabaki kudumaa. Hutamea wala kuchanua.
Ni Neno Fupi La Usiku.
Maggid,
Iringa.
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Mabadiliko Forum" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
To post to this group, send email to mabadilikotanzania@googlegroups.com.
Visit this group at http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania.
To view this discussion on the web visit https://groups.google.com/d/msgid/mabadilikotanzania/CAMD-ye4nGGH0pr2sfsWjQJFrt0LV2-U0jd3UW36%3DuojJLvEOtw%40mail.gmail.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments