Na Happiness Katabazi
WALE wazushi,Visarata Mtaa,Washambenga,wenye nongwa Kama ndugu wa mume ambao Katika zogo la Escrow,walimu hukumu Waziri wa Nishati na Madini, Professa Sospiter Muhongo Kuwa ni Muhongo kama jina lake na kwamba ni fisadi wa Escrwo Leo hii wameziweka wapi sura zao?
Licha ya Profesa Muhongo kutoa utetezi wake kupitia hotuba yake ndani Bunge ambapo pamoja na mambo mengine ,msomi Huyo alisema Fedha za Escrwo siyo za umma watu wakiwemo wanasiasa uchwara ambao ni wabunge walimpinga na kumuhukumu Kuwa ni Muongo mkubwa Kama jina lake na kwamba Fedha za a Escrow ni za umma.
Lakini Jana Baba mwenye nyumba nyumba, Profesa Jakaya Kikwete katika hotuba yake alikubaliana na Muhongo Kuwa Fedha zile siyo za umma ni za IPTL na hazijaibwa wala Kubebwa kwa Magunia Kama Zitto Kabwe wakati akisoma ripoti ya PAC bungeni alisema Fedha za Escrow zilibebwa kwa Magunia bila kufuata Taratibu ya Sheria ya Benki Kuu.
Waswahili wanamsemo wao usemao ' Mnafki hafi hadi ameumbuka'. Hivyo wanafki,Majaji mama DDP ,DCI ,majaji ,Mashushushu wa 'Kichina' ,mabush Lawyer ,wazushi na mahakimu uchwara ambao mlijipachika majukumu yasiyo ya kwenu ya kuhukumu Watu na kuwaita wakina Muhongo ni wezi ,wamekula Rushwa ,wamechota Fedha ya umma ya Escrow hotuba ya jana imewaumbua.
Naendelea kusisitiza tuache tabia ya kuhukumu au kushabikia jambo wakati Hatuna vielelezo Vya kutosha Kwani tukae tukijua uzushi unaumuiza watu wasiyo na hatia Katika baadhi ya mambo machafu wasiyo yatenda.
Leo hii kila kona watu wamepandikizwa chuki Mbaya sana ambapo baadhi ya wananchi ambao wao wakisikia jambo hawataki kilifanya utafiti wanaliamini, wanaamini Muhongo ni fisadi, kaiba Fedha za Escrow Kumbe ni uzushi tu unafanywa na wahuni wachache kwa Malengo Yao binafsi.
Narudia tena Kusema naipongeza hotuba ya Jana ya Rais Jakaya Kikwete Kwani kwa MTu mwenye akili timamu, na aliyekuwa na kiu ya kutaka kufahamu ukweli kuhusu zogo la Escrow ametambua ukweli ni upi na Kamati ya PAC inayoongozwa na Zitto Kabwe kuna baadhi ya mambo iliyopo tosha.
PAC ilipotosha umma Katika ripoti yake ilisema Kiwango Cha Fedha kilichokuwa kwenye Akaunti ya Escrow ni Sh.Bilioni 306.7. Wakati ukweli ni kwamba kiasi kilichokuwa kwenye Akaunti ya Escrow ni Bilioni 202.9. PAC ilisema Fedha za Escrow ni za umma, Rais amewaumbua amesema siyo za umma ni za IPTL.
Hali iliyosababisha wananchi kuwajengea Chuki ya wazi wakina Muhongo, Profesa Anna Tibaijuka, Katibu Mkuu Eliachim Maswi na aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa serikali Jaji Fredrick Werema ,CCM na serikali kwa ujumla Kuwa Si wazalendo kwa taifa na hao PAC na uongo wao Katika baadhi ya ripoti Yao ambayo imebainika Kuwa na dosari ndiyo wazalendo wa kweli.
Kwa hotuba ya jana naweza kusema Tibaijuka amepata hati yenye Mashaka, Muhongo,Maswi wamepata hati safi. Kwa hiyo Hakuna Ofisa wa serikali aliyetaja hati chafu.
Kamati ya PAC mlipewa Fedha za walipa kodi mkafanyekazi kazi ya uchunguzi Matokeo yake mmekuja na ripoti ambayo baadhi ya uchunguzi wake mlikusanya vielelezo Vya uongo ambavyo viliingiza taifa kwenye zogo. Kama ni Waungwana, Ombeni radhi kwa watanzania kwa Udhahifu huo ili tuendelee bila kuitilia Shaka Kamati yenu siku za usoni .
Hakuna rufaa tena Escrow na mjadala wa Escrow hapa duniani uliotungwa na Rais Kikwete rasmi jana , nafasi iliyobaki ya kujadili Escrow labda ni mbinguni ambako huko hatuna mamlaka nako.
Atakaye pinga hotuba yake kwa sasa atakuwa anapinga na rais na anaweza kuhesabika ni mtu anayehatarisha usalama wa nchi maana ki ukweli Rais ndiyo kiongozi juu wa Tanzania na ameishasema kuwa fedha za Escrow siyo za umma ni za IPTL.
Mnaolazimisha kuwa fedha za Escrow ni za umma endeleeni kulazimisha, ila haitawasaidia maana tayari mjadala huo Baba mwenye nyumba yaani Rais Kikwete aliufunga mjadala huyo kwa kusema fedha za Escrow siyo za ummma.
Waliomuita Profesa Muhongo ni Muhongo Kama jina lake kwasababu eti alisema Fedha za Escrow Si za umma, ni dhahiri shahiri hotuba ya jana imewaumbua. Mabingwa wa fitna kajipageni upya ili tukianza Mwaka mmoja muibuke na jungu jingine mAana shughuli kubwa mnayoifahamu ni kuwazushia wenzenu uongo.
Binafsi naamini ipo siku ushauri wa kisheria uliotolewa na aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali,Jaji Werema utakuja kueleweka ,ni suala la muda. Mungu ibariki Tanzania.
Chanzo: Facebook: Happy Katabazi
Blogg. www.katabazihappy.blogspot.com
0716 774494
Disemba 23 Mwaka 2014
Sent from my iPad
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments