[wanabidii] TUPE TATHMINI YAKO KUHUSU UCHAGUZI WA LEO!!

Sunday, December 14, 2014

TUPE TATHMINI YAKO KUHUSU UCHAGUZI WA LEO!!

Kwa taarifa nilizonazo, hadi sasa wilaya kibao mno uchaguzi haueleweki. Maeneo kibao tu hakuna wino wa kuweka vidoleni ili kuzuia watu wasirudie kupiga kura, maeneo mengine hakuna karatasi za kupigia kura wala masanduku. Maeneo mengine hakuna wasimamizi na vituo havijafunguliwa hasi saa 7 mchana huu.

Uchaguzi huu unasimamiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu na TAMISEMI, ni uchaguzi wa kihuni sana kuliko hata ule wa 2009, yaani ni kama demokrasia inakwenda rivasi.

Baada ya CCM kupitia wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya, wakurugenzi wa halmashauri, madiwani na wabunge wao kuweka mikakati dhahiri ya kuwawekea wapinzani mapingamizi ambayo mengi yamekubaliwa na kamati za rufaa ambazo nazo zinaundwa na watu walewale, na hivyo kupelekea wagombea wa CCM kusimama bila ushindani katika maeneo mengi, nilitaraji kuwa haya maeneo yanayoshindaniwa kutakuwa na aibu basi walau haki iachwe itendeke, lakini taarifa zilizopo ni kwamba idadi kubwa tu ya kata uchaguzi umeahirishwa kwa sababu ati "vifaa vya uchaguzi havikuandaliwa".

Kama baadhi ya maeneo ya Dar Es Salaam hakuna karatasi za kupigia kura, hakuna wino n.k.(Maeneo ya mjini), ni vipi huko vijijini ambako maduka ya vifaa kama wino, karatasi n.k hayapo?

Popote pale ulipo, tujulishe sasa hivi nini kinaendelea katika Kitongoji chako, Kijiji Chako, Mtaa wako, kata yako, wilaya yako na mkoa wako kuhusu UPIGAJI KURA.

J. Mtatiro,
DSM.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments