[wanabidii] Rais Kikwete jiuzulu nafasi ya Uenyekiti wa CCM Taifa

Sunday, December 21, 2014
Kwa nini Rais Kikwete anastahili kujiuzulu nafasi ya uenyekiti wa CCM Taifa?

Kuna sababu ambazo zipo wazi kutokana na serikali ya CCM hii ya Rais Kikwete, kushindwa kuchukua hatua stahiki na kwa wakati, yakiwemo masuala ya ufisadi na CCM kuendelea kuporomoka umaarufu na kunyimwa kura kila kona ya nchi.

Sipendi kukuna mahala palipoacha kuwasha, lakini kama ilivyo kwa binadamu kutoweza kusahau historia, kule mkoani Mtwara, serikali yake iliwaachia makovu ya miili baadhi ya wananchi wa mkoa wa Mtwara.

Hakuna ubishi kuwa katika opareshini ya kutokomeza ujangili nchini baadhi ya wauza duka la CCM yaani watendaji wa serikali waliopelekwa kwenye oparasheni hiyo wameneemeka na kuwaumiza wananchi. Vivyo hivyo, operesheni Kimbunga na escrow.

Namshauri Rais Kikwete ajiuzulu nafasi ya uenyekiti wa CCM Taifa, ili amwachie mwingine arejeshe imani ya chama hicho kuelekea uchaguzi mkuu 2015, vinginevyo kauli yake ya kuwataka wana CCM kujiandaa kisaikolojia kushindwa, hakika itatimia zaidi na historia haitamwacha salama.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments