Marekani yaitumia kashfa ya Escrow kudanganya raia
Vyombo vya habari vimeripoti kwamba Marekani imetangaza kuzuiya zoezi la uwekaji saini la utoaji wa msaada wake kupitia taasisi yake ya Millennium Challenge Corporation (MCC) ikisubiri hatua zitakazochukuliwa na Tanzania kufuatia Kashfa ya Escrow.
Balozi wa Marekani Tanzania, Mark Childress alinukuliwa akisema kuwa Mkutano wa Bodi ya MCC mjini Washington umezuiya kwa muda mgawo wa msaada wa Tanzania wa kiasi cha $9.78 million (Sh16.14 billion) kwa minajili ya kusubiri matokeo ya Uchunguzi wa Kashfa ya Escrow. Na pia kuona mageuzi mengine ya kupambana na ufisadi hususan katika sekta ya nishati ya gesi.
Maoni
Marekani inaidandia kashfa ya ufisadi ya Tegeta Escrow ya TSh306 bilioni iliyogusa hisia za wengi kujionesha ati inajali maadili mema na inapinga vikali vitendo vya ufisadi na rushwa. Jambo ambalo ni uwongo wa mchana kweupee !
Miradi yote ya Marekani kupitia MCC na mengineyo si zaidi ila ni mikakati ya ukolonimamboleo ya kumakinisha ushawishi wake, kuwaghilibu na kuwaziba macho raia ili waone dola hiyo ina imani na raia na kuwajali. Ilhali kiukweli ni dola inayolazimisha maamuzi ya kisiasa katika nchi zote changa ikiwemo Tanzania. Kwa upande wa kiuchumi, makampuni yao makubwa (multinational companies) na makampuni ya madola mengine ya kibepari ndio yanayopora rasilmali za nchi hii kama wanavyofanya katika nchi nyengine. Lau ingekuwa Marekani inajali raia na wanadamu kwa jumla kwanza wangaliacha kutekeleza mfumo hatari na wa dhulma wa ubepari na kujiepusha kuwa mstari wa mbele katika kupora na kunyonya rasilmali za nchi changa kwa kushirikiana na wanasiasa mafisadi
Mfumo wa kibepari ambao ndio mfumo unaotabikishwa na dola ya Marekani unajali kipimo kimoja tu nacho ni maslahi pekee na sio zaidi. Kwa hivyo, mwito kwa kujifanya kuzuiya misaada yao kwa nchi changa kwa dhamira ya kukabilina na rushwa na ufisadi, hawezi kulikubali jambo hilo ila mjinga asiyeelewa mfumo huo.
Pamoja na tangazo hili la kiuwongo la Marekani kupinga rushwa na ufisadi na kashfa ya Escrow ili Marekani ionekane kigezo cha maadili mema na ustaarabu. Kila mtu amejionea wazi ripoti ya karibuni ya bunge lao la Senate juu ya mateso yanayofanywa na shirika lao la CIA kwa wafungwa wa Kiislamu. Kwa udhati yaliomo ndani ya ripoti hiyo ni machache tu ikizingatiwa kwamba ripoti hiyo wameitoa Marekani yenyewe. Aidha, kila mtu anajionea kushamiri vitendo vya polisi wa nchi hiyo katika mauwaji ya kibaguzi kama yaliyojiri karibuni ya kuuliwa Eric Garner na kupelekea maandamano makubwa nchini humo.
Marekani imeshindwa na kamwe haiwezi kuwa kigezo cha maadili mema na ustaarabu kutokana na ufisadi, mateso na ukatili, bila ya kutaja uporaji wao wa rasilmali za nchi changa.
Kutoka Afisi Kuu ya Habari ya Hizb-ut Tahrir
Imeandikwa na Masoud Msellem
Naibu Mwakilishi Kwa Vyombo Vya Habari- Hizb ut Tahrir Afrika Mashariki
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments