[wanabidii] Kikwete, Wanajeshi Wakerwa na Lowassa

Sunday, December 21, 2014

Na Charles Jabu, Arusha.

Jana kwenye Chuo Cha Maafisa wa Jeshi Monduli kulikuwa na Sherehe ya kuwatunuku wahitimu. Lowassa alialikwa kama Mbunge wa eneo hilo. Cha ajabu alijisogeza na kuhakikisha anapigwa picha na Rais ili picha hiyo itumike magazetini. Na kweli pesa nyingi imetumika kuichapisha picha hiyo kwenye karibu magazeti yote. Ajabu kubwa kwamba magazeti yote yanachagua picha inayofanana kuweka ukurusa wa mbele. Jambo hilo huwa halitokei labda picha hiyo iwe imelipiwa kama vile tangazo la biashara. Na hivyo ndivyo ilivyotokea.

Kitendo hiki kimewakwaza na kuwakera wanajeshi wote kuanzia makamanda wa ngazi za juu hadi askari wa kawaida. Wanaamini kwamba jana ilikuwa ni siku yao mahsusi na kwamba picha ambazo zingepaswa kutoka ni picha za tukio lenyewe. Wamekerwa na mtu anayetaka kuwa Rais kuweka siasa mbele na kushindwa kuheshimu Jeshi na siku muhimu kwa Jeshi.

Vilevile, maafisa wa Ikulu mapema leo Arusha wameelezea Rais kukerwa na tabia ya mara kwa mara ya Lowassa kutumia nafasi ya matukio ya kitaifa kupiga picha na Rais halafu kuzisambaza magazeti kujaribu kuonyesha umma kwamba yeye na Rais wako sawa wakati ukweli ni kwamba yeye na timu yake kwa miaka 7 iliyopita wamekuwa wanamsengenya Rais kwenye vikao vyao na kuihujumu Serikali yake hasa Bungeni. Ukweli unabaki kwamba pamoja na nguvu kubwa inayotumika Lowassa hatapitishwa na vikao vya Chama. Hatakiwi na Mwenyekiti, Hatakiwi na Katibu Mkuu, hatakiwi na Mangula, Hatakiwi na Mkapa, Hatakiwi na Malecela, hatakiwi na Msekwa. System nzima ya uongozi wa juu wa nchi haimtaki anakuwaje Rais? Na sasa Jeshi pia limemuona hana maana.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments