[Mabadiliko] Yatakayojiri leo mkutano wa Prof JK na "Wazee wa Dar"

Friday, December 19, 2014

Nami pia natabiri hii itatokea, wewe je?


Source JF
Dalili ya mvua ni mawingu. Kufuatia Prof JK kumpongeza Jaji Werema (aka TUMBILI) kwa uaminifu na utumishi uliotukuka, kuna kila dalili kwamba leo JK atawasafisha rasmi Prof Muhongo, Tibaijuka, Maswi na wezi wengine kwa kisingizio kwamba tumbili aliyewapotosha tayari ameishaachia tawi! 

Kuna uwezekano mkubwa kwamba kujiudhuru kwa Werema ni mbinu iliyobuniwa na utawala kwa lengo kuwasafisha wezi waliosalia. Prof JK atasingizia kwamba Werema ndiye aliyewaponza wezi wenzake kwa hivyo haoni haja ya kuwafukuza tumbili waliosalia kwa kuwa tumbili mkubwa kajitoa kichakani.

Ni dhahiri kwamba JK hakuwa na nia ya kumfuta kazi Werema. Kitendo cha Werema kukataa kukiri makosa yake huku akisifiwa na JK kwa uaminifu na utumishi uliotukuka ni ishara inayotosha kudhihirisha kwamba JK hakuwa na nia ya kumfukuza kazi mtumishi huyu mwadilifu (Werema) wala watukuka wenzake na hilo litadhihirika leo mbele ya "Wazee wa Dar".

Amini nawaambia hakuna mwizi hata mmoja atakayewajibishwa leo hii.Habari ndio hiyo!

Nawasilisha.

--
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
 
 
For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Mabadiliko Forum" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
To post to this group, send email to mabadilikotanzania@googlegroups.com.
Visit this group at http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania.
To view this discussion on the web visit https://groups.google.com/d/msgid/mabadilikotanzania/CACChgVQ8Tb0DO0JQCXiA01G1-sdaNeNeNqdJg4CJLHf_7Q52NA%40mail.gmail.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments