[Mabadiliko] CCM inafutikia mbali 2015!

Friday, December 19, 2014

Wadau,

Kwa mwenendo ulioonekana kwenye uchaguzi huu wa serikali za mitaa, CCM ijiandae kukabidhi madaraka kwa UKAWA ifikapo mwakani 2015.

Uchaguzi huu,  ambao bila aibu kwa serikali hii dhalimu, umesamamiwa tena na ofisi ya kada wa CCM (ofisi ya waziri mkuu) na kuvurugwa vibaya sana, lakini bado UKAWA umeonyesha nguvu kubwa na kufanikiwa kuyafutilia mbali mafisadi haya kwenye maeneo muhimu hapa nchini.

Pamoja na ofisi hiyo chini ya waziri Hawa Ghasia kuyageuka makubaliano ya uchaguzi huo kupewa maandalizi ya kutosha ikiwa ni pamoja na kuangalia uwezekano wa kuiachia tume ya uchaguzi kuusimamia, lakini pia iliandaliwa mbinu ya kuweka mikakati ya kuudhibiti UKAWA ili waweze kupita bila kupingwa kwa kuweka mapingamizi yasiyokuwa na tija, na pia kutoa muda mchache kwa wapinzani ili washindwe kusimamisha wagombea katika maeneo mengi nchini na hasa vijijini.

Lakini harakati zote hizi za CCM za kuhakikisha wanapata viti vingi na hasa vijijini na baadhi ya maeneo yaliyolala mijini, bado zinaonekana kuwatokea puani maana ni kama wamewasha moto wa mabadiliko huko. Pamoja na kushtukizwa na uchaguzi huu wa kihuni, lakini makamanda wamesimama imara kwa haraka sana na kuyafutilia mbali mafisadi haya katika maeneo ambayo siku za nyuma yalikuwa ni ngome ya CCM.

Kitendo cha kutupeleka kwenye uchaguzi huu kihunihuni namna hii kimeipa nchi picha ya nini sasa hivi kinachoendelea hasa tunapoelekea kwenye uchaguzi wa 2015. Nashindwa kujua CCM watapitia wapi tena na mapingamizi yao ya kijinga kwa wagombea wetu wa ubunge na udiwani maana waswahili husema, ukupigao ndio ukufunzao!

Mwaka 2015 mafisadi hawa watakosa pa kutokea, ni kipigo tu kuanzia kwenye udiwani mpaka urais; kila tunakopita kuna hasira kubwa kwa wananchi kutokana na uhuni waliowafanyia kwa kuwanyima fursa ya kuwachagua viongozi wao waliowekewa mapingamizi ya kipumbavu. Nashindwa kujua CCM wataiepuka vipi hasira hii ya wananchi hawa, twende tu polepole kuelekea uchaguzi wa 2015!

SA.

--
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
 
 
For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Mabadiliko Forum" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
To post to this group, send email to mabadilikotanzania@googlegroups.com.
Visit this group at http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania.
To view this discussion on the web visit https://groups.google.com/d/msgid/mabadilikotanzania/CAPPZ%3DWwUQ%3DySsXc%3DBeD4KD7cKw8M0XuMJkw-9u6Z6Pq2Y-BwNQ%40mail.gmail.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments