(Huyu mama ingawa ni msomi lakini anaonekana haelewi maana ya uwajibikaji)
1. Kwanza tu kitendo cha yeye kukiri wazi kwamba anajishughulisha na biashara za mashule wakati ana majukumu lukuki ya umma ambayo kwa kiasi kikubwa yeye na wizara yake ameshindwa kupata suluhisho la matatizo ya ardhi ni kuuthibitishia umma jinsi anavyokiuka maadili ya uongozi.
2. Mama Tibaijuka anashindwa kuelewa kwamba hata kama hakuchukua hela za umma lakini hela ya wizi imekutwa kwake hiyo ni ushahidi tosha kwamba na yeye ana ushirika na wezi.
3. Mkutano wake na waandishi wa habari umeandaliwa na wasaidizi wa wizara je, ni mkutano wa kikazi au binafsi??!! Kama ni wa kikazi ina maana anaitetea wizara kupewa 1.6b na Rugemarila, kama ni wa binafsi nani atalipa gharama na kwa nini uandaliwe na wizara??!! Kwa ufupi huu ni mwendelezo wa matumizi mabaya ya ofisi za umma.
*Lukelo Felix Mkami Mwipopo
(Computer Programmer/Facilitator)
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Mabadiliko Forum" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
To post to this group, send email to mabadilikotanzania@googlegroups.com.
Visit this group at http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania.
To view this discussion on the web visit https://groups.google.com/d/msgid/mabadilikotanzania/CAErTtmXGsOrhkgfX0w_QhAq0W18ZOMKB72SOWfAjeBEsJsiHkQ%40mail.gmail.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments