KWAKO MWANAMKE....
Miaka kadhaa iliyopita dada mmoja ninayemfahamu kwa ukaribu tu aliivunja ndoa yake… nasema aliivunja kwa kuwa ni yeye ndiye aliyeondoka pale kwake na hakutaka kurejea kabisa. Yule dada alilaumiwa sana na jamii iliyomzunguka. ni watu wachache mnoooo walihoji uwezekano wa mumewe kuwa chanzo.
'Mwanamke mpumbavu huvunja ndoa yake kwa mikono yake mwenyewe…….' mwanamke uvumilivu bwana'…….. 'Ni mpaka kifo kiwatenganishe wewe ni mjinga sana uliyeshindikana ndio maana umeshindwa kudumisha ndoa'……… ' ulipaswa kusugua magoti umlilie Mungu wako mpaka ndoa isimame'….. 'hivi hakufikiria hata watoto wawili alio nao?... watu tunavumilia mengi sababu ya watoto.. yeye kashindwa nini?'
Maneno kama haya niliyasikia kila mara mwanamke yule alipojadiliwa. Kusema kweli kwa 85% nilikuwa upande wa jamii. Nilimlaumu kimoyomoyo kwasababu alipendezeana sana na mumewe. Yaani ukiwaona pamoja utatamani mahusiano yako yawe kama yao.
Siku moja nikakutana naye mahali. Katika maongezi ya hapa na pale nikamuuliza hivi kwani hamuwezi kusameheana mkarudiana?... Yule dada alicheka kwanza kisha akaniambia 'Laura wewe ni mwanamke siku moja utaelewa kwanini nilifanya nilivyofanya'… sikutaka kubishana naye lakini jibu lake halikuniridhisha. Nilichukulia kama mtu anayetafuta kujitetea!
Ni miaka imepita!.... yule dada hajaolewa tena sijui kwa kupenda au hajapata mwenza lakini ninachojua yuko katika mahusiano na analea watoto wake na ana mafanikio makubwa sana.
SASA Mume wa yule dada ana kesi kubwa polisi. Amempiga mkewe wa sasa mpaka amemvunja shingo na dada yu mahututi na si mara ya kwanza anamtandika vya kutosha! Safari hii ndugu wa mke wamechachamaa.
Leo hii ndio nagundua kuna nyakati UVUMILIVU NI UJINGA na ni excuse tu ya mtu kutaka kuendelea kukaa na mtu anayekuumiza kwa hofu kuwa huwezi kumuacha, huwezi maisha bila yeye, kwamba jamii itanionaje?
Sasa hivi jamii nzima inamtazama yule mke aliyepigwa kama mjinga tena…. Wanaulizana yaani anapigwa amekaa tu si angeondoka?....
Ni jamii hii hii ukimvumilia mwanaume Malaya utaambiwa atakuletea ukimwi shauri yako ukiondoka jamii inakwambia wanaume wote wako hivyo….. Ukivumilia manyanyaso ya kihisia unaambiwa atakuletea presha ufe uache watoto ukiondoka jamii inakwambia bibi zetu walivumilia zaidi ya hayo
Mwenzangu!....Jamii haijawahi kukosa cha kuongea wala haijawahi kuacha kulaumu…
maisha unayoishi ni yako!.... naamini mahusiano ni furaha, changamoto hazikosekani lakini zisizidi furaha!... mwaka mzima wewe ni mwezi mmoja tu una furaha!...unafanya nini hapo?!
Watoto unaong'ang'ania upo kwa ajili yao unawafundisha nini wanapoona unapigwa, unatukanwa, huna furaha, baba analala nje anarudi asubuhi, unalia kila mara…. Unakaa hapo ili wajifunze nini?...
sio kwamba ni kisingizio tu kwa kuogopa ukiondoka baba hatolipa karo? Sio kisingizio kwa kuwa unampenda huyu mnyanyasaji?.... wake up !....wake uuuup!... mfanye mwanaume ajue wewe ni mtu mzima mwenzake penye tatizo zipo njia bora zaidi za kutatua matatizo na sio NGUMI!!!
Unapoficha vipigo na unyanyasaji mwingine ili kuifurahisha jamii uonekane una ndoa imara au una furaha wakati unateketea vibaya mno…. Unajiumiza mwenyewe!
HATA ufunge na kuomba milele Mungu akishakuonyesha hapo sipo ni jukumu lako kutoka ukiendelea kung'ang'ania Muujiza wa Mungu ashushe winch akutoe… ndio tunasikia umeuawa kwa kipigo!
Hakuna tuzo inayotolea kwa kuvumilia vipigo na unyanyasi wa aina yoyote….HAKUNA TUZO MAMA!!
Maisha mafupi kutumia robo tatu ya siku yako kuombea mwanaume tuuu ukaacha kujiombea mengine kwa Mungu!...mwanaume naye ni binadamu kama wewe akikuchoka kakuchoka…kubali yaishe!
Anayekupenda hawezi kukutendea makorokocho hayo otherwise umeolewa na mgonjwa wa akili.
wewe mwenye mchumba/ boyfriend na ameshaanza kukutwanga makofi...unasubiri nini hapo?... atabadilika?.... umeambiwa tabia ni nepi inabadilishwa kirahisi? au ndoto za gauni jeupe linafunika yote?
Saying NO TO DOMESTIC VIOLENCE!!...INAANZA NA WEWE!!
Nitavumilia vyote sio kupigwa bora nionekane ni mke ovyo na nimeachika! maana vinginevyo Tutagawana nyumba za serikali wallah!!
IJUMAA NJEMA!!
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments