KWANINI VIONGOZI HAWA HAWAWI WAGENI RASMI KWENYE MAHAFALI?
Na Happiness Katabazi
NIMEKAA chini nimejiuliza sana bila majibu niomeona ni vyema niwaulize waungwana swali hili;
Hivi ni kwanini sioni wala kusikia mara kwa mara kuwa Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar, Seif Sharif Hamad, Mwenyekiti wa Chama Cha (Demokrasia), Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF), Professa Ibrahim Lipumba,Katibu wa Chadema, Dk.Wilbroad Slaa , Mwenyekiti wa Chama Cha NCCR- Mageuzi, James Mbatia, Mwanasheria wa Chadema, Tundu Lissu wanaalikwa Kuwa wageni rasmi Katika Mahafali ya vyuo vikuu , shule za Sekondari?
Nimezoea kuona kusikia na kuona kwenye mahafali ya Vyuo Vikuu Mgeni rasmi ni Rais Jakaya Kikwete, Makamu wa Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk.Mohammed Gharib Bilal, Rais wa Zanzibar, Dk.Ally Mohammed Shein, Marais wastaafu Ally Hassan Mwinyi na Benjamin Mkapa.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernad Membe, Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi Professa Anna Tibaijuka, Waziri wa Elimu na Ufundi Dk.Shukuru Kawambwa, Waziri wa Maji na Umwagiliaji Profesa Jumanne Maghembe, Waziri asiye na Wizara Maalum Profesa Mark Mwandosya na wengine.
Swali langu je hawa viongozi wa kisiasa wa vyama vya upinzani Mbona hatuoni wakialikwa Kuwa wageni rasmi Katika Mahafali ya Vyuo Vikuu, Sekondari ,Shule za Misingi ?
Je hawana hadhi na mvuto wa kualikwa kwenye mahafali ya Vyuo Vikuu, Sekondari na Shule za Msingi Kuwa wageni rasmi?
Au viwango vyao vya elimu vinatiliwa Shaka ndiyo maana hawaalikwi Kuwa wageni rasmi kwenye mahafali ya aina hiyo?
Au hadhi Yao ni kule kwenye mikutano ya hadhara ya kisiasa na katika mikutano yao na waandishi wa Habari tu kwenda kutoa hotuba za kuwasema wenzao ni mafisadi kila kukicha wakati nao ni wachafu pia?
Chanzo: Facebook: Happy Katabazi
0716 774494
Novemba 24 Mwaka 2014
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments