Mtoa maoni mmoja ametoa taarifa katika ujumbe ufuatao:
-- Vodacom inatatizwa na ukosefu wa usalama wa fedha zinazopitia mikononi mwao. Nina mifano mingi ila nitatoa mitatu tu.Taarifa hii imetolewa kwa njia ya maoni kupitia: plus.google.com/u/0/+SubiNukta/posts/JPDKXetkidN
i. Mmekuwa na tabia ya kuiba fedha wateja wanazo acha kama salio. Mara nyingi huwezi kulala na salio ukaamka ulikute!
ii. Mwanzoni mwa mwezi August mwaka huu nikitumia nba 0767773555 nilinunua kifurushi cha kupiga mitandao yote cha 15,000/=. Nilipongezwa kwa ununuzi ule wa Dakika 240 ila siku mbili baadae nilitumiwa meseji ati kifurushi changu "kimekwisha"! Nina uhakika sikupiga simu zaidi ya tano ambazo kati ya hizo hakuna iliyozidi dakika tano! Juhudi za kuwasiliana nao zili gonga ukuta hadi nikawa mpole; maana niko mbali na Dar.
iii. Tarehe mbili mwezi September nilifanya malipo ya 210,000/= kwenda namba 0766694413 toka namba yangu ya 0767773555 malipo yakiwa yamekusudiwa kwa Kampuni ya Ensol. La kushangaza fedha hiyo ilipotea na kwenda kwenye Akaunti ya mtu mmoja anayeitwa Francis Lengai ambaye hakuwa mlengwa. Niliwasiliana na Huduma kwa wateja dakika 2 baadae na kumwomba mhudumu azuie mwamala ule. Alikiri kuziona, kuzizuia na kuniahidi kuzirejesha kwenye Akaunti yangu ila alidai mpokeaji Francis hakuwa mwaminifu kwani alishahamisha 30,000/= kwenda kwa mtu fulani ambaye hata hivyo mmezikamata. Nilirejeshewa 180,000/= na kuahidiwa 30,000/= ndani ya masaa 24. Hadi leo wapi! 30,000/= mmeiiba!
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments