HIVI MNAPATA WAPI UJASIRI WA KUMTETEA MBOWE?
Hivi karibuni kumekuwa na picha ya mgando na video zikimuonesha mbunge wa Hai na mwenyekit wa CHADEMA akinyonyana mate na mke wake mbele ya kamera na kwa ridhaa yake mwenyewe. Muonekano wa picha zote unaonesha Mbowe alikuwa anajua kinachoendelea na alikiridhia. Watu wengi kwenye mitandao wameitazama ile picha katika hisia mbili tafauti.
Wapo waliosema Mbowe kama mwenyekiti wa chama na mbunge wa wananchi hakutakiwa kupigwa ile picha na ya kwamba ulikuwa ni upungufu wa maadili. Wapo waliosema Mbowe hakukosea, yale ni maisha yake binafsi na ya kwamba hata viongozi wengine duniani hufanya hivyo; hapa watetezi wa Mbowe walionesha picha za Obama akimbusu mkewe hadharani. Hivi watetezi wa Mbowe wanapata wapi ujasiri wa kumtetea?
Nakubali kuwa Mbowe ni binadamu na haki ya kufurahi na mkewe, lakini si katika namna ya kudhalilisha kiti cha CHADEMA na cha Hai. Si UTANZANIA kunyonyana ndimi hadharani, mimi hadi mama na baba yangu wanaingia kaburini sijawahi kuwaona wakipigana mabusu mbele yetu hata siku moja ndio seuze kunyonyana ndimi alikokufanya Mbowe? Kwa mujibu wa mila zetu, kunyonyana ndimi ni mambo ya faragha ya watu wawili tu.
Wazanzibar mara kadhaa wamewapiga bakora wazungu katika fukwe kutokana na kitendo chao cha kunyonyana ndimi hadharani. Wanafanya hivyo sababu kunyonyana ndimi hadharani si uzanzibar. Tuige mambo mazuri toka nje, lakini si kila cha kuiga kisa kafanya mzungu. Kitendo cha Obama kubusiana na mkewe hadharani hakutoe uhalali wa mtanzania yeyote kunyonyana ndimi hadharani, ndio sembuse kwa mbunge na mwenyekiti wa chama?
HIVI MAADILI YA TAIFA TUNAYAPELEKA WAPI?
Kwa mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani ambacho kinatarajiwa kuingia ikulu anakuwa na upungufu wa maadili wa kiwango kikubwa, je chama hicho kikikabidhiwa nchi kitaweza kukemea na kuzuia kufanyika vitendo hivyo hadharani? Je, watoto wetu watakuwa katika hali gani huko mashuleni na mabarabarani endapo chama kilichounda serikali kwao wao ni sawa kufanya vitendo vya faragha hadharani?
Hivi hiki chama hakiendi kutuletea uhuru usio na mipaka hasa hasa ukizingatia sasa hivi wanakula sahani moja na chama cha kilebarali?(chama walichokituhumu kutetea haki za wapenzi wa jinsia moja) Ndio maana tunasema, tusipigane kuitoa CCM tu madarakani lakini pia tuhakikishe manyang'au wa UTANZANIA wetu pia hawaingii ikulu. Kitendo alichokifanya Mbowe hakitarajiwi kufanya na mtu wa umri wake na wa wadhifa wake, Mbowe amefanya UNYANG'AU na kwakuwa yeye ndio taswira ya chama basi CHADEMA haiwezi kujitenga na unyang'au huu.
MWISHO.
Asante Mungu kwa kuwafichua wanafiki kabla ya jua la utosi, kinyume chake nchi hii ingeendeshwa kama nyumba ya kichaa endapo tungeipa CHADEMA ridhaa. Machale kundesa, Ngastuka!!!!!!
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments