[Mabadiliko] Neno La Leo: Katiba Na Ukungu Kwenye Kioo...

Wednesday, October 08, 2014


Ndugu zangu,

Leo Watanzania tutashuhudia Rais wa Jamhuri akikikabidhiwa Katiba Pendekezwa kwenye Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.

Kitakachofuatia ni Katiba Pendekezwa kupigiwa kura na Wananchi. Na Katiba ya Nchi ni sawa na Kioo cha Nchi. Tunajitazama kupitia katiba. Na tunafanyaje kama kioo kimeingia ukungu?

Mwingine atasema tukivunje, tutafute kipya. Lakini, kwa vile ukungu kwenye jamii utaendelea kuwepo daima na hatuwezi kuuzuia , je,tutavunja vioo vingapi?
Naam, mchakato wa katiba umefikia ulipofikia, na bado haujakamilika. Ukungu ungalipo, na mwingine unakuja. Na lipi lililo jema, kuvunja kioo au kufuta ukungu?

Tukitanguliza hekima na busara, tukitanguliza mapenzi kwa nchi tuliyozaliwa. Hivyo, uzalendo kwa nchi yetu. Basi, tutauona mchakato wa Katiba kama 'Mchakato Wa Kujifunza'. Tumejifunza mengi na tunaendelea kujifunza kama taifa. Tumeuona udhaifu wetu ambao huko nyuma hatukuuona. Tumeziona nguvu zetu pia. Tumeanza kujitambua zaidi.

Kuna wanaohangaika kumtafuta mshindi na mshindwa kwenye mchakato huu. Hao ni majuha, maana waliuangalia mchakato huu kwa rangi za vyama vyao na makundi yao.

Maana, hapa tulipofikia, pamoja na ukungu uliopo, bado Watanzania wote ni washindi. Wote walioshiriki kufanikisha kutufikisha hapa wamefanya kazi njema. Na tuamini, kuwa wengi wao walikuwa na nia njema, akiwamo Rais Jakaya Kikwete aliyeanzisha mchakato huu.

Na hapa naungana na alichosema Waziri Mkuu Mizengo Pinda pale Bungeni, kuwa ingekuwa vema pia, kama Katiba hii pendekezwa ingepigiwa kura na wananchi kwenye uchaguzi mkuu ujao, maana, nami naamini, wananchi tusingependa kusubiri sana kutoa kauli yetu kuhusiana na katiba, kwa kupitia sanduku la kura.

Naam, tulipofikia kama Taifa, hatuna namna yeyote ya kufanya, bali Kusonga Mbele, kwa kuendelea kujadiliana, na si kuandamana.

Ni Neno La Leo.
Maggid Mjengwa,
Nairobi.

--
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
 
 
For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Mabadiliko Forum" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
To post to this group, send email to mabadilikotanzania@googlegroups.com.
Visit this group at http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania.
To view this discussion on the web visit https://groups.google.com/d/msgid/mabadilikotanzania/CAMD-ye46GGuSiTX3mXYwgDP%3DvC-G1Qn1fJfLgHrMKLMfdzKhOg%40mail.gmail.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments