MHESHIMIWA Freeman Mbowe ni Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), pia ni Kiongozi Mkuu wa Kambi ya Upinzani bungeni, na huko nyuma aliwahi kugombea nafasi ya uraisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwa nafasi zake hizo na "mvuto" wake katika jamii, anachokisema kinaweza kubebwa kwa uharaka usio na kipimo.
Kwa kutambua hali hiyo ndipo nikaonelea Kalamu yangu kwa leo iandike ushauri kwa Watanzania haswa vijana kwamba: Maneno ya Mheshimiwa Mbowe yatafakarini kwanza kabla ya kuyatekeleza.
Katika hotuba yake aliyoitoa katika Mkutano mkuu wa chama hicho uliomuweka tena madarakani kwa kipindi kingine cha tatu, Mheshimiwa Mbowe kama alivyonukuliwa na Gazeti la Tanzania Daima la siku ya Jumatano tarehe 15/09/2014 amesema:
"Hatuwezi kukaa kimya huku maoni ya Watanzania yakiwa yanachakachuliwa, hivyo basi tutashirikiana na Taasisi mbalimbali, Ukawa, kufanya migomo na maandamano nchi nzima bila kikomo…aidha kuwa na kibali cha Polisi au Laa, na kwamba kuna watu watakaokuwa mstari wa mbele watajeruhiwa, lakini lengo likiwa kufikisha ujumbe wenye sura ya wananchi".
Mheshimiwa Mbowe aliendelea kusema: "Samahani maneno yangu ni makali na wala sifanyi uchochezi, kinachoendelea Dodoma ni ufisadi na wizi" (mwisho wa kunukuu).
Maneno hayo ya Mheshimiwa Mbowe yanahitajia tafakuri ya kina kwa sababu:
(a) Mheshimiwa Mbowe anafahamu wazi umuhimu wa jamii kuishi kwa kuheshimu sheria. Aidha anafahamu wazi madhara ya jamii inayopingana na mamlaka za dola, na tukio la kukaidi maelekezo ya vyombo vya dola kama kadhia ya maandamano ya Arusha yaliyosababisha madhara makubwa sana. Najua anakumbuka vizuri sana tena sana tukio hilo.
(b) Mheshimiwa Mbowe anafahamu madhara ya maandamano yasiyo na kibali cha Polisi na ndio maana ametamka mwenyewe kwamba kuna watu watajeruhiwa.
Hapo sasa ndipo ninapotaka vijana "wazame" kwanza kwenye tafakuri kabla ya kutii maelekezo au amri zitakazotolewa hapo pindi wakati ukifika. Je, kama ni kweli watu watajeruhiwa, ni nani atagharamia matibabu yao? Au kama watapoteza uhai kama ilivyotokea kwa wale ndugu zetu wa Arusha (katika yale maandamano ya CHADEMA yaliyopita).
Je, ni nani atalea familia zao? Na hata kama hakuna mauaji yoyote wala majeruhi wowote ila waandamanaji wamekamatwa kwa kosa la kuandamana bila ya kibali, Je ni nani atawaendeshea kesi zao? Na endapo ikitokea kuthibitika kwa kosa walilofanya na wakahukumiwa kufungwa kifungo cha muda wowote gerezani. Je ni nani atalea familia zao pamoja na kuwahudumia wazazi wao?
Maswali haya au tafakuri hii ni muhimu sana kuifanya kabla ya kukubali na kutii amri hiyo ya Mheshimiwa Mbowe juu ya maandamano yasiyokoma.
Ni vizuri sana Watanzania haswa vijana wakajiridhisha kwanza kwa kutafakari katika kuyaendea matukio ya wanasiasa kabla ya kuongeza mapya. Hivi ni kweli kwamba maandamano hayo lengo lake ni "kuhurumia" pesa zinazotumika katika Bunge Maalum la Katiba?
Je, huruma hizo Mheshimiwa Mbowe zinamjia leo hii wakati yeye na kundi lake "wamesusia" vikao vya Bunge Maalum la Katiba? Je, Mheshimiwa Mbowe ana msimamo gani juu ya fedha zilizotumika kuiendesha Tume ya Jaji Warioba?
Je, zile fedha zilizotumika wakati wa mwanzoni mwa Bunge Maalum la Katiba ambalo yeye na wenzake walikuwemo bungeni hazikuwa na thamani yoyote kwa Watanzania? Hivi fedha zenye thamani ni hizi ambazo wao wamezisusa tena kwa hiyari yao wenyewe na hakuna aliyewafukuza katika vikao hivyo?
Watanzania haswa vijana kama hawatokuwa makini wanaweza kutumiwa kama "upawa". Upawa ni kile chombo cha kuchotea mchuzi katika sufuria haswa ukiwa bado wa moto na huwezi kutia mkono. Lakini kazi ya upawa ni kuopoa tu, ukifika wakati wa kula upawa huwa hauna nafasi wala thamani yoyote tena mpaka wakati mwengine wa kupika.
Hivi ni nani asiyejua kwamba Bunge Maalum la Katiba lipo kwa mujibu wa sheria? Hivi Bunge lililoundwa kwa mujibu wa sheria na kuendeshwa kwa mujibu wa sheria linawezaje kukoma au kusimama kwa maandamano?
Je, Mheshimiwa Mbowe ambaye anaongoza Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwa kipindi cha tatu siku wanachama wake wakiandamana kwamba hawamtaki, yuko tayari kuachia ngazi ili kuheshimu demokrasia ya mawazo?
Ni vizuri Watanzania tukafahamu kwamba Demokrasia kwa sasa inabebeshwa tafsiri nyingi sana, kama hatukuwa makini wanaweza kuwa "wavunja demokrasia" wakajipa kuheshimu "demokrasia".
"UKAWA" ambao kwa idadi ya wawakilishi wao katika Bunge Maalum la Katiba ni wastani wa asilimia ishirini na Waheshimiwa Wabunge waliobakia ndani ya bunge hilo ni asilimia themanini, lakini jambo la ajabu zikaanza kutolewa fikra na mawazo kwamba Katiba itakayotolewa haitokuwa bora kwa sababu itaelemea upande mmoja, madai ambayo yanashangaza sana halafu wanaotoa mawazo kama hayo wanasifiwa kuwa ni wana demokrasia.
Hivi asilimia ishirini inaathiri vipi asilimia themanini katika maamuzi? Je hizo ni hesabu na takwimu kutoka nchi gani?
Maajabu zaidi ni pale Mheshimiwa Mbowe anapotamka kwamba maoni ya wananchi yanachakachuliwa kwa hiyo wao hawawezi kuwa kimya. Hivi kuchakachua kwa kiswahili cha Mheshimiwa Mbowe anajua maana yake?
Hivi neno "kuchakachua" kulihusisha na Waheshimiwa Wabunge sio kuwakosea nidhamu wao na bunge lote kwa ujumla? Hivi kwa mtazamo wa Mheshimiwa Mbowe kazi za Bunge Maalum la Katiba ni zipi ili kama wamefanya tofauti ndio waambiwe kuwa wanachakachua?
Kama huyo ndiye Mwenyekiti wa chama cha siasa ambaye anategemewa awe ndiye "kisima" cha busara ili kuongoza chama. Ikiwa huyo ndiye ambaye aligombea uraisi wa nchi hii na kama kura zingetosha leo hii angekuwa ndiye Raisi wetu na huo ndio uwezo wake katika kufikiri na kuyaendesha mambo.
Hapo ndipo ninapoendelea kuwakumbusha Watanzania haswa vijana kwamba maneno ya Mheshimiwa Mbowe muyapokee lakini muyatafakari kwanza kabla ya kuyatekeleza.
Niihitimishe Kalamu yangu kwa leo kwa kuonyesha "mishangao":
(1) Mshangao wangu wa kwanza ni pale Mheshimiwa Mbowe anapotamka maneno ya "uchochezi" mbele ya Msajili wa Vyama vya Siasa kisha Msajili huyo akakosa vifungu vya kisheria au hata busara na hekma za kiuongozi kumtaka Mheshimiwa Mbowe afute au airekebishe kauli yake hiyo.
Kimya hicho cha Mheshimiwa Msajili kinatia mashaka makubwa juu ya kiongozi mkuu mwenye dhamana ya kusajili na kusimamia sheria ya vyama vya siasa kama baba wa vyama hivyo.
Hivi kama maneno yale yangetamkwa na kiongozi wa chama fulani, Je Msajili angeendelea kukaa kimya kwa saa zaidi ya ishirini na nne huku jamii ya Kitanzania ikimshuhudia Mheshimiwa akivunja sheria tena hadharani?!!
(2) Mshangao wangu wa pili ni juu ya mualikwa mmoja miongoni mwa waalikwa wa Mkutano Mkuu ule kutoka nje ya nchi ambaye ni mwakilishi wa chama cha "kidini" katika nchi yake. Inavyoonekana upo uhusiano kati ya chama cha kidemokrasia cha hapa nchini na kile cha kidini cha huko nje, huu ni mshangao kwangu lakini ni ufunguo pia wa kuomba kuelimishwa juu ya uhusiano wa aina hiyo.
(3) Mshangao wangu wa tatu ni juu ya "azma" ya UKAWA kutaka waungane ili kuing'oa CCM katika Uchaguzi Mkuu ujao mwakani 2015. Maneno hayo yenye nia njema ya kuungana ni maneno yenye faraja kubwa sana kwa sababu ni umoja tu ndio ambao huifikisha jamii kwenye ushindi. Lakini:-
• Kitendo cha Mheshimiwa Mbowe kuutangaza "muungano" wa vyama vya upinzani katika Uchaguzi Mkuu ujao mwakani 2015 kitazaa tafsiri kwamba chaguzi zote za nyuma CCM ilishinda kihalali kwa sababu vyama hivyo havikuwa vimeungana, na safari hii vyama vinakusudia kuungana ili kupata ushindi.
Je, Mheshimiwa Mbowe anafahamu kuwa maneno yake yanazaa tafsiri hiyo? Na kama anakiri kwamba yanazaa tafsiri hiyo, Je yuko tayari kuwaomba radhi Watanzania kwa niaba ya chama chake ambacho kilidai kuibiwa kura na CCM kumbe hawakuibiwa? Bali walishindwa kwa sababu ni wachache, na kwa kuutaka ushindi wa kweli wameamua kuungana kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa mwakani 2015.
• Mheshimiwa Mbowe anautangaza muungano wa vyama vya upinzani huku"akisahau" uwezekano wa vyama hivyo kuungana kutokana na mitazamo na sera.
Hebu tuiangalie mikutano ya chama cha CUF kule Tanga hapa Dar es Salaam, Zanzibar, Pemba, Mtwara, Mwanza, Morogoro na Lindi; halafu tuiangalie mikutano ya CHADEMA kule Arusha, Kilimanjaro, Mbeya, Iringa na Musoma; kisha eti upande mmoja kati ya pande hizo mbili ambazo kila moja iko tofauti sana na mwenzake, ni vipi wanaweza kuungana kifikra na kimaamuzi na hatimaye kumpa kura mgombea uraisi atakayetoka katika chama kimojawapo?
Ni maneno gani utawaambia wafuasi hawa kwamba wajenge imani ya dhati kwa hawa wenzao ambao tayari kwa kupitia serikali ya Umoja wa Kitaifa, wao tayari ni sehemu ya serikali hiyo ambayo eti wana dhamira ya dhati ya kuiondoa madarakani?
Ukizingatia kwamba Makamu wa kwanza wa Raisi wa Zanzibar (ambayo ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania) pamoja na mawaziri kadhaa wanatoka katika chama cha CUF, ni lugha gani wataitumia kuonyesha "ubovu" wa serikali (ambayo wao wamo ndani yake) ili jamii iwaamini kwamba wao ni wahusika katika mafanikio tu ama mapungufu wao hawamo?!!! Je, haya yanaingia akilini?!!
Lakini ni lugha gani wataitumia hawa wenye mpango wa kuigawa Tanzania kwenye majimbo, na huku wakiamini kwamba katika kila sekta na idara za serikali ni lazima awepo "mtu wa kwetu", Je kura hapo zitatoka kweli?!!
Kuhusu ruzuku ya kutoka ndani na nje ya nchi, hivi tunaamini kwamba kipo chama hapa Tanzania kinaweza kujiunga chama kingine, ili chama hicho kipate ruzuku pamoja na mafanikio ya ushindi kupitia mgongo wa chama kingine? Je, haya tunayaamini kweli?
Lakini mwisho niwaombe viongozi wote wa vyama vya siasa watambue kwamba Watanzania siku zote shida zao sio aina ya jina la chama tawala, Laa hasha! Bali shida yao kuu ni kupata kiongozi atakayewaongoza katika misingi ya Amani na Utulivu, awe mvumilivu na mwingi wa kusamehe.
Asiwe king'ang'anizi wa madaraka (vipindi viwili vya utawala wake vikiisha yeye bado analazimisha utadhania chama chake hakina m-bora kuliko yeye, Je akifa yeye chama nacho kitakufa?).
Watanzania haja yao ni uongozi bora wenye kupendeza ndani na nje ya mipaka ya nchi yetu. Siku zote Watanzania hawapendi uongozi wa vurugu kwani wamejifunza kutokana na kuona yale yanayowakuta wenzao katika mataifa mengine.
Niwanasihi wapiga kura kamwe tusithubutu "kupiga kura ya hasira" kwani kura hiyo ina furaha kidogo kwa kuondoka usiyempenda lakini ina madhara makubwa kwa kumuondoa mwenye uuwezo wa kukuongoza. Kamwe tusithubutu kujiandaa kutaabika kwa miaka mitano kwa hoja eti herufi za chama zimebadilika.
Maneno ya Mheshimiwa Mbowe tuyapokee, tuyatafakari na tuyapime kisha kwenye utekelezaji tuwe makini.
Naomba kuwasilisha.
*Mwandishi wa makala hii Sheikh Mohamed Iddi Mohamed ni Mwenyekiti wa ARRISAALAH ISLAMIC FOUNDATION. Unaweza kuwasiliana nae kwa namba: +255 754 299 749, +255 784 299 749.
-- Kwa kutambua hali hiyo ndipo nikaonelea Kalamu yangu kwa leo iandike ushauri kwa Watanzania haswa vijana kwamba: Maneno ya Mheshimiwa Mbowe yatafakarini kwanza kabla ya kuyatekeleza.

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments