[wanabidii] WAISLAMU NA WAKRISTO WAIKATAA KATIBA YA CCM

Thursday, September 25, 2014

 Ni jambo lisilopingika kwamba CCM wamejipanga kisawasawa kuhakikisha akidi ya wajumbe inatimia bungeni ili katiba yao ipite bila kikwazo chochote. Hili suala liko wazi hasa ukizingatia kwamba CCM wamependekeza kwamba wajumbe watakaokuwa nje ya nchi wapige kura wakiwa hukohuko waliko. Sababu ya kutumia mbinu hii ni kutaka kuchakachua kura….hii mbinu ni nzuri sana kwa kuwa itawawezesha kuchokmekea kura za maruhani ili hatimaye akidi itimie na katiba ipigiwe kura za NDIYO bungeni kabla ya kuileta kwa wananchi.
 
Sababu ya pili itakayoifanya katiba hii ipite ni ukweli kwamba CCM wamekuwa wakitumia fedha nyingi sana kuwarubuni wajumbe wa kundi la 201 ili wawasaidie kupitisha katiba mpya, ijapokuwa kuna baadhi ya 201 ambao hawatetereshwi na hila za CCM.
 
Hili sio jambo la kushangaza kwani CCM wamejizatiti vizuri kuhakikisha kwamba hiyo mbinu yao ya kilaghai inafanikiwa. Ila kitakachonisikitisha sana ni ikiwa wakristo na waislamu waliopo uraiani wataipigia kura ya NDIYO katiba iliyopendekezwa. Hii hasa inatokana na sababu zifuatazo:
 
1.      Mahakama ya Kadhi yamezikwa na CCM waziwazi na hawataki hata kuyazungumzia. CCM wamefanya hivi kwa kuwa wanajiamini kwamba waislamu na mashehe waliomo Bunge la Katiba ni wachumia tumbo na kwamba wameishaukubali unafiki huu wa CCM kwa staili ya "Funika Kombe Mwanaharamu Apite". Sasa nitawashangaa sana wale waislamu safi (ukiondoa waislamu wa BAKWATA ya CCM na wachumia tumbo wachache) kama wataipigia kura ya NDIYO Katiba ya CCM iliyopendekezwa.
 
2.      Jumuiya ya kikristo (CCT) inayojumuisha makanisa yote ya kikristo, imeishaonesha msimamo wa kuikataa katiba hii ya CCM na wamejipanda vizuri kutoa elimu ya uraia kwa wafuasi wao ili waikatae wakati wa kupiga kura ya maoni. Wakristo daima wana msimamo wa pamoja na hawawezi kuwaangusha viongozi wao. Ninayo imani kwamba wakristo wote watakuwa kitu kimoja kuhakikisha kwamba katiba hii ya kiFISADI haipiti hata kwa dawa. Nitawashangaa sana wale wakristo watakaojitoa akili za kiroho na kumfuata shetani (CCM) pindi upigaji kura za maoni utakapowadia. Sio jambo la busara kwa wakristo kuvaa upagani (u-CCM) na kumtumikia shetani. Pepo la upagani lishindwe kwa jina la Yesu ili katiba hii ya kishetani ikose mamlaka duniani na hata mbinguni. Wote tuseme "Ameeeeeeeeeeen".
 
3.      Wananchi wote wapenda haki na maendeleo (wapagani na wakristo pamwe) wamechukizwa sana na kitendo cha CCM kukataa maoni yao waliyotoa kwa Tume ya Mh, Judge, Dr Joseph Sinde Warioba. Na hasira hizi za wananchi zitadumu hadi muda wowote katiba hiyo itakapoletwa mbele zao ili waipigie kura za HAPANA. Hasira za wananchi dhidi ya CCM hazitapungua milele hata kama wakiahirisha zoezi la upigaji kura hadi karne ijayo. Hili tu linanipa imani kwamba CCM wanatwanga maji kwenye kinu na hawajui walifanyalo….katiba hii ya CCM haitapita kamwe!

Share this :

Related Posts

0 Comments