UTUMISHI WA UMMA
Serikali ya Jamhuri ya Muungano
278. Mtu aliyekuwa anashika nafasi ya madaraka ya Rais wa Jamhuri ya Muungano kabla ya kuanza kutumika kwa Katiba hii, ataendelea kushika nafasi ya madaraka ya Rais kwa masharti ya Katiba hii hadi mtu mwingine atakapochaguliwa badala yake katika Uchaguzi Mkuu wa kushika nafasi ya madaraka ya Rais kwa mujibu wa Katiba hii.
Kuendelea kuwepo kwa Makamu wa Rais madarakani
279. Mtu aliyekuwa anashika nafasi ya madaraka ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano kabla ya kuanza kutumika kwa Katiba hii, ataendelea kushika nafasi ya madaraka ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano kwa masharti ya Katiba hii hadi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano atakapochaguliwa badala yake katika Uchaguzi Mkuu.
Kuendelea kwa Waziri Mkuu, Mawaziri na Naibu Mawaziri
280.-(1) Mtu anayeshika nafasi ya Waziri Mkuu ataendelea kuwa katika nafasi ya madaraka ya Waziri Mkuu hadi Uchaguzi Mkuu utakapofanyika, na Rais wa Jamhuri ya Muungano ameshika madaraka.
(2) Mtu anayeshika nafasi ya madaraka ya Waziri au Naibu Waziri ataendelea kushika nafasi hiyo ya madaraka hadi Uchaguzi Mkuu utakapofanyika na nafasi hiyo ya madaraka itakoma saa ishirini na nne kabla ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuapishwa kushika nafasi ya madaraka ya Rais.
(3) Masharti ya ibara ndogo ya (1) na (2), hayatatafsiriwa kwamba yanaondoa au kufifisha madaraka aliyonayo Rais kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 au sheria za nchi kufuta nafasi ya madaraka ya kumvua madaraka au kumwachisha kazi mtu anayeshika au kukaimu nafasi ya madaraka au kumwachisha kazi mtu anayeshika au kukaimu nafasi ya madaraka ya Waziri Mkuu, Waziri au Naibu Waziri kujiuzulu.
Kuendelea kwa utumishi wa umma
Sura ya 2
281.-(1)Kila mtu aliyeshika au kukaimu nafasi ya madaraka ya utumishi wa umma katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano, Bunge la Jamhuri ya Muungano au Mahakama ya Jamhuri ya Muungano kabla ya tarehe ya kuanza kutumika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 2014, ataendelea na atatambuliwa kuwa amechaguliwa, kuteuliwa au kuajiriwa kushika au kukaimu nafasi ya madaraka ya utumishi wa umma katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano, Bunge la Jamhuri ya Muungano au Mahakama ya Jamhuri ya Muungano na kwamba masharti ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Mwaka 2014 au sheria za nchi kuhusiana na kuchaguliwa, uteuzi, ajira na kula kiapo au yamini yamezingatiwa na kutekelezwa.
(2) Kila mtu ambaye kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa
103
Kuendelea kwa Ubunge na Uongozi wa Bunge
Sura ya 2 na 343
Tanzania ya Mwaka 1977 au sheria za nchi, atahitajika kuondoka katika nafasi ya madaraka baada ya muda maalum kupita au atakapotimiza umri wa kustaafu, ataacha kushika nafasi ya madaraka katika utumishi wa umma baada ya kufika mwisho wa muda huo maalum au atakapofika umri wa kustaafu.
(3) Masharti ya ibara ndogo ya (1) na (2), hayatatafsiriwa kwamba yanaondoa au kufifisha madaraka aliyonayo mtu au yaliyowekwa kwa mamlaka kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 au sheria za nchi kufuta nafasi ya madaraka na kumvua madaraka au kumwachisha kazi mtu anayeshika au kukaimu nafasi ya madaraka au kumtaka mtumishi wa umma kujiuzulu.
(4) Kwa madhumuni ya malipo ya kiinua mgongo au malipo mengine ya uzeeni, muda wa utumishi wa mtumishi wa umma anayehusika na masharti ya Ibara hii, utahesabika kuwa ni pamoja na muda wa utumishi aliokuwa nao kabla ya kuanza kutumika kwa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 2014.
(5) Isipokuwa kama itaelekezwa vinginevyo, masharti ya kazi ya mtumishi wa umma ambaye masharti ya Ibara hii yanamhusu hayatakuwa duni au hafifu ukiliganisha na masharti ya kazi aliyokuwa nayo kabla ya kuanza kutumika kwa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 2014 au sheria za nchi zitakazotungwa kwa ajili hiyo.
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments