[wanabidii] Ardhi katika Jamhuri ya Muungano

Wednesday, September 24, 2014

SURA YA TATU

 

ARDHI, MALIASILI NA MAZINGIRA

 

22.-(1) Ardhi ndiyo rasilimali kuu kwa ajili ya maendeleo ya kiuchumi, kijamii na ustawi wa nchi na watu wake wote. Serikali ya Jamhuri ya Muungano itaweka mipango bora ya matumizi endelevu ya ardhi kwa faida ya kizazi kilichopo na vizazi vijavyo.

 

(2) Ardhi yote itamilikiwa, itatumiwa na kusimamiwa kama itakavyoainishwa na sheria itakayotungwa na Bunge kwa kuzingatia misingi ifuatayo:

(a)    raia wa Tanzania pekee ndiye atakayekuwa na haki ya kumiliki ardhi ya Tanzania, na haki hiyo italindwa kwa mujibu wa Katiba hii;

 

(b)    mtu ambaye siyo raia wa Tanzania atakuwa na fursa ya kutumia ardhi kwa ajili ya uwekezaji na maendeleo mengine ya kiuchumi na makaazi;

 

(c)    haki ya kumiliki, kuendeleza na kuhifadhi ardhi kwa ajili ya makundi mbalimbali ya jamii wakiwemo wakulima, wavuvi, wafugaji na makundi madogo itatambuliwa na kulindwa kwa mujibu wa Ibara hii; na

(d)    kila mwanamke atakuwa na haki ya kupata, kumiliki, kutumia, kuendeleza na kusimamia ardhi kwa masharti yaleyale kama ilivyo kwa mwanaume.

 

23. Bunge litatunga sheria itakayoweka masharti kuhusu mgawanyo wa matumizi bora ya ardhi kwa makundi mbalimbali ya jamii.

 

24. Bila kuathiri masharti ya Ibara ya 45(2) ya Katiba hii, Serikali itaweka utaratibu wa kisheria kwa ajili ya malipo ya fidia stahiki endapo eneo au sehemu ya ardhi itachukuliwa kwa matumizi ya maendeleo ya kiuchumi na ya kijamii.


 

Maliasili


 

25. Maliasili zote za Taifa ikiwa ni pamoja na madini, gesi na mafuta ni mali ya umma, na Serikali ya Jamhuri ya Muungano au Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaweka utaratibu wa kuhakikisha zinatumika kwa manufaa ya kizazi cha sasa na vizazi vijavyo.


 

Mazingira                        26. Serikali itaweka mazingira wezeshi na mikakati mahsusi kwa ajili ya:

 

8


(a)   kuhakikisha matumizi endelevu, usimamizi na uhifadhi wa mazingira na maliasili, kwa manufaa ya kizazi cha sasa na vizazi vijavyo;

 

(b)   kusimamia na kutunza maeneo ya kihistoria na ya kale kwa manufaa ya wananchi wote;

(c)    kuhakikisha kuwa taasisi za umma na asasi za kiraia zinawajibika kusimamia utekelezaji wa matakwa ya kisheria katika kulinda na kuhifadhi mazingira; na

 

(d)  kuhakikisha kwamba wananchi wa Tanzania ndio wenye haki ya kumiliki rasilimali za kijenetiki za Tanzania kwa manufaa ya Taifa. 

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments