MABADILIKO CHADEMA kachakachua habari na katupostia uwongo juu ya Prof. Safari. Wanajukwaa ebu someni wenyewe hapo chini alichokisema prof. safari mlinganishe na alicho tuandikia huyo mpuuzi Mabadiliko Chadema
Prof. SAFARI: Nitamaliza dhana ya UDINI CHADEMA
Profesa Abadllah Safari ambaye anawania nafasi ya makamu mwenyekiti CHADEMA Taifa ameahidi kuleta mapinduzi ya kimtazamo kuhusu dhana ya udini iliyojengwa kipropaganda na watawala na kuathiri ukuaji wa vyama vya siasa vilivyoundwa nchini baada ya kuundwa kwa mfumo wa vyama vingi mwaka 1992.
Profesa huyo wa sheria, anasema kwa nia ya kuvuruga akili za watanzania ili waogope, wasivutiwe na wasishawishike kuviunga mkono vyama hivyo, watawala chini ya CCM wameaminisha wananchi kuwa CHADEMA ni chama kinachoungwa mkono na wakristo tu na kuwa eti CUF inaungwa mkono na waislamu tu.
Hiyo dhana potofu ndiyo anayokusudia kuifuta kwa kueleza na kuonesha kuwa vyama ni mali ya wananchi pasipo kujali itikadi za dini.
Habari hii kwa ufupi ni kwa hisani ya gazeti MA.W.I.O la wiki hii.
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments