[wanabidii] TAARIFA KWA UMMA KUHUSU TOLEO LA SARAFU YA SHILINGI MIA TANO

Saturday, September 13, 2014

TAARIFA KWA UMMA

TOLEO LA SARAFU YA SHILINGI MIA TANO.

Benki Kuu ya Tanzania ndiyo chombo chenye jukumu la kutoa sarafu 
na noti halali (legal tender) zinazotumika nchini. Katika kutekeleza 
jukumu hili Benki Kuu hutengeneza noti na sarafu zenye uwiano mzuri 
wa thamani (denominations) unaozingatia uwezekano wa zile zenye 
thamani kubwa kuweza kugawika katika zile zenye thamani ndogo 
ndogo.

Hii hulenga kurahisisha upatikanaji wa chenji na uwezekano wa 
wahitaji wa viwango mbalimbali vya bidhaa na huduma kupata
katika mafungu yatakayokidhi mahitaji yao.

Katika kutekeleza jukumu hili, Benki Kuu imetoa toleo jipya la Sarafu 
ya Shilingi 500. Hatua hii imezingatia yafuatayo:

* kwamba noti ya shilingi mia tano (500), ndiyo inayotumika 
zaidi kwenye manunuzi ya kawaida ya kila siku ya wananchi 
wengi kuliko noti nyingine yoyote. Hivyo noti hiyo hupita 
kwenye mikono ya watu wengi katika kipindi cha muda mfupi
sana na kuchakaa haraka. 
* Noti hizi hukaa katika mzunguko kwa muda mrefu bila 
kurejeshwa kwenye mabenki kwa wakati muafaka ili 
zibadilishwe zinapokuwa zimefikia ukomo wake.
* Sarafu hukaa kwenye mzunguko kwa miaka mingi zaidi kuliko 
noti. Sarafu hii inatambuliwa kwa kuangalia yafuatayo:
* Umbo lake ni la duara lenye michirizi pembezoni, kipenyo 
cha milimita 27.5 na uzito wa gramu 9.5 
* Ina rangi ya fedha na imetengenezwa kwa madini aina ya 
chuma (Steel) na "Nickel" 
* Kwa mbele ina sura ya Rais wa Kwanza wa Serikali ya 
Mapinduzi ya Zanzibar, Sheikh Abeid Aman Karume na kwa 
nyuma ina taswira ya mnyama nyati akiwa mbugani.
* Ina alama maalum ya usalama iitwayo "latent image" iliyopo 
upande wa nyuma ambayo ni kivuli kilichojificha. Kivuli hiki 
huonesha thamani ya sarafu '500' au neno 'BOT'
inapogeuzwa-geuzwa.

Sarafu hii mpya ya shilingi mia tano (500) inatarajiwa kuingizwa kwenye 
mzunguko kuanzia mwezi Oktoba 2014.

Sarafu hii, itakuwa ikitumika sambamba na noti zilizopo sasa za shilingi 
mia tano mpaka hapo noti hizo zitakapokwisha katika mzunguko.

Pamoja na taarifa hii; tunawaomba wananchi kuendelea kufuatilia vipindi 
mbalimbali vitakavyokuwa vinaeleza jinsi sarafu hii ilivyo na namna ya 
kutunza noti na sarafu zetu kwa njia salama.

Ahsanteni Sana.
(source: BOT) 8th september, 2014.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments