[wanabidii] Rais Kikwete ziarani nchini Marekani

Wednesday, September 17, 2014
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameondoka nchini usiku wa jana, Jumatatu, Septemba 15, 2014, kuanza ziara ya wiki mbili katika Marekani ambapo atahutubia Mkutano wa 69 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UN General Assembly) New York.

Mbali na kuhutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York, Rais Kikwete pia atahudhuria mikutano muhimu katika mji mkuu wa Marekani, Washington, D.C.

Mjini New York, Rais Kikwete atashiriki katika mikutano mikubwa zaidi ya 10 ikiwa ni pamoja na kuhutubia Baraza Kuu wakati wa Majadiliano ya Jumla ( General Debate) yaliyopangwa kufanyika Septemba 24 hadi 27 na Septemba 29 hadi Oktoba Mosi, mwaka huu, 2014.

Rais Kikwete amepangwa kuwa kiongozi wa 12 duniani kuhutubia Baraza hilo mchana wa Alhamisi ijayo, Septemba 25, 2014. Mkutano wa 69 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa utaanza Septemba 16 hadi Desemba 24, mwaka huu, Miongoni mwa mikutano mingine muhimu ambayo Rais Kikwete atashiriki ni pamoja na kuwa mwenyekiti wa Kamati ya Wakuu wa Nchi Wanachama wa Umoja wa Afrika (AU) Kuhusu Mazingira (CAHOSC) na Mkutano wa Wakuu wa Nchi Kuhusu Mazingira ulioitishwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Mheshimiwa Ban Ki Moon.

Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
16 Septemba , 2014.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments