[wanabidii] PATROBAS, PASCHAL KATAMBI- AJARI FEKI YA KISIASA-BAVICHA

Monday, September 08, 2014

PATROBAS, PASCHAL KATAMBI- AJARI FEKI YA KISIASA-BAVICHA.

Waheshimiwa Viongozi-Makamanda akutukanae hakuchagulii tusi lakini nidhahiri kuwa usilolijua ni sawa na usiku wa giza, sasa natoa giza lililotanda kwa kusema ukweli na naruhusu uchunguzi wa kina wa kiusalama/kiinteligensia kupitia idara ya usalama wa chama (Ninayo iamini sana kwa umakini) ifanye kazi tena na tena juu ya hili pia ikibaini ichukue hatua kali, Tusibakwe kimawazo tukaamua bila tafakari… huu ni woga wa mtu kushindwa kabla ya kura kupigwa ama uvivu wa kujenga hoja zitakazo wasaidia vijana na si majungu yakayowagawa…wahenga walisema kunguru mwoga hukimbiza mbawa zake…na pia mti wenye matunda ndio upondwao mawe…watu kama hawa situ kuwapuuza bali wapaswa chukuliwa hatua za kinidhamu washindwapo kuthibitisha kwa nyaraka na vielelezo (by brilliant and tangible evidence to help our beloved peoples' party CDM) kuhusu kuchafua watu, leo kwangu kesho kwako. Msingi wa haya yote ni mtu kutaka kujipunguzia upinzani ama kupita bila kupingwa kwa kuwaundia fitna na zengwe wagombea wenzake.

Ukweli Ni Kwamba; 
Mimi PATROBASS, Paschal Katambi nimekuwa mwana CHADEMA tangu 2005 nilivutiwa sana nakuiamini katiba na Ilani ya CHADEMA na hoja za mgombea ubunge Shinyanga mjini wakati huo Mhe. Hayati Bob N. Makani nikahamasika na kushawishika zaidi nilipomsikiliza kwa makini Mgombea Urais (CDM) Mhe. F.A. Mbowe, maneno yao hakika yalinikumbusha niliyoyasoma darasani katika masomo ya liwaya na historia yaliyojikita katika agizo la watu,viongozi na serikali kutenda na kusimamia misingi ya utu,haki, umoja, upendo, amani, usawa, na mshikamano ndivyo huleta maendeleo katika jamii yoyote ulimwenguni. Baada ya kumaliza kidato cha sita ilinilazimu kusoma Sheria ngazi ya shahada ya kwanza naya pili katika sharia za uchumi baada ya kuzawadiwa na chuo kwa kufanya vizuri katika degree ya kwanza.

Hoja 1. Nimekua mwanachadema mwaminifu tangu masomoni Sekondari, Chuo Kikuu hadi Kazini na kushiriki kazi zote na kushika pia kushinda nafasi nyingi za uongozi katika kukijenga Chama bila woga kwani najiamini na ninamsimamo katika mambo ya msingi na utetezi wa haki na usawa kwaajili ya CHADEMA na taifa, Viongozi wa juu katika chama ni mashahidi.

Hoja 2. Naaminika na naheshimu watu wote Nimetumikia nafasi zifuatazo kwa uaminifu, uadilifu, tija na manufaa ya wengi toka s/msingi hadi chuo kikuu :- kilanja, Chuo kikuu Serikali za wanafunzi- m/mkt tume marekebisho katiba SAUTSO, Katibu Mkuu SAUTSO, MKt Kamati maalumu ya Sheria Umoja wa Marais wa vyuo vikuu Tanzania –Tuliipinga kisheria na hoja Serikali kuondosha jina la Rais na Waziri vyuo vikuu, Tulitetea haki ya kupiga kura wanafunzi 2010 hadi Mahakama kuu nikiongoza jopo, Waziri wa Sheria, Mkt Tume ya Uchaguzi SAUTSO, Kwa CHADEMA nimekua kiongozi tangu 2007 hadi leo katika nafasi mbalimbali za ujenzi na uhamasishaji kukuza Chama bila unafiki wala woga kwani sinatabia ya kumuogopa mtu bali kuheshimu kwa kadri ya matakwa ya mila,tamaduni,desturi, sharia, taratibu na kanuni zinavyosema na matakwa ya wengi. Tanu 2007 hadi leo mi nikiongozi wa CHADEMA nafasi mbalimbali JE? BAVICHA SIO CHADEMA…au TATIZO NI MIMI KUOMBA NAFASI YA MKT-BAVICHA kulikoni? Wenye akili na nia njema na chama chetu wanajua… nafasi hiyo si ya mzaha,kuuzia sura wala kujifunzia uongozi ni nafasi ya kupanga na kutenda bila woga wala njaa.

Hoja 3. Jitihada na uaminifu wangu katika chama hauwezi potoshwa na watu wanaotaka madaraka kwa njia haramu, CHADEMA ni Chama makini kuliko vyote, kinawataalam, wasomi wabobevu na intelijensia madhubuti na thabiti kuliko hao wanaozusha maneno kwa kutaka wachaguliwe wao, hata kama ni uhuru wa mawazo au kuongea unamipaka na usitumike vibaya kupotosha kwa maslahi binafsi.

Hoja 4. Kuhusu kazi niliyokuwanayo hata makao makuu na uongozi wajuu CDM wanajua na nimekifaa vipi chama na wanachama mi mwanachama asietiliwa hata tone la shaka. Taarifa za kiusalama zinasema zimebaini Kuna mtu aitwae MW nawamgombea mwenzangu ndio wanapika skendo hizi kwa tama na kulipiza visasi na sasa wanamtumia mmoja wa waandishi nguli kufanya/kupanga njama za kunichafua kisiasa kwa kulazimisha kunihusisha na Diallo ama CCM kwa kigezo nilikua nafanya kazi hapo. Wenye akili wanajua CHADEMA haina viwanda, haina makampuni haiongozi Serikali hivyo wana CHADEMA wasomi na wasio wasommi watafanya kazi popote KWA MUJIBU WA SHERIA na si matakwa ya mwajiri (Ukiwa muislam ukaajiriwa na mkristo haikulazimu ubadili dini kwani haihusiani na itikadi hizo) Tuhukumu watu kwa ukweli na haki si kutumia elimu vibaya kupotosha na kupika maneno, hata kama nikikosa nafasi mnayoitaka kwa udi na uvumba bado nitakua mwanachadema imara nisieteteleka wanaonijua wanafahamu hili CCM nawashirika wao ipo siku mtakwama na hakuna atakae ishi milele kina Ghadafi na ubabe wao na uroho wa madaraka walifanya kila njia lakini mwisho ulifika.Nawasamehe bure tujenge hoja tujenge chama 
NIWAKUMBUSHE - ADUI YETU No. 1 ni CCM na WASHIRIKA WAKE… Kwa kushindwa kuondoa Ujinga, Umaskini, Maladhi, Ubaguzi na Ufisadi kwa Watanzania. Viongozi wazushi na wafitini tusiwape nafasi leo kwangu kesho watazusha kwako NANI ATABAKI SALAMA? Tunene na kutenda kwa haki na usawa uzuri tumepata taalifa za kiusalama zimesha wabaini na sasa mnavikao vya kupika skendo na fitna ili mnichafue kisiasa kwa bahati nzuri sikuhizi Watanzania sio wajinga tena watawapuuza tu.

Na, PATROBASS, K. PASCHAL = WABILLAH TOFIQ.


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments