Nadhani mnafutatilia habari na siku hizi za karibuni kuna sakata la Mtoto Happiness anayepotea na kuonekana katika mazingira ya Ajabu. Mara alionekana Zanzibar kasafiri na Ndege bila kuonekana. Akapatika na Mzazi (mama yake) akapempeleka nyumbani huko Tanga. Mtoto huyo alipotea tena huko nyumbani na alipatikana Dar. Jana kwenye ITV alionekana Kituo cha Kati cha Police. Maelezo ya mama ni kwamba alimpotea tena katika mazingira ya kutatanisha.
Alitoboa zaidi kuwa chanzo cha matatizo ya Mtoto ni baba yake, aliishie Mara au Musoma (Pole sikumbuki vema hapa) Kwa namna moja au nyingine chanzo cha matatizo ya mtoto inaonekana ni baba yake. Naona ukweli wa jambo hili unabaika kwa jinsi alivyojibu simu ya mwandisha wa habari jana kwa kiburi na jeuri na kutokujali kuwa mtoto wake anateseka.
Kwa ufupi mtoto huyu anaishi kwa nguvu za PEPO. Anaota madudu ya ajabu na alikiri kuwa anasafiria UNGO. Mtoto huyo anaweza kufunguliwa na MAPEPO kwa kwa nguvu ya SALA NA KWA JINA LA YESU. Ombi kwangu kwa wachungaji wote. TUMWOMBEE BINTI HUYU afunguliwe. Waliooko karibu naye wamtafute na kumwombea. Sisi tulioko Mbali tutafunga na kusali Juu yake. Hakika ATAPONA KWA JINA LA YESU.
Pili kwa akina dada, wasizoee kufuata mabwana na hata kazaa nao bila kuwajua. Oneni kuwa ni aibu kumpenda mtu hata kulala naye na hata kuzaa na mwanamke/Mme bila kumjua ametoka katika mazingira gani, familia gani nk. Mnakutana siku moja tu, na kuangukia DHAMBINI na hatimaye unazaa na JINI. Hakika utapata taabu maisha yako yooooote. Mnaona jinsi mama yule anavyohangaika kuhusu Binti yake. Bwana anakula raha zake na tena anakejeli. Je mama yule ana raha gani?
Jamani tuchunge maisha. Na pia tuepuke ZINAAA. Zinaa itatupeleka MOTONI!
Nawakilisha
KESSY
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments