[wanabidii] Kwanini Lowasa hatapitishwa Kugombea Uraisi na ccm 2015.

Saturday, September 13, 2014

Labda tuongee kwanini Lowasa hatapitishwa Kugombea Uraisi na ccm 2015.

1) yuko nje ya serikali karibu miaka 10 sasa na mara nyingi na katika nchi nyingi rais anatoka miongoni mwa mawaziri, sio miongoni mwa wabunge.

JIBU; Hakuna Sheria wala kanuni inasema anaekua Nje hawezi kuwa historia ya Dunia Ime prove kuwa wapo aambao hawajawahi kuwa Mawaziri wamekua Marais duniani hii ni Hoja ilotokana na Kasumba tu. Obama Hakua waziri ktk serekali ya Marekani kwahiyo hata mbunge anaweza because serikali inaendeshwa kwa Mifumo iliyotengenezwa kwa sheria na Kanuni na Msingi mkuu Katiba.Kwa hiyo hii si Hoja ya Msingi.

2) hoja ya kujiuzuru kwake itakipa ccm wakati mgumu kuomba kura na kumtetea na kwa kumtetea tayari JK anajipaka tope mwenyewe na ccm kadhalika.

JIBU; Jk hawezi kujipaka Matope because Edward akichukua Political Responsibillity kama Kiongozi Kujiuzulu na hapa alionyesha Uthubutu wa hali ya Juu kwa Kiongozi kuchukua hatua za Uwajibikaji kama alivofanya Mzee Mwinyi,na hii ilikua kuipa Heshima serikali na Umma kujua Ukweli wa Jambo lenyewe,CCM haiwezi kuwa na wakati mgumu kumtetea because Hakukua na Kosa juu ya Jambo lile Edward alikua anasimamia Maamuzi ya Baraza la Mawaziri,na Mkataba ule ulinunuliwa na Dowans tukaleta Siasa Tukashtakiwa tukalipa,Tukazuia Mitambo kununuliwa na serikali, ikanunuliwa na Symbion wakatuhudumia Tukaamua hivi karibuni Kuleta IPTL ichukue nafasi ya Symbion na leo Mitambo ile inahamia Nchi ya Jirani.

3) akijaza form atakuwa anashindana na Pinda na Sumaye kwenye kundi la mawaziri au waliokwisha kuwa mawaziri; ccm haiwezi kukata jina la aliye madarakani na kupitisha la aliyejiuzuru kwa kashfa.

JIBU; Edward hajajiuzulu kwa Kashfa angekua Amefanya Ufisadi ama ametumia madaraka yake vibaya Richmond ilipelekwa mahakamani wakatushinda, Na edward hashindani na Pinda wala sumaye kwani hakuna kinachowafanya washindane hawa ni viongozi wenye sifa na uwezo Tofauti na Historia Tofauti ya Utumishi wa Chama na Serikali kila mmoja atapimwa kwa sifa na Mapungufu yake,na Katika hilo edward amewazidi mbali sana hawa ktk Sifa kuu alosema Mzee Mkapa 2005 "Tuleteeni anae kijua Chama na sisi wapiga kura tunapofika mkutano mkuu hatutafuti Rais tu tunatafuta Mrithi wa mwenyekiti wa CCM"

4) Lowasa aliogopa kugombea NEC kupitia kundi la kifo, hii ni ishara tosha kwa ccm kuondoa jina lake maana kukubalika kwake ndani ya chama hakujapimwa.

JIBU; Edward hakuogopa kugombea Bali alitoa Nafasi kwa wale ambao mawilayani kwao hawakubaliki waende huko kwenye kapu,na kuheshimu kwa Vitendo mabadiliko aloleta Mkiti wa CCM kuwa Utumishi wa Chama usogezwe Kwa wanachama na kwakuwa edward anafaham kuwa wajibu wake kwa sasa ni kuwatumikia wana Monduli na wao wamempa heshima ya kuwa mbunge basi na UNEC wa wilaya kwa mara ya kwanza aliamua kugombea Wilayani .

5) Kashfa ya Richmond iliyokichafua chama hadi kikashindwa kujivua gamba.

JIBU; Richomond Haikua Kashfa ya edward bali ni siasa ilitengenezwa na wale waliopinga Mtandao 2005 na wale ambao ndani ya Mtandao walikua wanataka Uwaziri mkuu na kutaka kuhujumu serikali ya JK wakaungana kupotosha Umma juu ya hili lakini Mkataba ule ule Ulihamia Dowans na baadhi ya Mitambo ya Richmond na Baadae kuwa symbion, na wala dhana ya Gamba haikufanikiwa kwakua ilijengwa ktk Msingi wa Uongo,na Dhamira chafu dhidi ya watu flani,na walileta dhana hii na kusimamia ni wale walompiga JK 2005.

6) Kuwemo kwake kwenye List of Shame ya Dr Slaa inamfanya awe kitafunio kizuri kwa wapinzani endapo ccm itafanya kosa.

JIBU list of shame ni hoja Dhaifu na List hii haikumtaja Edward Peke yake ili taja watu 11.kama edward kutajwa ni uchafu basi wote walotajwa ni wachafu na kama wote ni wachafu je tujiulize wachafu wanaweza kumhukumu mchafu mwenzao?Hii list ilitengenezwa kwa Ajili ya Kudhoofisha Serikali ya CCM iliyokua ina Umri wa miaka 2 na waliotangaza na wapinzani na walotajwa almost 90pc ni wanamtandao waloshiriki kumsaidia JK,nia ilikua kudhoofisha serikali ya JK.

7) Afya yake intosha kuondoa jina lake hasa ukitilia maanani kwamba ccm wamejifunza kupitia kwa rais Satta wa Zambia.

JIBU;Edward hana Tatizo la kiafya hoja hii ndani ya CCM si Mpya hata JK 2005 walisema ni mgonjwa na wanaoibeba hoja hii sasa ni wale wale walompinga JK 2005 wali dai jk mgonjwa ndo Hao wanasema leo Edo mgonjwa.Hii si hoja ya Msingi na Haina mashiko.

wapinzani kila kona wakaubiri machafu yake.

Jibu :Wapinzani kutukana mwana CCM sijambo la Ajabu hata akija malaika watasema.


Ccm itakuwa na Kazi kubwa Sana ya na sabuni ya unga. :

JIBU hakutakua na Kazi yoyote kuosha wala kusafisha,bali kutakuwa na kazi ya kuwaeleza watanzania tutawafanyia nini


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments