[wanabidii] VIONGOZI WA CHADEMA MKOA WA TANGA WAHAMIA ACT TANZANIA

Tuesday, August 26, 2014
Ama kweli kwa jirani kwa dhidi kuteketea na mzimu wa Zitto wazidi kuwamaliza. 
Gazeti ka mwananchi la tarehe 26/8/14 ukurasa wa tano limetoa taarifa ya kujiuzulu kwa Kamati Tendaji ya wilaya ya Tanga mjini. 
Wamejiuzulu kwa kukasirishwa na kitendo cha uvunjifu wa katiba ya chama hicho. 
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari aliyekuwa Katibu wa chadema wa wilaya ya Tanga Khalid Rashid anasema"nimeandikiwa barua ya kusimamishwa uongozi kinyume na taratibu na kupewa tuhuma kumi miongoni mwa hizo ni kupingana na maelekezo ya Kamati kuu kuhusu kumvua nyadhifa aliyekuwa naibu Katibu mkuu Zitto Kabwe"
Khalid anaendelea kusema Mimi na iliyokuwa kamati ya utendaji tumeamua wote kujiunga na chama cha Umoja wa mabadiliko na uwazi (ACT-Tanzania) na tutahakikisha tunakijenga chama mkoa wa Tanga kwa kufanya ziara wilaya zote kuanzi mwezi wa Tisa mwaka huu. 
Wajumbe wa Kamati ya utendaji waliojiuzulu na kujiunga na ACT ni:-
Kisua mrami
Hussein baruti
Mohamed kidege
Hassan Maulid
Juma yunusi
Zaina manyeki
Seleman hassan
Mwanaisha kambimbaya
Mohamed sululu.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments