Katika miaka ya 1900 mwanaharakati Mao Ze Dong akiwa kama kiongozi wa upinzani wa nchini CHINA, walijiunga na chama tawala katika hali ya kukurupushwa (muungano usio rasmi) kumpiga aduiambae ni nchi ya JAPAN walipoivamia nchi hiyo (CHINA) kijeshi. Baada ya kumshinda adui JAPAN na kumuondoa nchini kwao wakauvunja ule umoja wao wa kukurupushwa na kuanza uhasama kama kawaida...
Leo katika kile kilichoitwa UKAWA wameamua kuungana kwa dhana ya kutaka serikali tatu na si kwa maslahi ya katiba ya wananchi kwakua vyama hivi vinamisimamo yake na ilani zake na kujifanya wamesahau tofauti zao za kisiasa za hapo awali hadi kufikia CHADEMA kuwaita CUF tawi la Ccm..
Mfano mmoja wa kuthibitisha kwamba yapo masuala ambayo wangetofautiana ni suala la mahakama ya kadhi ambapo kwenye ilani za CHADEMA suala hili lilikua mwiko ilhali kwenye ilani ya CUF ni suala lililokua limepewa kipaumbele..
Nachelea kusema iwapo ule mchakato wa katiba ungeendelea na wote wamo ndani ya bunge bila ya kua na kitu chochote kinachowaunganisha basi ni dhahiri shahiri wangeshikana mashati wenyewe kwa wenyewe (Cuf vs Cdm)...
Siku zote hakuna umoja ambao unadumu hasa ule wa kisiasa kwakua malengo, ilani na sera za vyama husika hua tofauti isipokua kama waliungana kwa hiari bila ya shinikizo lolote.
Hatima ya umoja huu itakua ni kila mmoja kumtupia mwenzie lawama na kuanza kumtafuta mchawi ni nani na kuvipa vyama vingine mwaya wa udhaifu huu kuchanja mbuga..
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments