[wanabidii] CYBER BULLYING - UNYANYASAJI KWENYE MITANDAO

Sunday, August 31, 2014

CYBER BULLYING – UNYANYASAJI KWENYE MITANDAO 


Betty Ndejembi ni msichana mrembo na mwanamitindo , anatumia sana huduma za mitandao ya kijamii kwa ajili ya shuguli zake mbalimbali za kujiingizia kipato na kujitangaza zaidi .


Siku moja alibakwa mpaka akapoteza fahamu , akaokotwa na watu akapelekwa hospitali , alipofika hospitali aliendelea kutumia mitandao ya kijamii kwa ajili ya kufahamisha wenzake anavyoendelea kwa nia nzuri kabisa .


Jinsi alivyokuwa anafahamisha umma kuhusu maendeleo yake ndio baadhi yao walitumia fursa hiyo kumtukana , kumnyanyapaa , kutumiana picha zake na dhihaka nyingine nyingi kwa njia ya mitandao hiyo hiyo .


Msichana Betty alifariki dunia baadaye wakati anaendelea na matibabu , lakini matusi aliyovurumishiwa , maneno aliyoambiwa na unyanyasaji mwingine umeleta historia mpya katika matumizi salama ya mitandao ya mawasiliano .


Jijini arusha  kijana mmoja kutwa na mke wa mtu , akadhalilishwa huku akipigwa picha , zile picha zikawekwa kwenye mitandao kadhaa ya kijamii , baada ya siku chache yule kijana alionekana amejinyonga chini ya daraja .


Huko marekani dada mmoja anayeitwa Rebecca Ann Sedwick , aliamua kujitoa uhai baada ya kudhalilishwa kupitia mtandao wa kijamii unaoitwa Ask FM na Kik Messenger .

 

Kitendo alichofanyiwa Betty na huyo Kijana kwa kiingereza kinatwaita CyberBulling yaani mtu kutumia njia za mawasiliano kwa nia ya kuumiza , kudanganya au kumdhalilisha mwingine , labda kwa maneno , picha , sauti , video na vingine vingi .


Vitendo hivi ni kama kutumia picha ambayo mwenye nayo hajaruhusu , kuandika habari za uwongo haswa za udaku , kuuandika au kutoa maoni ambayo si ya kweli kwa nia ya kudhalilisha au kuumiza , kudanganya kuhusu bidhaa au huduma Fulani kwa nia hiyo hiyo .


Tafiti mbalimbali zilizofanyika zinaonyesha watu wengi wanaohusika katika matukio ya unyanyasaji kwa njia za mitandao ni vijana au makundi ya vijana pia zimeeleta madhara haswa vifo .


Mimi binafsi niliwahi kukumbana na sakata kama hili , lakini ilimkuta rafiki wa rafiki yangu mmoja , yeye alikuwa na mpenzi wake , kumbe wakiwa kwenye starehe yule mwanaume alikuwa na tabia za kumpiga picha .


Siku ikafika hawakuelewana ikabidi kila mtu aendelee na maisha yake , yule kijana akaingia facebook akatengeneza jina bandia akaweka picha za yule binti na kuwarushia watu wa karibu wa binti halafu akafuta lile jina .

Binti alienda polisi kutoa taarifa , polisi wakaomba ushahidi wa picha , lakini ndio hivyo jamaa alikuwa ameshafuta mpaka jina , kwahiyo wakaomba msaada , nikawapeleka polisi makao makuu kitengo cha CYBERCRIME .


Polisi waliweza kupata taarifa zote zinazohusu yule kijana kwenye mitandao ya kijamii na wakaenda kumkamata alipokuwa anaishi wakakagua simu zake , kompyuta na nyaraka nyingine wakapata picha zote kama ushahidi na sasa hivi huyu kijana yuko jela .


Huko mitaani kuna kina betty wengi wamezushiwa , wamedhalilishwa , wamepakaziwa na kutengenezewa habari nyingi mbaya na za kuumizwa na watu wanaowajua au kutowajua lakini wanakaa kimya lakini madhara yake ni makubwa tu .


Inawezekana una ndugu yako , jamaa yako , wewe mwenyewe au mtu mwingine yoyote umeona amedhalilishwa au anataka kudhalilishwa , ni vizuri utoe taarifa kwenye vyombo husika ili wafanyie kazi kwa haraka na mapema zaidi kabla ya tukio kuwa kubwa zaidi .

Unachotakiwa kujua ni kwamba mawasiliano yote kuanzia simu , facebook , watsup , instagram na mengine mengi yanahifadhiwa , hata kama mtu alifuta , kampuni inayotoa huduma husika huwa inasehemu yake ya kuhifadhi mawasiliano yote .


Tushirikiane pamoja ili kuweza kumaliza au kupunguza tatizo hili la unyanyasaji kwa kutumia vyombo vya mawasiliano ili tuweze kuwa na jamii iliyostarabika kwenye mitandao haswa ya kijamii na watu waweze kutumia mitandao hii kwa faida na uhuru zaidi bila kuogopa au kuogopana .


YONA FARES MARO

0786 806028

 



--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments