Leo kuna maCCM wawili nimewakuta kwangu wakiwa na daftari wanapita nyumba kwa nyumba wanaandikisha wakazi eti wakisingizia kwamba wanaandikisha wakazi ili wapewe vitambulisho vya uraia! Ilibidi niwaweke chini ya ulinzi makada hao wa CCM kwa kuingia nyumbani kwangu bila kibali na kuanza kuwahoji. Baada ya kuwadadisi sana nikagundua kwamba hawa washenzi wamekuja kuandikisha majina kinyemela ili baadaye wayachambue na kuyachakachua kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa wa 2014 na uchaguzi mkuu 2015.
Nilijaribu kuwanyanganya yale makaratasi yao lakini mmoja wao aliyadaka na kujaribu kukimbia nayo. Kwa bahati mbaya, karatasi moja lilidondoka chini kwenye mkeka waliokuwa wamekaa nikaipiga picha ijapokuwa haikuonekana vizuri kwa sababu ya purukushani. Nilipoona wananizidi nguvu niliwafungulia mbwa wawang'ate. Mbwa alifanikiwa kumkamata mmoja wao na kuuachana msuli aliokuwa ameuvaa. Ana bahati sana hutu mshenzy, asingekuwa amevaa amevaa msuli mbwa angemrarua mpaka akome. Hatimaye walifanikiwa kukimbia na kutokomea kizani. Nimeripoti hili kama tukio la kuvamiwa na vibaka nyumbani kwangu lakini poliCCM wamegoma kunipa RB kwa kisingizio kwamba mpaka niwataje majina yao, nami sikubahatika kuwauliza majina.
Nijuavyo ni kwamba hakuna utaratibu kama huu wanaofanya hawa washenzi. Tangu lini raia wanaoandikishwa uraia wakasakwa nyumba kwa nyumba na makada wa CCM? Kama labda mimi ndio sijui utaratibu, naomba nifahamishwe isije ikawa nimewabana bure hawa makada bila kujua. Watu wa Dar ambako tayari zoezi hili lilishapita naomba mtujuze utaratibu ulikuwaje. Mimi ninachojua ni kwamba raia wote wanaostahili kupewa vitambulisho huandikishwa kwenye ofisi ya serikali ya kijiji/mtaa. Kila anayehitaji kitambulisho huenda kujiandikisha huko. Sasa iweje hawa makada wa CCM waje kuwasaka raia nyumba kwa nyumba?
Hivi hawa CCM ni lini wataacha WIZI wa kura? Ama kweli hawa wanahizaya wamezoea kuishi kwa ulaghai na hii laana ya ulaghai ndiyo itakayowapoteza kabisa katika uchaguzi wa 2014/2015! Baada ya kuona kwamba hawana pa kutokea, ndipo wameamua kuwatumia makada wao kupita nyumba hadi nyumba ili waanze kucheza rafu mapema. CCM nawaambia kwamba wananchi wa leo sio wale wa enzi za "zidumu fikra za mwenyekiti". Na msipoangalia mtavunjwa miguu, ikiwa mtaendelea kuingia kwenye nyumba za watu kama majizi…mtaitiwa wezi na kuuliwa kama vibaka. Shauri yenu.
0 Comments