[Mabadiliko] Neno Fupi La Usiku: Heri Ya Mariadhiano Kabla Ya Vurugu, Kuliko Vurugu Kisha Mariadhiano...

Monday, August 11, 2014


Ndugu zangu,

Leo alfajiri nilikuwa Mwenyekiti wa mjadala kuhusiana na kipindi cha 'Soko la Habari Kariakoo' kinachorushwa na Redio Kwanza Jamii kwa kushirikiana na Redio Nuru FM, zote zenye makao yake Iringa.

Ni kuhusiana na mivutano hii ya mchakato wa Katiba. Nilitilia mkazo umuhimu wa pande zenye kukinzana kuisogelea meza ya mazungumzo.

Maana, hili la Katiba tayari ni mgogoro wa kisiasa kwenye jamii. Na siku zote, walio kwenye mgogoro hawawezi kuikimbia meza ya mazungumzo. Na hata wakijaribu kufanya hivyo, wataumizana, na mwishowe watalazimika kuirudia meza, kuzungumza ili kuyamaliza.

Naam, meza ni neno la Kireno na lenye maana pana kwa maisha ya mwanadamu. Na zamani sana kabla ya ujio wa Wareno, wahenga wetu hawakuijua meza. Mambo yao mengi ikiwamo migogoro ilipatiwa ufumbuzi chini ya kivuli cha mti, na jadi hiyo ingalipo. Maana, Uafrika ni imani, na Mwafrika haukimbii mti. Afrika miti mingine ni ' mitakatifu'- Haikatwi. Ni mwiko kuikata,inaanguka yenyewe.

Leo asubuhi nimeelezea hofu yangu juu ya chuki inayojengeka katika jamii kuhusiana na hili la Katiba. Nikaweka tahadhari ya kuwa ni makosa kufikiri kuwa haya tunayoyashuhudia ni madogo, wakati mara nyingi huanza hivi hivi na kuwa makubwa.

Nikatoa mfano wa Rwanda na mauaji ya kimbari ya mwaka 1994. Kwamba Watusi na Wahutu kwa asili ni watu wamoja na wameishi kwa kushirikiana. Lakini, kuna nguvu za nje zilizowafanya wajenge misingi ya kubaguana.

Na kwa vile siku zote chuki huzaa chuki, Watusi na Wahutu, wenye kuishi nchi moja na kuzungumza lugha moja wakafikia kuchinjana kama wanyama.

Na tujiulize basi, ni kwanini sisi Watanzania, wenye kuishi kwenye nchi moja na kuzungumza lugha moja ya Kiswahili, kuwa tunashindwa kukaa chini kuzungumza na kuridhiana katika mambo ya msingi kuhusu nchi yetu tuliyozaliwa?

Na hakika, moja ya mambo yanayonihangaisha sana ni kujaribu kujiuliza maswali na kutafuta majibu ya jinsi sisi Watanzania tunavyofikiri.Inahusu Antropojia ya Kijamii( Social Anthropology).

Nilipata kujiunga na Chuo Kikuu cha Tumaini hapa Iringa mwaka 2006 ili niweze kujifunza jambo hili la Antropolojia ya Kijamii. Hivyo, nikapata bahati ya kufundishwa na marehemu Profesa Mshana juu ya Social and Cultural Anthropology. Baada ya kozi hiyo nikamuaga Profesa wangu na kujiendea zangu. Nyuma nikiwaacha wanafunzi wenzangu wakinishangaa, kuwa iweje nimelipa ada ya mwaka mzima kwa kozi hiyo tu? Kuna waliofikiri kuna ' aliyenituma'!

Nataka kusema nini? Kuwa yanayotokea kwenye jamii yetu kwa sasa si masuala madogo. Tusiyachukulie kishabikishabiki tu. Inahusu uhai wa taifa letu, leo, kesho na miaka mingi ijayo. Nasi hatutakuwepo, maana, muda wetu wa kuishi humu duniani ni mfupi sana.
Hivyo, na tuyafanye yote tukihakikisha Umoja Wetu wa Kitaifa Unabaki.

Maana, hata sasa tunapozungumza juu ya umuhimu mariadhiano, hivi, tumejiuliza; kuwa maridhiano yanajengwaje, na ipi ni mipaka ya maridhiano?

Labda naongea sana. Lakini nikumbushe nilikoanzia, kuwa ni heri ya maridhiano kabla ya vurugu, kuliko vurugu kisha mariadhiano.

Oh! Oh!... Ni Neno Refu La Usiku...! Unaweza kusikiliza..http://mjengwablog.com/habari-za-kijamii/item/13751-sikiliza-kipindi-cha-soko-la-habari-kariakoo.html
Maggid Mjengwa,
0754 678 252

--
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
 
 
For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Mabadiliko Forum" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
To post to this group, send email to mabadilikotanzania@googlegroups.com.
Visit this group at http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania.
To view this discussion on the web visit https://groups.google.com/d/msgid/mabadilikotanzania/CAMD-ye40E0gGY569KLzADRBJV24DN%2BJFV9v4hh%2BdTaRk7WuL_A%40mail.gmail.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments