[wanabidii] Wayahudi Dhidi ya Wapalestina: KWANINI?

Thursday, July 10, 2014
                    Israeli Waliwapenda zaidi Waedomu.
                                -Noah  W. Hutchings
 
 Si Rais Barack Obama, katibu wa Serikali John Kerry, viongozi wa siasa wa Umoja wa Ulaya wala 99.9 asilimia ya raia wa Marekani (ikiwa ni pamoja na vyombo vya habari), wanaojua kwa uhakika ni kwanini Wapalestina Waislamu wanajilipua wakiwa na lengo la kuwaua Waisrael wachache, wengi wao wakiwa wanawake na watoto.
 
Inakisiwa kwa makosa kwamba kama Wapalestina wanawachukia Wayahudi kiasi kikubwa hivyo cha kujitoa muhanga nafsi zao, kwamba Israeli lazima iwe inatenda maovu sana dhidi ya hawa watu maskini wasio na ulinzi. Ili kufikia kwenye ukweli halisi ulio nyuma ya Wapalestina wasio halisi/Wayahudi wafanyao mauaji ya maangamizi, ni lazima turudi nyuma miaka mia nne elfu iliyopita katika historia.
 
Palikuwepo mtu, kulingana na maelezo ya Biblia ambaye jina lake lilikuwa Abraham. Mke wa Abraham aliitwa Sarah. Abraham amewekewa kumbukumbu katika mafundisho  mengi ya ziada ya Biblia. Sarah alimzalia Abraham mwana katika siku zake za umri mkubwa.
 
Wawili hawa wakamwita mtoto wao wa muujiza jina lake Isaka. Baadaye Isaka alimwoa binti aliyeitwa Rebeka. Rebeka akamzalia Isaka wana wawili mapacha. Mapacha hao wakaitwa Esau na Yakobo. Esau alikuwa mzaliwa wa kwanza, ikimaanisha ndiye aliyekuwa mkubwa hata japo kwa dakika chache, alikuwa akipaswa kupata mbili ya tatu ya milki ya baba yake na baraka nyingine za msingi.
 

Imeandikwa katika vitabu viwili vya Biblia, Malaki na Warumi, kwamba hata kutoka tumboni mwa mamaye, Mungu alimpenda Yakobo na kumchukia Esau. Maandiko yanaonyesha sababu yake kuwa sio ile hali ya kiumbe kisichokuwa na hatia na hata kilichokuwa tumboni ambacho Mungu alikichukia, lakini ni vile kizazi chao kitakavyokuwa.
 
Hakuna siri ya kwamba ni kwanini
Mungu akamchukia Esau;
Ni kwasababu Esau alikuwa                       MALAKI 1:3
mwenye maneno machafu.              Je, Esau siye ndugu yake
Alikuwa mwovu. Wakati                Yakobo? Asema Bwana:
Esau alipokuwa katika                      Bali nimemchukia Esau
Mahangaiko yake ,                        na kumpenda Yakobo.
Yakobo alimwibia haki yake             
ya uzaliwa wa kwanza na                         RUMI 9:13
baraka zake. Esau alichukua            Kama ilivyoandikwa
sehemu moja ya tatu ya                    nilimpenda Yakobo na
milki ya baba yake kwenye               kumchukia Esau.
milima ya seira (baadaye iliitwa
Petra na Wayunani), ikiwa mji mkuu wa himaya ya Esau, Edomu (Mwa. 25:30).
 
Ndugu yake Esau ambaye ni pacha mwenzie aliyeitwa Yakobo alikwenda Kaskazini hadi Harani ambapo alienda kupata mali nyingi. Wakati Yakobo alipokomaa kiroho hadi kufikia uwezo wa kutimiza baraka za babaye, Mungu alimpa jina jingine-Israel, (Mwz 32:28). Kwa hiyo vizazi vya Esau walikuwa Waedomu na wazao wa Yakobo walikuwa Waisraeli.
 
Waedomu waliishi nchi isiyo na rutuba ya miamba na mapango. Kama wamiliki wa baraka za msingi., Waisreli wao waliishi katika nchi iliyojaa maziwa na asali.

 Kabla vizazi vya Yakobo hawajaja kwenye nchi ya ahadi, walikuwa kwenye vifungo Misri. Wakati Mungu alipomtuma Musa kuwakomboa Waisraeli kutoka kwenye utumwa wa Misri, walihitaji kusafiri kupitia Edomu ili kufika kwenye nchi ambayo ilielezwa katika urithi wa Abrahamu, kwa Isaka, kwa Yakobo.
 
Hata hivyo wazao wa Esau, wa Edomu si tu kwamba walikataa Waisraeli wasipite kwenda nchi ya ahadi, lakini walitoka nje ya Petra wakiwa na nia ya kumuua kila mzao wa Yakobo. Chuki kubwa namna hii ilitoka wapi? Bila shaka ni kutoka kwenye mila zao za asili walizopokezana kutoka kizazi kimoja hadi kilichofuata wakielezana jinsi Yakobo na uzao wake, Waisraeli, walivyoiba haki ya uzaliwa na baraka zao.
 
Kusini mwa Edomu kulikuwa na Waarabu, mahali uzao wa Ishmael na wanawe walipoishi na kuanzisha ufalme. Baada ya Wanegebu, mzaliwa mwingine - mjukuu wa Ishmael, Naboth, alihamia Edomu katika karne ya 15B.C. Edomu alichukuliwa ni wa Arabia Kaskazini.
 
Kaskazini mwa Edomu kulikuwa na Wamoabu na wa Amoni vizazi vya Lutu kupitia uhusiano wa kughadhibisha na mabinti zake. Magharibi mwa Edomu, baada ya Waisraeli kuweka makazi yao katika nchi ya Kaanani vilikuwapo vijiji vya Waisrael vilivyokuwa vimejitenga kutoka Beersheba hadi Eilati.
 
Kumbukumbu za kibiblia zinawaelezea Waedomu kama watu wa vita, wenye hasira, wagomvi, waongo na jamii ya watu wasio waaminifu.
 

 Waedomu wangewauza wateka wa Waisraeli na Wamoabu utumwani; na vikundi vya wavamizi kutoka Petra walikuwa wakishuka kuvuka Araba na kupora kwenye vijiji vya Waisraeli na kuwaua wenyeji wa vijiji vile. Hatimaye mfalme Daudi akachoka kuwalinda wenyeji walioishi kusini mwa wavamizi wa Edomu kwa hiyo akapanga vita kinyume na Waedomu na aliwaweka walinzi katika Edomu kulinda amani (1Nyak. 18:13).
 
Suleimani kinyume na maonyo  ya Mungu, alioa wanawake wa Kiedomu na wale walinzi wakaondolewa. Wavamizi wa Edomu wakarudia tena kuwavamia Waisraeli na baada ya kila uvamizi Waisraeli walikuwa wakijibu shambulio, sawa sawa na Waisraeli wanavyofanya leo- katika mgogoro wao na Wapalestina.
 
Katika mwaka 800BC, mfalme Amazia aliwaua Waedomu elfu kumi katika bonde la chumvi (Arava), kusini mwishoni mwa bahari ya chumvi, kisha akawachukua mateka elfu kumi wa Waedomu na kuwarudisha Petra na kuwatupa chini kutokea kwenye jabali lililokuwa refu (2Wafalme 14:7).
 
Hata hivyo Yakobo na Esau walikuwa ndugu, na Waedomu na Waisraeli walikuwa makaka, Mungu aliwaonya Waisraeli wasiwachukie Waedomu kwa sababu walikuwa ndugu zao. Lakini Mungu pia aliwaonya Waedomu kwamba kwa vile walisababisha vurugu kinyume cha nyumba yao wenyewe, Israeli, baadaye jamii hiyo itaharibiwa. (Obadia 1:8).
 
Vita kati ya Waedomu na Waisraeli iliendelea. Katika siku za Yehoshafati, Waedomu wakafanya  ushirikina na Wamoabu na Waamoni ili kuiharibu Yerusalemu.
 
 Muungano wa nguvu hizo ukapanga mashambulizi katika bonde la Kidroni. Lakini Waedomu hawakuweza kupigana licha ya fungamano lao, na majeshi hayo matatu yakaingia kwenye mapambano wakichinjana wenyewe kwa wenyewe. Yerusalemu ikaokoka.

Kama miaka 600BC, himaya ya Babeli ilijitanua mashariki na magharibi. Yuda alitishwa, na katika hali ya kukata tamaa wakafanya mapatano ya kusaidiana kwa mkataba na maadui zao wa Edomu. Waedomu wakaungana na Wababeli wakawasaidia kuuharibu Yerusalemu na hekalu. Tendo hili pia linaonyesha/fafanua udanganyifu na asili ya Waedomu ya kutokuwa na waaminifu.
 
Kando ya mito ya Babeli ndiko tulikoketi, tukalia tukiikumbuka Sayuni. Katika miti iliyo katika yake, tulivundika vinubi vyetu. Maana huko waliotuchukua mateka walitaka tuwaimbe; na walituonea walitaka furaha; Tuimbieni baadhi ya nyimbo za Sayuni. Tuimbeje wimbo wa BWANA katika nchi ya ugeni?
 
Ee Yerusalemu, nikikusahau wewe, mkono wangu wa kuume na usahau. Ulimi wangu na ugandamane na kaakaa la kinywa changu, nisipokukumbuka. Nisipoikuza Yerusalemu zaidi ya furaha yangu iliyo kuu. Ee BWANA uwakumbuke wana wa Edomu, siku ya Yerusalemu. Waliosema, Bomoeni, Bomoeni hata misingini!
 
Ee Binti Babeli, uliye karibu na kuangamia, heri atakayekupatiliza, ulivyotupatiliza sisi. Heri yeye atakaye wakamata wadogo wako, na kuwaseta wao juu ya mwamba.
 
 
Katika siku hizo makabila kuchanganyika ili kulishinda Taifa lililoshinda kuharibu utambulisho wao ili kupinga kuingiliwa; lilikuwa jambo la kawaida. Wayahudi wasomi wazuri na wale wenye nguvu nyingi za mwili walichukuliwa mateka hadi Babeli.   Zaburi 137:1-7
 
Kisha Waedomu waliondolewa Petra na kuingizwa Yuda. Wanegebu, wazao wa mjukuu wa Ishmaeli-Naboth, walihama kuelekea juu kutoka kusini mwa Arabia na kuichukua Edomu. Hii ilikuwa imetabiriwa katika Obadia 1:19, "Na watu wa Negebu wataumiliki mlima wa Esau na watu wa shefela watawamiliki wafilisti, nao watalimiliki konde la Ephraim¼"
 

Wafilisti walimiliki konde la Efraimu katika mateka wa Siria na Wanegebu kutoka Arabia wakati mateka wa Babeli walimiliki Edomu, ikiwa ni pamoja na Petra. Waedomu wakakaa Yuda. Baada ya miaka sabini ya kutekwa na Wababeli, mabaki ya Wayahudi waliruhusiwa kurudi kuujenga tena Yerusalemu pamoja na hekalu.
 
Wajenzi Wayahudi iliwabidi kujenga wakiwa na silaha zao upande mmoja ili kupigana na Waedomu ambao walikuwa wakijaribu kuzuia mradi wa ujenzi. Kurudi kwa Wayahudi kutoka kwenye utumwani Babeli ili kujenga upya Israeli ilikuwa tendo gumu na la muda mrefu.
 
Uhamisho wa kitaifa ulikuwa mgumu pia kutokana na mwendo wa majeshi yaliyowashambulia katika nchi yaliyotokea Misri na Siria. Ingawaje chini ya Makabeshi Waisraeli walirejesha kiasi fulani cha utukufu wao wa awali, Warumi walikuja Mashariki ya Kati na taifa hilo likawa tena chini ya mamlaka ya serikali ya kigeni.
 
Yusufu alinukuu matendo ya Waedomu (walioitwa na Warumi  Waidumeni) wakati wa kipindi hiki. Warumi hawakuweza kuwaweka Wayahudi kwenye nafasi serikalini, kwa hiyo waliwateua vibaraka wa Kiedomu kusimamia ulinzi uliohitajika na shughuli za kijamii.
 
Maherode walikuwa Waedomu. Wakati Warumi walipoharibu Yerusalemu na Hekalu mwaka 70A.D Wayahudi wengi waliuwawa au kuuzwa utumwani au walikimbilia nchi nyingine. Waedomu wakiwa hawana chochote cha kuhofia kutoka kwa Warumi walikaa kwenye nchi na kuwa mababu wa Wapalestina wa leo.
 

Yusufu amenukuu sehemu nyingi katika vitabu vyake viwili matendo maovu ya Waedomu kwa Waisraeli. Katika Vita ya Wayahudi  Kitabu cha 4 sura ya 5 ni tukio la mara moja la Waedomu la ukichaa na ukatili:
 
¼hata Waidumeni hawakumbakiza mtu yeyote; kwa kuwa kama asili yao ilivyo ni Waberiberi kwa kiasi kikubwa na taifa la wamwaga damu¼na wamefanya kwa mtindo ule ule kama wale waliosihi kwa ajili ya maisha yao wale waliowapiga; kiasi kwamba waliwakimbiza na panga zao wao waliotamani wakumbuke uhusiano uliokuwepo kati yao na kuwaomba wawe na staha kwenye hekalu lao la kawaida.
 
¼hekalu la nje lilifurika damu, na siku ile, kama ilivyotokea kuona miili iliyokufa elfu nane na mia tano pale. Lakini ghadhabu ya Waidumeni haikutoshelezwa kwa uchinjani huu, lakini sasa waliendelea hadi jijini (Yerusalemu), na kupora katika kila nyumba na kumchinja kila mmoja waliyemkuta.
 
Yusufu alisema Waedomu walikuwa vichaa waliopindukia na watu wakatili wakiwa na dhamira ya chuki kwa Wayahudi. Mwanahistoria huyo anahitimisha kwa kusema chuki hii inapoachiliwa haijui sababu wala mipaka.
 
Filo wa Alexanda aliandika hivi kuhusu Waedomu;
 
¼Waedomu hawa wa kidunia wakiwa na uchungu uliopindukia, waweza kututisha kwa vita visivyosuluhika¼
Waedomu hawa wa kidunia wanafikiria ni sahihi kuweka uzio barabara za mbinguni na za ufalme na zilizo njema na sababu za kiungu za kuweka uzio barabara zake na kwa wote wanaofuata mawazo yake¼kwa kuwa magonjwa ya nafsi kwa kweli si  tu kwamba ni magumu kutibu bali hata hayathibiti.

 
Kazi ya Filo, uk.172-173 (The work of Philo, pg 172-173)
 
Inaweza kuonekana kuwa jambo lisilolinganishwa kwenye ufahamu wa yeyote kwamba mfalme wa Waedomu, Herode, aweza kutoa amri ya watoto wote wa Wayahudi chini ya miaka miwili wa Bethlehemu na maeneo yaliyowazunguka wauwawe. (Mat.2:16).
 
Lakini tukirejea nyuma katika historia ya PLO (Mkataba wa Wayahudi tangu mwaka 1920), tunagundua tukio hadi tukio; jambo hadi jambo ambapo magaidi wa kipalestina waliwaua watoto wa shule wa kiyahudi kwa makusudi. Ndani ya Israeli siku za leo, wakati unapoona kundi la watoto wa shule, utaona na askari wenye silaha wakiwalinda.
 
Wauaji wa kujitoa mhanga wa PLO wanatafuta makundi ya vijana wadogo wa umri kati ya miaka 10 hadi 20 ili wawaue, au wa mama wenye watoto wadogo na walio wachanga. Kulengwa kwa watoto wadogo kwa wauaji hawa wa kujilipua kumezungumziwa tena na tena na vyombo vya habari katika majuma ya hivi karibuni.
 
Mbinu za PLO na makundi ya magaidi wanayohusiana nao zinaonekana kushabihiana katika kila mipango ya kina kama ile iliyofanywa na Waedomu. Hii huenda ikawa inafanana na chuki ya ndani ya Esau na uzao wake yaani Waedomu. Huenda ikawa si kwa bahati mbaya kwamba chuki kali ya Esau na uzao wake, Waedomu, imekolea kati ya tabia za Wapalestina.
 
Katika Sura ya 38 na 39 ya kitabu cha Ezekieli tunawaona Wayahudi wakiwa wamerudi katika ardhi yao katika siku za mwisho. Wakiwa wamejikusanya kutoka mataifa yote. Sura ya 35, 36 na 37 ya Ezekieli inahusiana na matukio yanayofananishwa na kukusanyika.
 

Tena neno la Bwana likanijia kusema, mwanadamu kaza uso wako juu ya mlima Seiri, ukatabiri juu yake¼miji yako nitaiharibu, nawe utakuwa ukiwa, nawe utajua ya kuwa mimi ndimi BWANA. Kwa kuwa umekuwa na uadui usikoma, nawe umewatoa wana wa Israeli wapigwe kwa nguvu za upanga wakati wa msiba wao, wakati wa mwisho wa uovu.
                                                     -Ezekiel 35:1-2, 4-5
 
Unabii mwingine wa kuvutia ambao unahusianishwa na madai ya siku hizi ya mamlaka ya Wapalestina kuhusiana na Hekalu Mlima na ardhi ya Israeli  ni Ezekieli 36:2,5:
 
Bwana Mungu asema hivi: Kwasababu adui amesema juu yenu, Aha! Na mahali pa juu pa zamani pamekuwa petu tupamiliki;¼basi Bwana MUNGU asema hivi; Hakika kwa moto wa wivu wangu nimenena juu ya mabaki ya mataifa na juu ya Edomu yote; waliojiandikia nchi yangu kuwa milki yao, kwa furaha ya mioyo yao yote, kwa jeuri ya roho zao, ili waitupe nje kuwa mawindo.
 
Ni ushindani wa mamlaka ya Palestina, kama ilivyofundishwa katika shule za Kiislamu za Palestina, kwamba hapajawahi kuwepo Hekalu la Wayahudi katika mlima Moria, na kwamba ardhi ya Israeli ni mali ya Wapalestina. Hata hivyo kama tunaiamini Biblia na Mungu wa Biblia, basi ni lazima pia tuamini neno la Mungu, kwamba aliwapa ardhi hii uzao wa Abraham kupitia Isaka na Yakobo.
 
Waedomu walikuwa na ardhi yao na wakaiacha, na kwamba hadi leo bado kuna nafasi tele kwa ajili yao katika ardhi hiyo walioiacha kama watataka kurudi. Hata Jiji la Petra la ukubwa wa maili za mraba thelathini na mbili lina Wabedui wachache wanaoishi pale. Labda Yesu Kristo atawaweka tena kwenye nchi yao atakaporudi.
 
Uadui/uhasama wa vizazi vya Esau kwa Waisraeli haudhuru tu Waisraeli. Sumu hii ya miaka elfu nne imekuwa ikitapakaa Marekani yote kwa vile Marekani inashutumiwa kwa kuwepo taifa la Israeli.

 
Mwanzo 25.
29 Yakobo akapika chakula cha dengu. Esau akaja kutoka nyikani, naye alikuwa amechoka sana.
30 Esau akamwambia Yakobo, tafadhali unipe hicho chakula chekundu nile, kwakuwa ninazimia mimi. Kwa hiyo walimwita jina lake Edomu.
31Yakobo akamwambia kwanza uniuzie leo haki yako ya mzaliwa wa kwanza.
 32 Esau akasema; Tazama mimi ni kifa itanifaa nini       haki hii ya uzazi?
33 Yakobo akamwambia, uniapie kwanza. Naye akamwapia, akamwuzia Yakobo haki yake ya mzaliwa wa kwanza.
      
 
 

Share this :

Related Posts

0 Comments