[wanabidii] TAMKO LA KIKUNDI KAZI CHA SERIKALI ZA MITAA CHA POLICY FORUM KUHUSU UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2014

Friday, July 18, 2014
TAMKO LA KIKUNDI KAZI CHA SERIKALI ZA MITAA CHA POLICY FORUM KUHUSU UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2014

Sisi wajumbe wa Kikundi Kazi cha Serikali za Mitaa cha Policy Forum, tunaowakilisha zaidi ya Asasi  70 za Kiraia tuliounganisha nguvu zetu  ili kuchangia katika kuifanya michakato ya sera ngazi ya serikali za mitaa kuwa yenye uwazi zaidi, ya kidemokrasia, iliyo shirikishi na yenye uwajibikaji, tunapenda kutoa  mchango wetu katika mchakato huu  muhimu wa uchaguzi wa serikali za mitaa wa 2014.  

Tunatambua umuhimu wa serikali za mitaa, ambazo zinalenga kupeleka madaraka kwa jamii au kusogeza madaraka ya kufanya maamuzi kwa wananchi ili kuboresha na kuimarisha utoaji wa huduma kulingana na matakwa ya wananchi.  Tunatambua pia, kwamba mchakato wa uchaguzi wa serikali za mitaa unategemea mchakato wa katiba mpya ambao umepoteza ratiba yake ya awali ambapo katiba mpya ingezinduliwa tarehe 26 Aprili 2014 na kwa sasa umefika njiapanda na hivyo haijulikani wapi tunaelekea katika uandikaji wa katiba mpya.

Kutokana na ukweli kwamba uchaguzi wa serikali za mitaa ulitakiwa kufanyika kati ya Septemba na Oktoba 2014 na kutokana na matamko mbalimbali yaliyokwishatolewa na viongozi pamoja na wachambuzi wa masuala ya kisiasa pamoja na wadau mbalimbali na sisi kama wadau katika uongozi wa serikali za mitaa tunajiuliza maswali mengi juu ya hatima ya uchaguzi wa serikali za mitaa kwa mwaka huu.

Tungependa kujua kama wadau wakuu ni lini Uchaguzi wa Serikali za mitaa utafanyika? Kama tunavyofahamu kipindi kama hiki utaratibu umekuwa kwamba kanuni za uchaguzi huwa zinakuwa zimeshaandaliwa na kutolewa ambazo kazi yake kubwa ni kutoa mwongozo na taratibu wa jinsi serikali za mitaa zitakavyoendeshwa hivyo tungependa kujua kama kanuni za uchaguzi zimeshaandaliwa? Na kama zimeshaandaliwa zimeandaliwa na chombo gani? Na ushiriki wa wadau ulikuwaje? 

Sisi tunataka kusema kuwa tumeona mkutano wa vyama vya siasa na TAMISEMI uliofanyika Morogoro hivi karibuni ambao tumesoma kupitia vyombo vya habari ulikuwa wa kuandaa kanuni za uchaguzi wa serikali na hapa tunataka kusema kuwa kama wadau toka mashirika yasiyo ya kiserikali hatujashiriki wala kushirikishwa katika mchakato wa kuandaa kanuni.

Sisi kama kikundi kazi cha mtandao ambao unajihusisha na masuala ya serikali za mitaa nchini Tanzania tunaungana na Rais Daktari Jakaya Mrisho Khalfan Kikwete kuwa Tanzania kama nchi kwa sasa iko kwenye mtikisiko mkubwa kuhusiana na mchakato wa kuandika katiba mpya hivyo haiwezi kuhimili pamoja na mchakato wa katiba na chaguzi mbili kuu, hivyo basi tunapendekeza uchaguzi wa serikali za mitaa ufanyike pamoja na Uchaguzi Mkuu Oktoba 2015 kama ilivyo kwa Kenya na Zimbabwe.

Kwa  kutambua kuwa TAMISEMI sio chombo mahususi cha kuendesha chaguzi hapa nchini,  pia tunapendekeza uchaguzi wa serikali za mitaa  usimamiwe na kuendeshwa na Tume Huru ya Uchaguzi na kwa sasa tupate nafasi ya kubadilisha sheria za uchaguzi na kufanya maandalizi mengine ili tuwe na chaguzi huru na zenye ufanisi mkubwa.

Taarifa kwa waandishi:
Kwa habari zaidi tafadhali wasiliana na wafuatao:
Mwenyekiti Kikundi Kazi cha Serikali za Mitaa : Hebron Mwakagenda:  theleadership2000@yahoo.com,0713612681
Alex Ruchyahinduru   +255 757716333, policy2@policyforum.or.tz


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments