TAARIFA FUPI KUHUSU MKUTANO WA 22 WA KAMATI YA MISITU DUNIANI-COFO ULIOFANYIKA MAKAO MAKUU YA FAO MJINI ROME, ITALIA: 24-27 JUNI 2014
Mkutano wa ishirini na mbili (22) wa Kamati ya Misitu (Committee on Forestry-COFO) ya Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) umefanyika mjini Rome, Italia kwenye makao makuu ya FAO. Hii ni kawaida kwa mikutano ya nchi wanachama wa FAO kufanyikia mjini Rome, Italia. Kamati ya Misitu (COFO) inawezekana ikaeleweka kwa wengi kama ni kamati ndogo ukweli ni kwamba tunaposema Kamati ya misitu duniani tunamaanisha ni nchi wanachama wa FAO ambazo hukutana na kwa pamoja kuweza kuzungumza na kushauriana juu ya masuala mbalimbali yanayohusu sekta za misitu, wanyamapori na kwa upande fulani nyanda za malisho ya mifugo hasa kwa maeneo kame. Kwa mara ya kwanza kikao cha Kamati ya Misitu duniani kilifanyika mwaka 1977. Kikao cha 22 COFO kimefanyika Rome, Italia tarehe 24 hadi 27 Juni 2014 na kuhudhuriwa na nchi wanachama 125 na mashirika ya kimataifa yapatayo 10 yameshiriki na kuweza kutoa michango yao pale wawakilishi wa mashirika hayo walipoona ni muhimu kufana hivyo. Mkutano wa Kamati uliambatana na shughuli mbalimbali za Juma la Misitu Duniani (World Forest Week) ikiwemo na mijadala tofauti na ile ya Mkutano wa COFO hasa iliyoongozwa na mashirika ya kimataifa yanayojishughulisha na masuala mbalimbali ya misitu pamoja na wanyamapori ikiwepo utafiti, mafunzo, masuala ya kijamii na uhifadhi wa mazingira.
Mkutano ulifunguliwa rasimi tarehe 23 Juni 2014 (siku ya Jumatatu) kuanzia saa nne asubuhi kwanza, kwa Mwenyekiti wa Mkutano wa Kamati wa 21: Dkt. Felician Kilahama kutoka Tanzania alipotimiza wajibu wake kwa kuwakaribisha rasimu kwenye mkutano wajumbe wote wa mkutano wakiwemo Mawaziri, Manaibu Mawaziri, Makatibu Wakuu, Wageni Mashuhuri na wawakilishi wa nchi na wale wa mashirika ya kimataifa. Pili, Mwenyekiti wa COFO 21 Dr. Kilahama aliweza kutamka rasimi kuwa sasa Mkutano wa nne wa Juma la Misitu Duniani (World Forest Week) na Mkutano wa 22 wa Kamati ya Misitu (COFO) sasa vimefunguliwa rasimi. Baada ya hapo mwenyekiti wa COFO-21 Dkt. Kilahama, aliendesha shughuli za ufunguzi kwa kuwakaribisha wageni waalikwa sita kutoka sehemu mbalimbali duniani ili waweze kutoa nasaha zao. Awali ya yote Dkt. Kilahama alimkaribisha Mhe. Jose Graziano da Silva, Mkurugenzi Mkuu, FAO aweze kusema machache na kuweza kuzinduliwa rasimi Balozi Mteule wa FAO kwa masuala ya Mazingira na misitu mwana wa Mfalme: H.R.H Prince Laurent kutoka Belgium. Katika hotuba yake H.R.H Prince Laurent aliishukuru FAO kwa kumpa heshima hiyo ya kuwa Balozi mteule katika Mazingira na misitu na akaahidi kuwa atatoa mchango wake ipasavyo. Mwenyekiti wa COFO-21 Dr. Felician Kilahama, pia alimpongeza Mhe. Prince Laurent wa Belgium kwa kazi hiyo kwa faida ya dunia nzima. Vilevile, Dr. Kilahama alimwomba atakapoonza kufanya kazi atoe kipaumbele kwa Bara la Africa maana ni sehemu ambayo ina hali ngumu sana kimazingira ukilinganisha na mabara mengine. Aidha Dr. Kilahama alitumia fursa yake ya uwenyekiti kuwaomba na kuwakaribisha wajumbe wa mkutano wa 22 wa COFO kuiona Tanzania kama ni sehemu muhimu ya kutembelea kwa sababu kuna vivutio vingi ikiwemo mlima mrefu kuliko yote barani Africa-Mlima Kilimanjaro (Come to Tanzania the land of Kilimanjaro).
Wageni wengine walioweza kuongea wakati wa ufunguzi wakiongozwa na Dr. Kilahama ni pamoja na:
Mhe. Rosine Amane Baiwong Djibergui, Waziri wa Kilimo na Mazingira nchini Chado ambaye pia ni Rais wa COMIFAC;
Mhe. Shin Won-Sop, Waziri wa Misitu, Jamhuri ya Korea;
Mhe. Thomas Gass, Naibu Katibu Mkuu, Umoja wa Mataifa anayeshughulikia, Masuala ya Kiuchumi na Kijamii,
Mhe. Piet Vanthemsche, Rais wa AGRICORD, Ulaya na mwisho ni
Mhe. Jose Graziano da Silva, Mkurugenzi Mkuu FAO.
Baada ya wageni hao waalikwa kutoa hotuba zao Mwenyekiti Dr. Kilahama alifunga shughuli za ufunguzi na hatimaye kuanzisha rasimi Mkutano wa 22 wa Kamati ya Misitu Duniani uliosadikiwa kuhudhuriwa na wajumbe Zaidi wa 600 kutoka nchi 120 na mashirika ya kimataifa 10. Tanzania katika mkutano huo iliwakilishwa na wajumbe sita alioongozwa na Mhe. Balozi Msekela aliyefuatana na Afisa kutoka Ubalozini Bwana Ayoub. Kutoka Dar-Es-Salaam Wizara Ya Maliasili Na Utalii ni Bwana Zawadi Mbwambo aliyewakilisha Wakala wa Huduma za Misitu (TFS) na Bwana Lyimo kutoka Wizarani. Pamoja na hao walihudhuria Prof. Yonica Ngaga, Mkuu wa Kitivo Cha Misitu na Uhifadhi Asilia na Dr. Laurence Mbwambo, Kaimu Mkurugenzi Mkuu, Taasisi ya Utafiti wa Misitu (TAFORI) yenye makao makuu katika Manispaa ya Morogoro.
Baada ya kufungua rasimu mkutano wa 22 wa COFO kwanza, Mwenyekiti aliwaomba wajumbe wapitishe rasimu ya Agenda za mkutano kitu ambacho walikifanya bila ya kusita. Pili, aliendesha Agenda iliyohusu uchaguzi kwa kuwathibisha Wenyeviti sita wa Makundi au mabara ili wawe Makamu wa Mwenyekiti wa COFO-22 ambayo kipindi chao cha uongozi kitaisha wakati wa mkutano kwa 23 wa COFO utakaofanyika 2016 mjini Rome. Baada ya uthibitisho kufanyika ikawadia zamu ya kumchagua Mwenyekiti mpya ambapo wajumbe kwa pamoja Walimchagua aliyekuwa Rais wa Gayana, America ya Kusini (kwa kipindi cha miaka 12 na aliwahi kuwaa waziri wa Fedha wa nchi hiyo kwa miaka sita) Mhe. Dr. Bharrat Jagdeo, kuwa Mwenyekiti wa COFO 22. Kwa tendo hilo hapo Mwenyekiti wa COFO 21 Dr. Felician Kilahama wa Tanzania alihitimisha uongozi wake katika chombo hicho muhimu cha kimataifa kwa niaba ya Bara la Africa.
Pichani ni sehemu tu wa baadhi wa Wajumbe Zaidi ya 600 waliohudhuria Mkutano 22 wa COFO na mbele yao ni Viongozi wa FAO (Mkurugenzi Mkuu wa FAO Mr Graziano da Silva wakiwa kulia kwa Dr. Felician Kilahama (Mwenyekiti wa COFO-21) na kushoto kwake ni Mkurugenzi Mkuu Msaidizi (Bwana Edward Rojas Briales ambaye anasimamia Idara ya Misitu ndani ya FAO). Kulia kwa Mhe. Jose Graziano da Silva ni HRH Prince Laurent wa Belgium na Mana ni Waziri wa Mazingira na Misitu na pia Rais wa COMIFAC kutoka Chad Mhe. Rosine Amane Baiwong Djibergui
Baada ya kumabidhi uongozi Mwenyekiti wa COFO-22; Dr. Kilahama aliwashukuru wajumbe kwa heshima waliyoipa Africa na kwa ushirikiano mzuri alioupata kutoka kwao wakati wa mikutano kama hii na pia alipotembelea America ya Kusini na Mashariki ya kati (Near East) na kuhudhuria mikutano yao iliyofanyika katika majiji ya Geargetown, Guyana na Amman. Jordan sawia. Wajumbe pia walimpogeza sana Dr. Kilahama kwa kuiongoza COFO vizuri sana na kwa hekima kubwa kitu ambacho kimeteta mshikamano mzuri na ni kitu ambacho wengi hawakukitarajia kuwa angeweza kufanya hivyo. Mkurugenzi Mkuu Mdaidizi ambaye ndiye mkuu wa Idara ya Misitu FAO: Bwana Edwardo Rojas Briales, wakati akitoa shukrani zake kwa Dr. Kilahama alisema FAO ilimpata Mwenyekiti wa COFO 21 lakini mwanzoni walikuwa na wasiwasi kama ageweza. Lakini wakiwa katikati ya mkutano wa COFO 21 uliofanyika tarehe 24-28 September 2012 jijini Rome makao makuu ya FAO nay yeye akiuongoza mkutano huo, waligundua kuwa Mwenyekiti anacho kipaji cha kuweza kupambana na hali ngumu na hatimaye kuweza kuwaweka wajumbe katika hali ya kuelewana. Aliendesha mkutano na mikutano ya Kamati ya Uongozi kama mwanadiplomasia wa hali ya juu. Aliongeza kuwa FAO inajivunia sana uongozi wa Dr. Kilahama maana hata vikao vitatu vya Kamati ya Uongozi wa (COFO-Steering Committee) vilivyofanyika kwa nyakati tofauti kati ya 2012 na 2014 aliviongoza kwa umakini mkubwa na kuweza kumalizika kwa muda uliopangwa. Hii ilitushangaza sana alisema Bwana Eduardo Briales na kumkabidhi zawadi ya pekee akimshukuru kwa kazi nzuri aliyoifanya kwa niaba ya bara la Africa na nchi ya Tanzania. Bwana Edwardo Briales aliongeza kuwa kwa heshima ya Dr. Kilahama, imeonekana ni vyema Mkutano wa pili wa Kama ya Uongozi wa COFO ufanyikie nchini Tanzania kwa tarehe zitakazoafikiwa hapo baadaye. Wakjumbe wa Mkutano pia walikubaliana na maneno ya Edwardo Briales juu ya Dr. Kilahama na pia walimpongeza sana kwa kazi nzuri aliyoifanya. Hata hiyo Dr. Kilahama hakusita kumshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa kusema kuwa haya yote ni mapenzi yake Mungu na kama siyo yeye Mwenyezi Mungu kumtia nguvu, kumwongoza ipasavyo na hekima asingeweza kitu hivyo Sifa na Utukufu ni wake Mungu aliyemweza wa yote sisi ni watumishi tu.
Institut d'études de sécurité - SA
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments