Leo hii ukiajiriwa Qatar hata kama ni raia wa nchi nyingine wakati wa kusaini mkataba wa ajira lazima usaini mkataba wa nyumba na mkopo wa gari kwani wanaamini huwezi kufanyakazi sawasawa kama hauna usafiri na nyumba. Qatar haina mafuta gesi wala dhahabu wanawezaje? Na sidhani kama wana kiwanda cha saruji hata kimoja.
Leo hii nyumba na gari ndo vyanzo vya kodi sawa na sigara na pombe. Kodi katika ununuzi wa nyumba ni zaidi ya gharama za ujenzi? Kodi katika ununuzi wa gari ni zaidi ya bei ya kununulia gari. Unanunua gari tena mtumba japani kodi inazidi bei ya kununulia! Wakati ni hitaji la msingi kukuwezesha kufika kazini mapema.
Makazi yaliyojengwa na mkoloni kule mwanza kwa ajili ya watu wa hali ya chini yamevunjwa na kujengwa supamarket ya matajiri, ujamaa hakuna tena.
Kambi za genge saba hakuna tena tunajenga mabondeni milimani kando mwa barabara bora shuka lisitiri mwili.
Mama mmoja mwalimu wa shule ya msingi aliniambia bado miaka miwili astaafu ndo kwanza nyumba iko kwenye renta, Halafu akienda mjini anaona mahotel ya kifahari ya nssf na ppf, mtawasingizia ukawa majanga mnayachuma wenyewe.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments