[wanabidii] MAISHA BINAFSI YASIYO KUATHIRI

Thursday, July 17, 2014

MAISHA BINAFSI YASIYO KUATHIRI

Na Goodluckies Good.

Husika kichwa cha habari hapo juu, niseme tu kuwa tunaweza kuwa na umri sawa, elimu sawa, dini sawa, kabila sawa, kipindi kifupi au kirefu tumeishi pamoja, tumeshirikiana ktk matatizo na furaha, lakini kamwe tabia za ndani, mawazo, uwezo wa kuona na kupambanua mambo, utayari wa kukubaliana au kupingana na jambo au mambo fulani, na mambo mengi sana, hatuwezi kuwa sawa kamwe.

Kwa mimi binafsi najihesabia ni mtu huru, nisiyejisikia vizuri, au nisiyependa kuingiliwa uhuru wangu. Aidha wa kutenda ama kusema, kwani siku zote za maisha yangu hujutia na hupata masumbuko ya moyo ninapomfanyia mtu jambo ambalo lingetokea kwangu lingeniathiri.
Lakini madhara ni mengi, kauli ina madhara makubwa sana kuliko matumizi ya nguvu, endapo nikitoa kauli yenye kumkwaza mtu, kumkatisha mtu tamaa, kumtishia mtu, kumzuia mtu, kumtukana mtu, au kuathiri uhuru wake kwa namna yoyote ile, atavyojisikia ndivyo nitavyojisikia mimi nikifanyiwa hivyo, hasa katika nyakati hizi ngumu. Hakuna aliye na mamlaka juu ya ubinadamu au utu wa kiumbe kingine kinachoitwa binadamu, wote tumekuja duniani kwa njia moja, na tutaondoka kwa njia moja, kwahiyo kila mtu kaja afanye yake kisha aondoke, iweje nifanye kama wewe? Iwezekaneje nifikirie kama wewe? Iwezekaneje niishi kama wewe? Hii naisema tu, kinywa chenye maneno ys busara kikifumbwa ni sawa na pete ya dhahabu kwenye pua ya nguruwe.

Wengi tunaendeshwa na hofu ya maisha na kifo, hivyo kujikuta kufanya mambo au kuishi maisha ya wengine kwasababu ya hofu hiyo, najitahidi kuikataa hiyo ili niwe mimi, kwani maisha ni haya na kifo ni sehemu ya maisha, kwahiyo tusiingiliane kimtazamo kama tunapishana, kutoa au kupokea ushauri usiofaa pia ni sawa na kujilisha upepo. Nawashukuru watu wote tunaoenda sawa aidha kwa kukubaliana au kwa kupingana, ila napenda kuwashauri kila mmoja alinde na aheshimu uhuru wake na wa mwenzie bila hofu yoyote ile wala vikwazo.

Asalaam.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments