[wanabidii] LUKUVI NA SIRI YA DAWA ZA KULEVYA

Wednesday, July 02, 2014

Yapata miezi kumi 10 sasa tangu Bwana Lukuvi aweke bayana kuwa ofisi ya Rais tayari inamajina ya vinara wa madawa ya kulevya nchini

" Orodha hii ya majina tunayo muda mrefu, na kwa orodha hii tukiwataja wengi wenu hamtabaki salama. Kwa hiyo mwenye taarifa atuletee majina na ushahidi na tutamtaja na yeye" 
27/ 08/2013

Kwa kauli hii maswali yafuatayo yanaweza kutuongoza kujua mambo ya msingi juu ya viongozi wanaotokana na CCM

1. Je kuna nia ya dhati kutaka kukomesha biashara hii haramu inayopelekea taifa kupoteza nguvu kazi kwa kiasi kikubwa??

2. Je kama serikali inajua wahusika ni kwa nini imeshindwa kuwataja tu kwa majina na mitandao yao achilia mbali kuwapeleka mahakamani ni kweli kuwa kuna ukweli kuwa serikali yetu ni dhaifu kiasi cha kushindwa kuthobutu kutaja watu binafsi??

3. Serikali kupitia Waziri wake Lukuvi inaogopa nini kuwataja hata hao wabunge aliosema hawatabaki salama? Je wao wanahati miliki ya kufanya maovu kiasi cha serikali kuhofia usalama wao wa kiuongozi na madaraka kwa ujumla??

4. Je nini maana ya uzalendo? Ni kukesha kushinda kutwa nzima kuhangaika na UKAWA na kuacha mambo ya msingi kama haya hayana majibu na utatuzi wake

5. Serikali inawadharau wananchi kwani imekuwa ikiwahadaa majukwaani juu ya uadilifu na maadili ya utumishi wa umma.

6. Vipi sasa ile taasisi tanzu iliyo chini ya Ofisi ya Rais na maanisha TAKUKURU imeshindwa hata kudhani kuwa rushwa ni dhana pana ikaanza kumchunguza Lukuvi na watendaji wake juu ya uwezekano wa kuwa wamehongwa na hao mapapa ili wawalinde???

Kama serikali inawaogopa hao wauza unga (madawa ya kulevya) naishauri ifanye mambo matatu

(a). Ijivue lawama iwapatie vyama vya siasa majina hayo hasa vyama vikubwa kama CHADEMA, NCCR- Mageuzi na hata CCM inawatu kwa Nape na kinana waweza wakaisaidia kuwataja.

(b). Serikali kupitia Waziri Lukuvi wajipange vizuri waamke siku moja usiku wa Manane wayabandike hayo majina hadharani kwenye stendi za mabasi, viwanja vya ndege, masoko, maduka makubwamakubwa kama Mlimani City n.k pia sambamba na hilo wawataje watu hao kwenye vitabu vya kiada na ziada mashuleni ngazi zote

(C) Hao jamaa waitwe ikulu wapate chakula cha jioni na ofisi ya ikulu halafu wawauwe kwa kuwapatia vyakula vyenye sumu wafe kabisa.

Lengo kuu la makala hii ni kuikumbusha serikali wajibu wake na si kuichochea hasira serikali initafute na kunipoteza ka yule bwana wa mwaka jana mwaka juzi na hata mwaka huu.

Mungu ibariki Tanzania na wananchi wake.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments