[wanabidii] Elimu isiyo sahihi kuhusu kondomu yachangia maambukizi mapya ya VVU

Saturday, July 26, 2014
Na Mwandishi wetu

Tafiti zimebaini kwamba Vijana hawatumii Kondomu na hutoa sababu nyingi ikiwa ni pamoja na kutopata ladha wakati wa tendo la ndoa na kwamba inapunguza nguvu na visingizio vingine vingi vinavyopelekea kuashiria hatari ya maambukizi.

Hayo yameelezwa na Afisa Mradi wa Elimu ya Afya na VVU/UKIMWI kutoka UNESCO, Bw. Herman Mathias wakati akizungumza na washauri wa Vikundi vya Vijana wasikilizaji juu ya masuala muhimu kuhusiana na kuzuia maambukizi ya VVU na Afya ya Uzazi kwa Vijana wenye umri kati ya miaka 15-24 katika warsha ya kuwajengea uwezo washiriki hao katika matumizi ya mwongozo wa 
ufuatiliaji wa vipindi kwa wasikilizaji walengwa wa Mradi wa SHUGA Redio.

"Asilimia 40 ya Wasichana na Asilimia 47 ya Wavulana ndio wenye ufahamu wa kina juu ya maambukizi ya VVU huku asilimia kubwa wakiwa hawana elimu ya kutosha na hawajui afya zao kwa kuwa hawana utamaduni wa kupima VVU ", amesema Bw. Mathias.


Katika warsha hiyo ya siku mbili inayoendeshwa na UNESCO kwa kushirikiana na UNICEF katika kituo cha Redio cha Nuru FM Iringa, Bw. Mathias amesema kuna umuhimu mkubwa wa kutoa elimu sahihi kwa Vijana ya kujikinga na maambukizi ya VVU na Mimba kutokana na uelewa mdogo wa Vijana katika matumizi sahihi ya Kondomu.

Wakichangia mada kuhusu masuala muhimu yanayowahusu vijana katika maambukizi ya VVU vijana wamesikitishwa na mimba za utotoni kwa wasichana zinazochangia vifo vya Mama na Watoto na wasichana kuacha masomo.

Washiriki wa warsha hiyo wametaka hatua za haraka zichukuliwe kuhakikisha kuwa sheria za mtoto zinazoruhusu mtoto wa kike kuolewa katika umri mdogo zinafanyiwa marekebisho ya haraka kulinda haki ya mtoto wa kike..

Wakijadili mada hiyo washiriki wamesema mila na tamaduni pia zinachangia kwa kiasi kikubwa kumkandamiza mtoto wa kike katika masuala mbalimbali ya maendeleo yake.

Wakitoa mifano ya baadhi ya mila zilizowafanya wapaze sauti kuhusu mabadiliko ya sheria za mtoto ni ile sheria ya ndoa na mila inayoruhusu mtoto wa kike kuolewa akiwa na umri wa miaka 14 kwa ridhaa ya wazazi. Umri huo unakinzana na haki za mtoto kufurahia maisha yake na kupata elimu.

Mifano mingine ya kitamaduni ni pale mwanamume anapochumbia mimba wakati akijua wazi mtoto ana haki zake za msingi za kuishi.

Wamezitaja pia asasi za dini kutoa elimu kwa vijana ili kusaidia hali iliyojitokeza ya wazazi kutokuwa na muda na watoto wao kuwaelimisha kuhusu mabadiliko ya miili na afya zao.

Akitoa mada kuhusu mbinu mbalimbali za kuwezesha majadiliano katika vikundi vya wasikilizaji, Meneja Mawasiliano kutoka Pangani FM, Bw. Abdul Mfuruki amewataka wawezeshaji kutotumia nafasi walizonazo ili kuendesha mjadala wenye tija.

Amesema washauri wa vikundi hawana budi kuweka mizania kutumia busara, kusoma mazingira na kutoingiza imani au itikadi itakayopelekea kuharibu mjadala unaoendeshwa wa kufuatilia vipindi vya SHUGA Redio, kuwa wavumilivu, kusoma na kuheshimu mawazo ya wengine na kutofungamana na upande wowote ili kumweleza mshiriki wa majadiliano kufunguka zaidi.

Bw. Mfuruki amesema vijana wa vikundi vya wasikilizaji kuwaza mambo mengi ni vyema kuwasikiliza kwa uvumilivu, kupata ushauri wa wengi kwa lengo la kufanya maamuzi sahihi bila kulazimishana na vile vile kuwa wabunifu kwa kutumia mbinu mbadala ili kupata habari iliyojificha.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments