[wanabidii] Wakili Yasinter Rwechungura kortini kwa kumjeruhi binti msaidizi wa ndani

Thursday, June 26, 2014
Wakili wa kujitegemea, Yasinter Rwechungura (44) amefikishwa Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni kwa mashitaka ya kujeruhi mfanyakazi wake wa ndani. 
Rwechungura ambaye amenyimwa dhamana kwa kile kilichoelezwa ni kwa ajili ya usalama wake kutokana na wananchi wa eneo analoishi kuwa na hasira kwa kitendo anachodaiwa kufanya, alifikishwa mahakamani juzi.

Alisomewa mashitaka na Wakili wa Serikali, Mohamed Salum mbele ya Hakimu Mkazi Suleiman Mzava.

Salum alidai Juni 11, mwaka huu, eneo la Boko Njia Panda, 
Yasinter alimjeruhi Marina Mathayo kwa kumpiga na waya wa kompyuta sehemu mbalimbali za mwili wake na kumpiga kichwani kwa kutumia jagi la kusagia matunda jambo lililomsababishia maumivu.

Mshitakiwa alikana kutenda kosa hilo. Upande wa mashitaka ulidai upepelezi wa kesi hiyo haujakamilika. Mahakama iliombwa izuie dhamana ya mshitakiwa kwa muda kutokana na taarifa walizopata kutoka kwa Mkuu wa Upelelezi wa Kanda ya Kinondoni kwamba hali ya majeruhi si nzuri na pia wananchi wana hasira naye. 

Kesi iliahirishwa hadi Julai Mosi, mwaka huu itakapotajwa tena.

--via HabariLeo

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments