[wanabidii] UTAFITI WA MAFUTA NA GESI ASILIA KATIKA MAENEO YA MOROGORO NA KILIMANJARO

Tuesday, June 24, 2014
TAARIFA KWA UMMA 
UTAFITI WA MAFUTA NA GESI ASILIA KATIKA MAENEO YA MOROGORO 
NA KILIMANJARO 
 
Katika toleo Na. 1734 la gazeti la Jambo Leo la tarehe 10 Juni, 2014 katika 
ukurasa wa tatu iliandikwa taarifa iliyokuwa na kichwa cha habari 
"Utafiti wa gesi kuinufaisha Morogoro, Kilimanjaro". Taarifa hiyo ilieleza kuwa 
wakaazi wa mikoa tajwa watanufaika na ugunduzi wa mafuta na gesi uliofanywa 
na Kampuni ya Swala katika maeneo hayo. 
 
Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) linapenda kuwafahamisha 
wananchi kuwa taarifa ya kwamba Kampuni ya Swala imegundua gesi na mafuta 
katika maeneo ya Morogoro na Kilimanjaro sio sahihi. Ugunduzi wa mafuta 
hufanyika tu baada ya kuchimba kisima cha utafiti na hatimaye mafuta au gesi 
iweze kutoka yenyewe kutoka ardhini. Hatua ya kuchimba kisima cha utafutaji 
hutokana na tafiti mbali mbali za awali za mitetemo ya ardhi na kubaini kama 
maeneo hayo yana uwezekano wa kuwa na mafuta au gesi ama la. Hata kama 
eneo linaonesha dalili nzuri za awali ni lazima sehemu hiyo ichimbwe na matokeo 
yake ni kuwa na ugunduzi au la. Vilevile ugunduzi huo lazima uonyeshe kutoa 
kiasi cha rasilimali ambacho kinaweza kuzalishwa kibiashara (economically 
viable). 
 
Kazi zilizofanyika mpaka sasa na Kampuni ya Swala katika maeneo ya Morogoro 
– Kilosa na Pangani - Kilimanjaro ni utafiti wa awali wa kukusanya takwimu za 
mitetemo na kubaini kama maeneo hayo yana kina (thickness) cha kutosha cha 
miamba tabaka ambayo utafiti wa mafuta na gesi unaweza kufanyika. Hivyo 
utafiti wa kina unaendelea ili kubaini kama kuna miamba mashapo (prospects) ya 
kutosha kwa ajili ya kuchimba kisima cha utafiti. Uchimbaji wa kisima hicho 
unaweza kutoa mafuta au/na gesi au maji matupu. Hatua ya uchimbaji visima 

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments