[wanabidii] Taarifa ya Ikulu ya JK kuhusu Bomu la Zanzibar Ijumaa jioni

Sunday, June 15, 2014
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia salamu za pole Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein kufuatia kuuawa kwa mtu mmoja na wengine sita kujeruhiwa akiwemo mhubiri wa amani ajulikanaye kama Sheikh Ahmed Haidari Jabir wa Zanzibar, kutokana na kurushwa kwa Bomu katika shughuli ya kidini iliyokuwa ikifanyika katika eneo la Darajani tarehe 13 Juni,2014, mjini Unguja.

'Hicho ni kitendo cha kulaaniwa kwa nguvu zote na watu wote wapenda amani Bara na Visiwani, ni kitendo cha woga na kisicho na ustaarabu na wala hakikubaliki katika dunia ya sasa' Rais amesema na kuongeza kuwa; 'Hiki ni kitendo kilichofanywa na watu waoga, wasio na ustaarabu wa aina yeyote ile'.

Rais amekemea na kuwataka watu kuwa wastaarabu, wavumilivu na kuheshimu imani na mitizamo ya watu wengine hata kama hawakubaliani nao.

Rais amesema amesikitishwa zaidi na watu hao wasio na ustaarabu ambao wamefanya kitendo hicho cha kihalifu kwenye shughuli ya kidini ambapo ndipo mahali panapostahili Amani, Uvumilivu na Unyenyekevu zaidi kwa kuwa ni wakati ambapo binadamu anapofanya mawasiliano na muumba wake.

Rais Kikwete amelitaka Jeshi la Polisi kuwasaka na kuwafikisha mbele ya vyombo vya haki wale wote waliohusika katika tukio hilo lisilo la kistaarabu.

Imetolewa na; 
Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
Ikulu-Dodoma
15 Juni, 2014

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments