Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania – TRL unawataarifu abiria wote na wananchi kwa jumla kuwa kutokana na kutetereka kwa daraja la reli kati ya stesheni ya Ruvu na mchepuko wa reli ya Ruvu kwenda Mruazi usiku wa kuamkia leo, umeamua kusitisha kwa muda huduma ya usafiri wa abiria hadi ukarabati wa daraja utakapokamilika.
Tokea asubuhi ya leo Mkurugenzi Mtendaji wa TRL Mhandisi Kipallo Aman Kisamfu na Wahandisi waandamizi na Mafundi ujenzi walifika katika daraja hilo lililopo km 82/5 na kulifanyia tathmini kuwa linahitaji kuimarishwa ili lirejee katika kiwango cha usalama kuruhusu treni za abiria kupita.
Kwa taarifa hii wananchi na wateja wa TRL na wananchi kwa jumla ambao walikuwa wasafiri kwenda bara kwa treni ya leo Juni 10, 2014 wanatakiwa kufika katika stesheni zilizokaribu nao ili warejeshewe nauli zao ili watafute usafiri mbadala.
Aidha Uongozi wa TRL unaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.
Imetolewa na Afisi ya Uhusiano kwa Niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa TRL Mhandisi Kipallo Aman Kisamfu
Dar es Salaam
Juni 10, 2014
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments