Rgrds
Magora
---------- Forwarded message ----------
From: "Magora" <hmagora@yahoo.com>
Date: Jun 21, 2014 12:13 AM
Subject: Fwd: CCM IFAFANUE TAMKO LA LUKUVI DHIDI YA UISLAMU NA MADAI YA KUREJEA WAARABU Z'BAR
To: <magorah15@gmail.com>
Cc: <hmagora@yahoo.com>
-------- Original message --------
Subject: CCM IFAFANUE TAMKO LA LUKUVI DHIDI YA UISLAMU NA MADAI YA KUREJEA WAARABU Z'BAR
From: musa khamis <mizanimedia@yahoo.com>
To: Magora Hassan <hmagora@yahoo.com>
CC:
-- From: "Magora" <hmagora@yahoo.com>
Date: Jun 21, 2014 12:13 AM
Subject: Fwd: CCM IFAFANUE TAMKO LA LUKUVI DHIDI YA UISLAMU NA MADAI YA KUREJEA WAARABU Z'BAR
To: <magorah15@gmail.com>
Cc: <hmagora@yahoo.com>
-------- Original message --------
Subject: CCM IFAFANUE TAMKO LA LUKUVI DHIDI YA UISLAMU NA MADAI YA KUREJEA WAARABU Z'BAR
From: musa khamis <mizanimedia@yahoo.com>
To: Magora Hassan <hmagora@yahoo.com>
CC:
CCM IFAFANUE TAMKO LA LUKUVI DHIDI YA UISLAMU NA MADAI YA KUREJEA WAARABU Z'BAR
Kutoka gazeti la mizani june 20, 2014
Hivi karibuni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Uratibu na Bunge), ndugu William Lukuvi, alitoa kauli nzito Kanisani huko Dodoma ambayo ilikuwa na maudhui kadhaa ikiwemo kuwataka wananchi kupinga serikali tatu zilizopendekezwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba, na akatoa vitisho kwamba vinginevyo nchi itatawaliwa na jeshi kwa kuwa Serikali ya Muungano itashindwa kuwalipa mishahara wanajeshi.
Ndugu Lukuvi alikaririwa akisema hayo mnamo 13 Aprili mwaka huu, katika Kanisa la Methodist, Jimbo la Dodoma alipokuwa mgeni rasmi akimwakilisha Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, mbele ya waumini waliofurika katika ibada ya kumsimika Mchungaji Joseph Bundala kuwa askofu wa Kanisa hilo katika jimbo, na akatoa ombi kwa waumini wa Kanisa kuwa waendelee kuliombea Bunge lifanye uamuzi sahihi wa Serikali mbili.
Mimi binafsi hayanishughulishi matamko ya Ndugu Lukuvi ya kupiga kampeni ya kuwa na Muungano wa Tanganyika na Zanzibar wenye muundo wa Serikali mbili kama ilivyo sasa. Hii ni kwa sababu hata mimi binafsi naunga mkono muungano wa mfumo huo nikiwa na dhana kuwa kuondoa kero za muungano ni jambo la msingi zaidi kuliko kuongeza mzigo wa Serikali nyingi ambazo hazina tija wala hatuna uwezo wa kuziendesha.
Aidha rasimu ya Katiba iliyowasilishwa na Tume ya Jaji Warioba kwa upande wetu Waislamu tunaiona haifai hata pesa mbili, kwa sababu imezingatia udini zaidi kutokana na kutokuwemo ndani yake maoni ya jamii ya Waislamu. Jaji Warioba na wenzake hawakuwa na haki hata kidogo ya kupuuza maoni ya jamii kubwa kama ya Waislamu kwa kiwango kwamba wakaona hayafai hata kujadiliwa. Huo ni udini ulioanikwa katika jua kali la mchana wa kipwa na wala si kazi waliyoteuliwa kuifanya.
Katika ujumbe wa Ijumaa hii, sikusudii kuzungumzia suala la muundo wa Muungano. Nia yangu kutafakari maelezo yaliyohusu Uislamu kama dini yangu, ndani ya hotuba ya Ndugu William Lukuvi katika hotuba yake akiwa ndani ya Kanisa ambako ameupaka matope Uislamu na kuudhalilisha.
Ndugu Lukuvi akiwa ni Waziri katika Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Uratibu na Bunge) ametushitua sana Waislamu hapa nchini pale alipotoa matamko yanayoonyesha uadui iliyo nayo Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania juu ya Waislamu, kwa kiwango kwamba sababu za kutowapa Wazanzibari haki zao ni kwa kuhofia Uislamu ambao Lukuvi anadai ni kitu hatari. Isitoshe Lukuvi ameonyesha chuki kwa Waarabu ambao ni Waomani waliotawala Zanzibar nchi ambayo kwa ni rafiki na ndugu wa kihistoria w Tanzania.
Kwa kuwa Lukuvi ni Waziri anayesimamia sera za Serikali, na ukizingatia ukweli kuwa Serikali hii ni ya chama cha Mapinduzi (CCM), utapata jibu kuwa Sera ya CCM ni kuing'anga'nia Zanzibar kwa kuhofia kuwa, kwa kuwa asilimia 95 ya Wazanzibari ni Waislamu, basi wanaweza kuamua kuunda Serikali ya Kiislamu ambayo Sera za Serikali inaona kuwa hilo ni jambo hatari kwa usalama wa Tanzania Bara.
Kabla ya kuendelea mbele tafadhali msomaji rejea sehemu ya maneno ya Waziri Lukuvi na hapa ninamnukuu:
''Tunataka tuwaache Wazanzibari wajitawale wenyewe na Tanganyika! Wazanzibari kule waliko asilimia 95 ni Waislamu. Tunataka wajitangazie Serikali ya Kiislamu kule? Mnajua madhara yake? Wale waarabu watarudi. Watazalisha siasa kali kule watakuja kutusumbua, mimi najua, kabisa...'' mwisho wa kunukuu.
Sisi kama viongozi wa Taasisi, Waalimu na Masheikh wa dini ya Kiislamu, wajibu wetu wa kwanza mbele ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake (SAW) na mbele ya waumini tunaowaongoza ni kuutetea na kuunusuru Uislamu pale unaposhambuliwa na kusingiziwa na watu kama Ndugu Lukuvi.
Kwa msingi huo haiwezekani hata kidogo, iwe Ndugu William Lukuvi kama alivyo kiongozi mwandamizi Serikalini, awe ametumwa na Serikali, au CCM, au hata kama iwe ni kwa chuki zake kinafsi, au fikra zake tu, atoe tamko la kuudhalilisha na kuutangazia umma kuwa Uislamu ni imani ya kutisha na kuogofya, na kisha sisi tunaojifanya wahubiri na watetezi wa Uislamu tukae kimya. Tukikaa kimya tutakuwa tumeogopa na kuwasaliti Waumini tunaowaongoza. Na kwa wajibu huo tunajibu tuhuma zake kama ifuatayo;
Kwanza ni juu ya tamko lake kuwa Tanganyika ikiiacha Zanzibar, basi kwa kuwa asilimia 95 ya Wazanzibari ni Waislamu wataunda Serikali ya Kiislamu. Kwa tamko lako hili ndugu Lukuvi, umekusudia kuonyesha kuwa ninyi Wakristo mliomo ndani ya Serikali ya Muungano au serikali yenyewe katika vikao vyenu vya siri, hamuupendi Uislamu na kwa chuki hizo mnaishikilia Zanzibar kimabavu kwa hofu kuwa isije ikawa taifa la Kiislamu.
Aidha tamko hilo linadhihirisha ukweli ambao kila mtu anautambua kwamba, misingi ya kuunda muungano haikufuatwa wakati wa kuziunganisha nchi mbili hizi. Mwalimu Nyerere na Sheikh Karume walikubaliana wao wenyewe kuziunganisha nchi zao na kila mmoja kati yao alikuwa na sababu zake binafsi. Hakuna mwenye akili timamu anayeweza kulaumu dhamira yao njema na hasa kutokana na mfumo na nidhamu ya utawala enzi hizo na shakhsiya ya watu wenyewe na imani ya wananchi juu yao kwa wakati huo.
Ndugu Lukuvi anapaswa kufahamu kuwa wakati Sheikh Abeid Amani Karume akifanya Mapinduzi Zanzibar waislamu walikuwa ni wengi na zaidi ya asilimia 95 anazotaja yeye. Kama leo Zanzibar kuna asilimia 95 ya Waislamu, basi hiyo asilimia 5 anayodhani kuwa ni ya Wakristo ni wahamiaji ambao wamehamishiwa Zanzibar kutoka Bara kwa shabaha ya kupandikiza Ukristo Zanzibar na kwa lengo hilo hilo wamekuwa wakinunua ardhi ya kuanza kujenga Makanisa ambayo hayahitajiki, jambo ambalo limekuwa likizusha chuki na kusababisha vitendo vya uchomaji wa Makanisa.
Lakini kubwa kuliko yote tunamuuliza Ndugu Lukuvi kabla ya Muungano wa mwaka 1964, Zanzibar ambayo ilikuwa ikitawaliwa na Sultan Muomani kulikuwa na Serikali ya Kiislamu? Na je Serikali hiyo ilikuwa na madhara gani kwa amani na usalama wa Bara? Na je Mzee Karume alipopindua Serikali ya Sultan aliunda Serikali ya Kiislamu? Je kabla ya Mapinduzi na baada ya Mapinduzi ni jambo gani linalotokana na Uislamu wa wazanzibari limekuwa hatarisho la usalama wa Watanganyika na hususan Wakristo? Tunataka jibu lako, au la Serikali au CCM yenyewe.
Juu ya madai ya Ndugu Lukuvi kuwa sababu ya Tanganyika kuing'ang'ania Zanzibar ni kuwa eti waarabu watarejea na kuzalisha siasa kali, tunamuomba Ndugu Lukuvi afahamu kuwa maneno yake hayo hayana ukweli wowote ule na hayakutegemewa kutamkwa na mtu mzito Serikalini ambaye amepewa dhamana ya kusimamia Sera za Serikali.
Hadi sasa bado tunamuona Lukuvi kama mtu mwenye nia njema ya kutaka kuhakikisha muungano unadumu, lakini mwenye kutumia njia isiyofaa ambayo inajenga chuki baina ya Waislamu na Serikali ambayo yeye ni kiongozi wake.
Ndugu Lukuvi unaweza kutueleza ni madhara gani yatakayotokea kwa Watanganyika iwapo wazanzibari ambao wewe mwenyewe unasema ni Waislamu kwa asilimia 95 wakiamua kujitawala wa mfumo wa Serikali yenye kufuata maadili ya dini yao wenyewe ya Uislamu? Unasema maneno haya kama kiongozi wa Serikali au Mkristo mwenye kuchukia Uislamu? Kama si yote mawili unasimamia wapi wakati unapowatishia wananchi na kuwataka wawe na hisia mbaya juu ya Uislamu?
Sisi hatudhani kama ni busara kwa kiongozi mzito kama wewe kujaribu kuwatia hofu na kuwatisha wananchi kwa kutolea mfano dini ya Kiislamu ambayo unafahamu fika ina wafuasi ambao wako tayari kuipigania dini yao kwa hali na mali? Aidha tunakuomba ufute kabisa maneno yako unayoutuhumu Uislamu kuwa ni ''SIASA KALI''.
Mimi nafahamu wazi kuwa wewe hujui chochote juu ya Uislamu. Na sifa ya mwanadamu kamili ni ujinga, na dawa ya ujinga ni kusoma. Nani aliyekwambia katika Uislamu kuna mafunzo yanaitwa imani ya siasa kali? Panua ufahamu wako kwa kufahamu kuwa hakuna kinachoitwa siasa kali katika Uislamu. Tamko hilo ni neno lililotungwa na viongozi wa Kikristo wa mataifa makubwa kwa nia ya kuzishambulia na kuziangamiza nchi za kiislamu kwa chuki zao na kwa nia kupora utajiri wao.
Kwa faida yako na napenda nikupe darsa la maneno machache ambayo yatakuelimisha na kukuweka katika ufahamu wa nini maana ya Uislamu kama ifuatavyo;
Dini ya Kiislamu ni sheria, kanuni na maadili ya Kiungu ambayo ndani yake kunapatikana mfumo kamili wa maisha ya mwanadamu na viumbe wote. Katika kanuni hizo Mwenyezi Mungu hajawahi kuufanya uhalifu kuwa ni mfumo kamili wa maisha ya viumbe. Bali Mwenyezi Mungu ametutaka tufahamu kuwa uadilifu ndiyo mfumo sahihi na timilifu wa maisha ya viumbe.
Ili maisha ya viumbe yawe ya amani, ni lazima uadilifu uwe ndiyo msingi wa maisha yenyewe, na uadilifu ni utiifu wa kanuni na sheria zilizoletwa na Mwenyezi Mungu kupitia kwa Mitume wake. ukipatikana Uadilifu ndipo amani pia hupatikana. Na hii ni kwa sababu amani ni zao la uadilifu.
Uadilifu si swala linaloweza kunasibishwa na imani fulani, bali ni swala la kimaumbile kwa kuwa ni silika ya kila mwanadamu kupenda uadilifu na kuchukia dhulma. Na ni kwa sababu ya kutaka kusimamisha uadilifu ndiyo maana tunaona mahakama zimewekwa hadi kwenye jamii zisizokuwa na dini ili kila mwenye kudhulumiwa awe na pahala pa kupatia haki yake nia ikiwa kusimamisha haki.
Ndugu Lukuvi, hiyo ndio maana ya Uislamu tuliyojifunza sisi wenyewe Waislamu. Huo Uislamu wa siasa kali unaowatisha nao watu umejifunza wapi? Kutoka kitabu gani cha Kiislamu? Na ni hivyo ndivyo Sera za Serikali ya Jamhuri ya Muungano zinavyoitakidi kuhusu Uislamu? Unadhani Waislamu tungetambua kuwa CCM na Serikali yake vinautazama Uislamu kama adui tungekuwa wapenzi na wanachama wa adui yetu?
KUREJEAA WAARABU Z'BAR
Ndugu Lukuvi kama walivyo wanasiasa wengine wenye chuki, akiwa Kanisani aliwatisha Waumini wa Kikristo kwa kuwaambia kuwa endapo Tanganyika itaicha Zanzibar, basi Waarabu watarudi kuleta siasa kali za kiislamu ambazo madhara yake amedai eti anayajua. Hili nalo si jambo la hakika. Ni propaganda za chuki kwa waarabu lakini msingi wa chuki hii ni kuchukia Uislamu.
Lukuvi anapozungumzia kurejea tena utawala wa Waarabu, anazungumzia Dola ya Usultani wa Omani ambao hivi sasa inaendeshwa na mjukuu wa Wafalme hao ambaye ni Sultan Qaboos bin Said Al Said.
Lakini kwanza nataka Ndugu Lukuvi aelewe kwamba sisi sote tunautaka muungano. Na lazima muungano huu ujengeke katika misingi imara ya maridhiano na sio kama anavyofanya Lukuvi kuweka vitisho vilivyojaa chuki akidhani kufanya hivyo kutasaidia maridhiano. Labda tumsaidie Ndugu Waziri Lukuvi kufahamu anachosema juu na hao anaodai kuwa ni Waarabu na anaohofia watarudi Zanzibar.
Waarabu waliokuwa wakitawala Zanzibar ni wa kabila la Al Busaidi na Al Said. Waarabu hawa walitawala Zanzibar miaka mingi kabla ya ujio wa Ukristo. Wakati Ukristo ukiingia Zanzibar uliukuta Uislamu kwa miaka zaidi ya 800. Ni Sultan wa Zanzibar (Muarabu) ndiye aliyewapa kiwanja Mapadre cha kujenga Kanisa na akawapa pia saa kubwa iliyowekwa juu ya mnara wa Kanisa. Ndugu Lukuvi ukijikumbusha hayo utafahamu vema Uislamu unavyowatazama Wakristo, si maadui ni marafiki na hata ni ndugu.
Tunaomba Ndugu Lukuvi afahamu kuwa Waarabu waliokuwa wakitawala Zanzibar hawawezi, hawana mpango wala nia ya kurejea kutawala Zanzibar. Wakafuate nini Zanzibar? Ukoo uliokuwa ukitawala Zanzibar hivi sasa unatawala Dola ya Usutani wa Oman. Kiongozi wa Dola hiyo ni Sultan Qaboos bin Said Al Said.
Napenda nimjuze Waziri wetu kuwa historia inatukumbusha kuwa Dola ya Oman ilikuwa Dola kubwa miongoni mwa Dola za Kiarabu. Enzi za utawala wa Masultani wawili ndugu, Yolanda na Jolanda, Oman ilikuwa ni pamoja na nchi zote zinazofahamika sasa kama nchi za Umoja wa Falme za kiarabu ambazo ni pamoja na Abu Dhabi, Umm al-Quwain, Ras al-Khaimah, Sharjah, Dubai na Ajman. Usultani wa Umani ulianza miaka ya 751 na Al Said umeanzia mwaka 1744 na ungali ukiendelea hadi sasa.
Falme za Kiarabu zimekuwa nchi tajiri hivi sasa kutokana na akiba kubwa za mafuta ya petroli. Utajiri huu unapatikana kwa viwango tofautitofauti kati ya nchi za Imarat zinazounda shirikisho hili. Abu Dhabi ikiwa ni mwanachama mkubwa na kiongozi wa huo muungano ina pia kiasi kikubwa cha petroli na mapato makubwa kutokana na mauzo ya mafuta.
Kama Sultan Qaboos angekuwa na tamaa na kutaka kutawala, kwanini asigombee kurejeshewa ardhi zake ambazo hivi sasa zimeganywa katika mataifa madogo madogo na sasa yanatajwa kuwa tajiri, badala yake aje akagombee kurejea kutawala Zanzibar? Kwani Zanzibar kuna nini cha kuisaidia Oman?
Aidha kwanini Waarabu wa Oman watoke maelfu ya kilometa kuja Zanzibar badala ya kupigania nchi yao iliyojaa utajiri wa mafuta ambayo imegawanywa vipande vipande na ambayo hawahitaji kusafiri ili kuikomboa? Je watu hawa wana azma kweli ya kupanua himaya yao kama anavyosema Lukuvi?
Ni vizuri kufahamu pia Sultan Qaboos bin Said ni kiongozi ambaye anaheshimika na kusifika kwa utawala wake wenye kuzingatia haki na uadilifu na asiyependa mapambano wala siasa za kujitukuza na kujitanua. Sultan Qaboos amekuwa msuluhishi mkubwa sana katika eneo la Ghuba ya Uajemi kwa matatizo na hitilifu zinazoyakumba mataifa ya kiarabu.
Sultan Qaboos katika utawala wake amefanikiwa kujenga nchi yake ya kuboresha kiwango cha maisha ya wananchi wake kwa kiasi kwamba ni vigumu katika nchi ya Oman kutambua nyumba anayoishi ndani yake masikini na tajiri.
Mfamle Qaboos ni mtawala mwenye kujali na kusikiliza kwa nia ya kutatua matatizo ya raia wake, na kwa nia hiyo amejiwekea ratiba ya kutembelea vijijini nchini mwake, ambako huko hukaa katika mahema majangwani. Akiwa mikoani hukutana na wakuu wa Makabila (machifu) na kupata fursa na kusikiliza vilio vya raia wa ngazi ya chini kabisa uso kwa uso. Akiwa Muscat Sultan hukutana na wananchi karibu kila siku na kusikiliza shida zao na kuzipatia ufumbuzi wa papo kwa hapo.
Hali hii imepelekea Sultan Qaboos kuwa kipenzi cha Waomani kwa kiasi kwamba ukitembelea nchi hiyo huwezi kukutana na Muoman ambaye anamlaani, kumpinga, kumlaumu au kulalamika juu Sultan Qaboos wala kusema maneno ya fedhuli dhidi yake na kila raia anamuombea dua njema.
Hali hiyo ni tofauti na hapa nchini ambapo moja ya sifa yetu watanzania ni kuwatukana, kuwadhalilisha na kutokuwa na adabu na viongozi wetu. Mimi binafsi nasoma kila siku gazeti moja ambalo lina ukurasa maalum kwa ajili ya kumtukana na kumdhalilisha Rais Jakaya Kikwete binafsi, sijakwambia Mawaziri wake.
Wakati Rais Kikwete akigombe muhula wa pili baadhi ya ndugu zake Lukuvi wakristo walitoa mwito wa kukesha makanisani usiku wa kuamkia kupiga kura na kulishana kiapo cha kutomchagua JK kwa sababu ya chuki kwa nini atawale mwislamu. Ukiwa Serikalini bila shaka unajua jambo hili na mengine mengi ambayo hapa si wakati wake.
Oman nchi ambayo ardhi yake imetawaliwa na majabali, haina mito, maziwa wala mvua, haina taabu ya maji kama iliyopo Tanzania ambayo ina mito, mabwawa, maziwa, maji mengi chini ya ardhi na pia bahari. Miundo mbinu ya barabara imezunguka nchi nzima huku zikijengwa bara bara za kisasa za juu (flyovers) ambazo Tanzania hadi tunafikisha miaka 50 ya uhuru hakuna hata barabara moja kama hiyo. Mjini Muscat kuna barabara kama hizo zaidi ya kumi na mwishoni mwa mwaka huu zinatazamiwa kufikia 20 kwa mji mmoja tu.
Mfalme Qaboos katika kuboresha hali ya maisha ya wananchi wake anatoa elimu bure na kugharamia elimu ya juu nje ya nchi kwa gharama za serikali. Kima cha chini kabisa cha Muomani Serikalini ni Riyale za kiomani 381 ambazo ni sawa na shilingi za Tanzania 1,562,000/=. Aidha kima cha chini katika sekta binafsi ni Riyale 325 ambazo ni sawa na zaidi ya shilingi za Tanzania 1,330,000/=.
Muomani ambaye anafanya kazi anaruhusiwa bila pingamizi lolote kuchukua mkopo wa gari na nyumba, ambapo mkopo wa nyumba utadumu kwa miaka 20 ya mkopaji na endapo mkoapaji atafariki wakati wowote baada ya kupokea mkopo wake wa nyumba, basi Benki haina haki ya kupokea marejesho kutoka kwa warithi. Watu wanaoishi katika hali kama hiyo Ndugu Lukuvi wanakuja kutawala Zanzibar ili wapate kitu gani?
Pamoja na kuanzishwa mataifa mengine ndani ya ardhi ya Oman Sultan Qaboos pia amesamehe ardhi ya nchi yake iliyoporwa kimabavu na watawala wa ukoo Al Saud wanaotawala hivi sasa Saudi Arabia. Sultan Qaboos amesamehe ardhi hiyo huku dunia ikijua kuwa imevamiwa na watawala wa Saudia kwa tamaa ya mafuta yaliyopo katika eneo hilo. Ikiwa hali ya mambo ni kama hivyo tunawadanganyaje wananchi kuwa Waomani watarudi Zanzibar wakiwa wanakuja kuanzisha siasa kali ili kuhatarisha Maisha ya akina Lukuvi? Ama kweli chuki ya kidini humpeleka mtu mbali na ukweli!
Sasa tuangalie nchini Oman kwenyewe ambako watu wengi wana uhusiano na Tanzania Bara na visiwani. Kwanza lazima tukiri kuwa watu wa Oman na Tanzania wana uhusiano wa karibu sana na wa kidugu. Wako Waomani Waarabu waliozaliwa na mama wa kiafrika na pia wapo wale ambao baba zao ni waafrika na mama zao ni waarabu. Watu kama hawa mahala ambapo uadilifu unatawala ni raia wa nchi zote mbili.
Ndugu mmoja alipokuwa Marekani akisoma na mkewe walibahatika kupata mtoto huko Marekani na kisha baada ya masomo yao walirejea nyumbani. Baada ya miaka mingi kupita binti yao huyo alikwenda kwenye ubalozi wa Marekani kuomba visa ya masomo na akaacha hati yake ya kusafiria ubalozini hapo. Aliporudi kuchukua visa aliambiwa kuwa Marekani haiwezi kumpa visa raia wake anapotaka kwenda nyumbani. Na hii ilitokana na kumbukumbu kuonyesha kuwa binti huyo alizaliwa Marekani kwa hivyo ana haki zote za Taifa hilo.
Hivi ndivyo ilivyostahili kuwa baina ya Waarabu wenye asili ya Omani ambao walizaliwa Tanzania badala ya Sera mbovu za Ndugu Lukuvi za kujaribu kuwatisha wananchi kwa kulifanya jina la mwarabu kuwa tishio kwa amani na usalama wa nchi yetu badala ya ndugu. Hawa ni ndugu zetu na hawawezi kamwe kuisahau Tanzania na lazima watakuja kwani hapa ni kwao na wana haki japo Serikali kwa chuki za Wakristo wenye ushawishi Serikalini wanajaribu kupandikiza chuki na kuweka vikwazo.
Wakoloni daima huzivamia nchi zetu kwa nia ya kutaka kupora utajiri wetu wa mailiasili. Ukoo wa Al Said na Al Busaidi hauwezi kurejea Zanzibar kwa kuwa hakuna wanachokihitaji huko. Na ikiwa hali ya Omani ni nzuri kiuchumi na kuna Serikali inayosimamia vema mapato ya nchi, Waomani wanaoingia Zanzibar wanafanya hivyo kwa kuwa zanzibar ni kwao walikozaliwa na wala si kwa ajili ya kupelekea Uislamu ambao Lukuvi anauchukia.
Ni jambo lililo wazi kuwa Wazanzibari wenye asili ya Oman wameisaidia sana Zanzibar kwa kuingiza mitaji na kuanzisha miradi mbai mbali ya kiuchumi ambayo kwa kiasi kikubwa imesadia kupunguza hali ya ufakiri na umasikini baina ya wazanzibari na kuboresha hali za maisha yao. Labda kinachomkera Lukuvi ni kuona Waislamu Zanzibar hali zao zinaimarika huko Zanzibar na kwa kiwango fulani kufeli njama za kuuangamiza Uislamu kwa kuanzisha kila mahala Makanisa ambayo hata hivyo hayana wa kusali ndani yake.
Nimalize ''Ujumbe wa Ijumaa'' kwa kutoa tamko ambalo majibu yake yataleta natija ya maudhui hii kwa kusema, Nawaomba viongozi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano. Kama wao hawana wakati wa kujibishana na sisi mnaotuita "SIASA KAli" basi niwaombe viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndugu Abdurahmani Kinana na Ndugu Nape Nnauye watupe ufafanuzi Waislamu ambao tumekerwa sana na Maneno ya Kada wenu Ndugu William Lukuvi.
Ndugu Lukuvi amesema kuwa Serikali ya Muungano imeing'ang'ania Zanzibar kwa hofu kuwa Zanzibar ikiachwa ijitawale, kwa kuwa Wazanzibari asilimia 95 ni Waislamu, itatangaza Serikali ya Kiisalamu ambayo italeta Siasa kali ambazo zitahatarisha amani ya Tanganyika. Tunaomba kujua hiyo ndiyo sera ya CCM au Serikali yake au chuki za kidini za Lukuvi binafsi?
Jibu la swali hilo kwa Waislamu wa Tanzania litatusaidia Waislamu kufahamu kama CCM ni adui wa waislamu ili nasi tujue tunashika njia gani kwa kuwa Uislamu unatufundisha kuchukua tahadhari tena kubwa sana kwa adui yako hasa anayeichukia dini yako.
Wabillahi taufiq
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments